Tarehe 06 Oktoba, 2021
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Mohamed Mchengerwa amewaelekeza Waratibu wa TASAF wilayani Sengerema
kuwaandikisha walengwa wenye sifa ya kunufaika na Mpango wa Kunusuru Kaya maskini
katika kata ya Nyamatongo ambao walisahaulika wakati wa zoezi la uhakiki na
uandikishaji.
Mhe.
Mchengerwa ametoa maelekezo hayo akiwa Wilayani Sengerema Kata ya Nyamatongo, wakati
wa ziara yake ya kikazi ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF
wilayani humo.
Katika
kuhakikisha anatimiza azma ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya kuzifikia kaya
zote maskini nchini, ameutaka uongozi wa Wilaya, Mkoa na TASAF Makao Makao
kufanya ufuatiliaji wa karibu ili kujiridhisha na utekelezaji wa agizo lake.
“Waandikisheni
wote wanaodai kusahaulika na mhakikishe mnajiridhisha kama wana sifa za kuwa walengwa
na mniwasilishie taarifa ya utekelezaji wa agizo langu ndani ya wiki mbili,”
Mhe. Mchengerwa amesisitiza.
Ameongeza
kuwa, ndani ya wiki hizo mbili Waratibu wahakikishe wanafanya mapitio ili
kujiridhisha kama waliojiandikisha wamekidhi vigezo na sifa za kuwa wanufaika
wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali.
Aidha, Mhe.
Mchengerwa amewataka wananchi wa kata ya Nyamatongo kuendelea kuwa na imani na
Serikali ya Awamu ya Sita, kwani ofisi yake itaendelea kutekeza jukumu la
usimamizi wa TASAF kikamilifu ili kuunga Mkono kwa vitendo kaulimbiu ya Mhe.
Rais Samia Suluhu Hassan ya KAZI IENDELEE.
Kwa upande
wake, Mbunge wa Sengerema Mhe. Tabasamu Hamisi amemshukuru Mhe. Mchengerwa kwa
hatua hiyo na kuongeza kuwa, kaya maskini ambazo hazijaandikishwa zimeibua
malalamiko katika jimbo analoliongoza.
Kufuatia
hatua iliyochukuliwa na Waziri mwenye dhamana ya usimamizi wa TASAF, Mhe.
Tabasamu amewahakikishia wananchi wa jimbo lake kuwa walengwa wote
waliosahaulika wataandikishwa kama ambavyo Mhe. Mchengerwa ameelekeza.
Mhe.
Tabasamu amesema, jimbo la Sengerema na Buchosa lina wazee zaidi ya elfu tisini
lakini wazee wanaonufaika na mpango wa TASAF hawazidi elfu kumi na tatu hivyo
agizo la Mhe. Mchengerwa ni muafaka wa changamoto hiyo.
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Mohamed Mchengerwa amefanya ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya
TASAF wilayani Sengerema, mara baada ya Mbunge wa Sengerema Mhe. Hamis Tabasamu
kuwasilisha malalamiko ya wananchi wa jimbo lake kutoandikishwa kwenye mradi wa
TASAF.
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Mohamed Mchengerwa akilakiwa na wananchi na wanufaika wa TASAF wa Kata ya Nyamatongo
wilayani Sengerema wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutembelea na kukagua
utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani humo.
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Mohamed Mchengerwa akizungumza na wananchi na wanufaika wa TASAF wa Kata ya Nyamatongo
wilayani Sengerema wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutembelea na kukagua
utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani humo.
Sehemu ya
wananchi na wanufaika wa TASAF wa Kata ya Nyamatongo wilayani Sengerema
wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza
nao wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa
miradi ya TASAF wilayani humo.
Kaimu Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mhe. Amina
Makilagi akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed
Mchengerwa kuzungumza na wananchi na wanufaika wa TASAF wa Kata ya Nyamatongo
wilayani Sengerema wakati wa ziara ya kikazi ya waziri huyo ya kutembelea na
kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani humo.
Mbunge wa Jimbo
la Sengerema, Mhe. Tabasamu Hamisi akielezea hali ya utekelezaji wa TASAF
katika Jimbo lake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe.
Mchengerwa ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani
Sengerema.
Mmoja wa
Maafisa wa Kata ya Nyamatongo, Wilaya ya Sengerema akiandika majina ya wananchi
ambao wanadai kusahaulika katika zoezi la uandikishwaji wa wanufaika wa baada
ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa kutoa maelekezo ya uandikishwaji wa wananchi hao wakati
wa ziara yake ya kikazi ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF
wilayani Sengerema.
No comments:
Post a Comment