Sunday, October 30, 2022

MHE. JENISTA AAHIDI KUTEKELEZA KIKAMILIFU JUKUMU ALILOPEWA NA MHE. RAIS KUWAHUDUMIA VIONGOZI WASTAAFU NA WAJANE WA VIONGOZI HAO IKIWA NI SEHEMU YA KUTAMBUA MCHANGO WALIOUTOA KATIKA TAIFA

 

Na. James K. Mwanamyoto-Dar es Salaam

Tarehe 30 Oktoba, 2022

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama ameahidi kuendelea kutekeleza kikamilifu jukumu la kuwatembelea na kuwahudumia Viongozi Wastaafu wa Kitaifa pamoja na Wajane wa Viongozi hao kama alivyoelekezwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango walioutoa katika taifa.

Mhe. Jenista Mhagama ametoa ahadi hiyo jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na Mama Anna Mkapa alipoenda kumtembelea nyumbani kwake ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.

Mhe. Mhagama amesema, katika kipindi ambacho anamsaidia Mhe. Rais kusimamia utumishi wa umma na utawala bora hatopenda kusikia kuwa viongozi wastaafu wa kitaifa na wajane wao wamekosa huduma wanazostahili kupatiwa na ofisi yake. 

Mhe. Mhagama amesema, amelipokea kwa furaha kubwa jukumu la kuwahudumia viongozi wastaafu na wajane wa viongozi hao, kwasababu wametoa mchango mkubwa katika kuleta amani, utulivu na maendeleo yaliyopo katika taifa.

Aidha, Mhe. Mhagama amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa nia yake ya dhati ya kuhakikisha viongozi wastaafu na wajane wa viongozi hao wanapatiwa huduma stahiki na bora, ili wawe na furaha na kutambua kuwa taifa linathamini mchango walioutoa.

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Mama Anna Mkapa, Mjane wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin William Mkapa alipomtembelea mjane huyo nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwasilisha salamu za Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa Mama Anna Mkapa, Mjane wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin William Mkapa alipomtembelea mjane huyo nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.

 

Mama Anna Mkapa, Mjane wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin William Mkapa akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama wakati waziri huyo alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.

 


 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akikagua mazingira anayoishi Mama Anna Mkapa, Mjane wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin William Mkapa alipomtembelea mjane huyo nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.


 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiangalia mazingira ya makazi ya Mama Anna Mkapa, Mjane wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin William Mkapa alipomtembelea mjane huyo nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.