Na. James
K. Mwanamyoto-Mara
Tarehe 07 Oktoba, 2021
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Mohamed Mchengerwa amewataka Watumishi wa Umma nchini kuwa
wanyenyekevu wanapotoa huduma kwa wananchi ili wawe na imani na Serikali yao.
Mhe.
Mchengerwa ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Watumishi wa Umma wa Mkoa wa
Mara wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa
Umma mkoani humo.
Mhe.
Mchengerwa amesema Watumishi wa Umma hawana budi kuwatumikia wananchi kwa
unyenyekevu, uadilifu na moyo wa upendo kwani wameajiriwa kwa ajili ya
kuwatumikia wananchi.
“Fanyeni kazi
kwa uadilifu, kazi tunazozifanya ni kwa ajili ya kuwatumikia wananchi,
tumeajiriwa na wananchi, nchi hii ni ya wananachi, tujishushe kwa wananchi,
tutekeleze majukumu yetu, tujenge matumaini kwa wananchi, tuwatembelee
kusikiliza changamoto zao kwani tusipofanya hivyo tutakuwa hatuwatendei haki,”
Mhe. Mchengerwa amesisitiza.
Ameongeza
kuwa, hakuna atakayedumu katika kazi kwani kila mmoja anapita, hivyo ni vema
tufanye kazi zetu kama ibada hasa katika kuwahudumia wananchi ili hata
ukiondoka kwenye nafasi yako ukumbukwe kwa mema.
Amewasihi watumishi
wanapotekeleza majukumu yao kushirikiana na wananchi hasa katika kutoa taarifa ya
miradi mbalimbali inayotekelezwa ili wajue ni nini kinaendelea katika maeneo
yao.
Mhe.
Mchengerwa amesema, Serikali inatamua haki za wananchi hivyo watumishi wa umma tufanye
kazi kwa bidii na uadilifu ikiwemo kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo na
kuhakikisha fedha za miradi zinazotolewa zinafanya kazi iliyokusudiwa.
Mhe.
Mchengerwa ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Samia Suluhu
Hassan inatekeleza miradi mingi ya maendeleo na kutoa mfano wa madarasa 15,000 ambayo
Serikali inaenda kuyajenga hivyo amewasisitiza Watumishi kusimamia kikamilifu
fedha zitakazotolewa, ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Mohamed Mchengerwa akisalimiana na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Mkoa wa Mara apowasili Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara kuanza ziara
yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma mkoani humo.
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Mohamed Mchengerwa akizungumza na Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Mara wakati wa ziara
yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma mkoani humo.
Sehemu ya
Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Mara wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa
(hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi ya
kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma mkoani humo.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Bw. Msongela Palela akiwasilisha hoja kwa Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Mohamed Mchengerwa (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara
yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma mkoani humo.
No comments:
Post a Comment