Na. James K. Mwanamyoto-Arusha
Tarehe 13 Novemba, 2021
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za
Mitaa, Mhe. Abdallah Chaurembo amesema, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ana dhamira ya dhati ya kuhakikisha Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii (TASAF) unatekeleza azma ya kupambana na adui umaskini
pamoja na ujinga na maradhi ambao ni kikwazo cha maendeleo ya taifa.
Mhe.
Chaurembo amesema hayo leo akiwa kwenye ziara ya kikazi ya kamati yake, iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF
katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
Akizungumzia vita ya TASAF dhidi ya adui ujinga, Mhe. Chaurembo
amemuelekeza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye ndiye mwenye dhamana ya usimamizi
wa utekelezaji wa shughuli za TASAF kuhakikisha wanajenga uzio na mabweni ya
wanafunzi wa kiume wa Shule ya Sekondari ya Oldonyowas ili kuimarisha usalama
wa wanafunzi hao na kuondokana na tatizo la utoro kwa baadhi ya wanafunzi.
“Pamoja na kazi nzuri ya ujenzi wa madarasa, mabweni ya wanafunzi wa kike
na nyumba za Walimu katika shule hii, bado kuna kazi inatakiwa kufanyika, kama
tulivyomsikia mwakilishi wa wanafunzi akiomba wajengewe uzio na mabweni ya
wanafunzi wa kiume ili wapate mazingira rafiki yatakayowawezesha kupata elimu
bora kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla, hivyo kamati yangu inaielekeza
Serikali kuzingatia ombi hilo,” Mhe. Chaurembo amesisitiza.
Awali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa alisema, msingi wa utekelezaji wa miradi
ya TASAF ni vita dhidi ya adui wa haki ambaye amegawanyika katika sehemu kuu
tatu ambazo ni ujinga, maradhi na umaskini.
Mhe. Mchengerwa amesema ili kupambana na adui ujinga, Mhe. Rais Samia
Suluhu Hassan ametafuta fedha na kuielekeza TASAF kuangalia maeneo ambayo
watoto hawapati elimu kwasababu ya kukosa madarasa na mabweni ihakikishe
inajenga ili watoto hao waweze kupata elimu itakayowaondolea ujinga.
“Mhe. Diwani amesema, wengi wa watoto wanaosoma shule hii ya Oldonyowas ni
watoto wa wafugaji na katika nyakati hizi, wangekuwa wako porini wanasaidia
kufuga mifugo ya wazazi wao, lakini leo wako shuleni kwasababu Serikali ya
Awamu ya Sita imejenga madarasa na mabweni,” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.
Mhe. Mchengerwa ameahidi kuwa wanafunzi watakaofanya vizuri kwenye masomo katika
shule hiyo, Serikali itahakikisha inawapatia mikopo kwa asilimia mia moja ili
taifa liweze kupata Walimu, Madaktari, Wanasheria na wataalam wengine katika
kada mbalimbali wanaotokana na kaya maskini ambao watatoa mchango mkubwa katika
maendeleo ya taifa.
Mhe. Mchengerwa amesema adui namba mbili ambaye TASAF inapambana naye ni
maradhi ambapo kupitia mradi wa TASAF Awamu ya Nne uliozinduliwa hivi karibuni,
Serikali itajenga zahanati katika vijiji vyenye uhitaji ambavyo vinanufaika na
mpango huo.
Akizungumzia mapambano yanayofanywa na TASAF dhidi ya adui umaskini, Mhe.
Mchengerwa amesema, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza kaya zote maskini
zinazostahili kuingia kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ziingizwe kwenye
mpango huo ili ziweze kuboresha maisha yao.
Kwa upande wake, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amesema, utekelezaji wa miradi
inayoibuliwa na wananchi itaendelea kwasababu Waziri Mchengerwa ameelekeza
kuhakikisha kila sehemu miradi inakoibuliwa wataalam watumike vema kuwasaidia
walengwa ili miradi hiyo iwe endelevu na kuwanufaisha.
Kuhusiana na changamoto ya baadhi ya wananchi kulalamika kutoingizwa kwenye
mpango, Mhe. Ndejembi amesema, tayari Mhe. Mchengerwa ameshaelekeza Waratibu wa
TASAF warejee kwa ajili ya kujiridhisha na kuwaingiza kwenye mpango kwa wale
wenye sifa za kunufaika.
Naye Mkurugenzi
Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga amesema, TASAF itaendelea kutoa
ushirikiano wa kutosha kulingana na mahitaji yaliyopo na wako tayari kutekeleza
maelekezo ya kamati kwa ajili ya kuzinusuru kaya maskini.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Abdallah Chaurembo akizungumza
na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Oldonyowas pamoja na Wananchi wa Kijiji
cha Oldonyowas wakati wa ziara ya kikazi ya kamati yake iliyolenga kukagua
utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza
na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Oldonyowas pamoja na Wananchi wa Kijiji
cha Oldonyowas wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Utawala na Serikali za Mitaa iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF
katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi
akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Oldonyowas pamoja na Wananchi
wa Kijiji cha Oldonyowas wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Utawala na Serikali za Mitaa iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya
TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga akielezea namna TASAF ilivyowezesha
ujenzi wa madarasa, mabweni na nyumba za Walimu wa Shule ya Sekondari ya
Oldonyowas iliyoko Kijiji cha Oldonyowas wakati wa ziara ya
kikazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa iliyolenga
kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakisikiliza ushuhuda wa Mwanafunzi wa
Shule ya Sekondari ya Oldonyowas, Everlight Ayo alipokuwa akitoa ushuhuda wa
namna walivyonufaika na mradi wa TASAF wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hiyo
iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya
ya Arusha.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Abdallah Chaurembo akisisitiza
jambo kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Oldonyowas wakati wa ziara ya kikazi
ya kamati yake iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika
Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha
Oldonyowas pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Oldonyowas
wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na
Serikali za Mitaa, Mhe. Abdallah Chaurembo (hayupo pichani) alipokuwa
akizungumza nao wakati wa ziara ya kikazi ya kamati yake iliyolenga kukagua
utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya
Oldonyowas, Everlight Ayo akitoa ushuhuda wa namna walivyonufaika na mradi wa
TASAF wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali
za Mitaa, iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri
ya Wilaya ya Arusha.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa
akiteta jambo na Naibu Waziri wake, Mhe. Deogratius Ndejembi wakati wa ziara ya
kikazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, iliyolenga
kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Abdallah Chaurembo akiwa na
akiwaongoza wajumbe wa kamati yake kujionea bidhaa zinazozalishwa na walengwa
wa TASAF katika Kijiji cha Oldonyowas wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hiyo
iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya
ya Arusha.
No comments:
Post a Comment