Thursday, October 31, 2019

SERIKALI KUBORESHA MIFUMO YA UFUATILIAJI NA TATHMINI ILI KURAHISISHA UPATIKANAJI WA TAARIFA



Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Nolasco Kipanda akifunga mafunzo ya wadau yenye lengo la kuwajengea uwezo wa Ufuatiliaji na Tathmini watendaji wa Serikali yaliyofanyika jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Mikataba ya Utendaji Kazi Serikalini, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Hassan Kitenge akiwasilisha mada wakati wa mafunzo ya wadau yenye lengo la kuwajengea uwezo wa Ufuatiliaji na Tathmini watendaji wa Serikali yaliyofanyika jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya wadau yenye lengo la kuwajengea uwezo wa Ufuatiliaji na Tathmini watendaji wa Serikali wakifuatilia mada wakati wa mafunzo hayo jijini Dodoma.

Wednesday, October 30, 2019

UFUATILIAJI NA TATHMINI SERIKALINI NI CHACHU YA UTENDAJI KAZI NA UWAJIBIKAJI KWA WATUMISHI WA UMMA



Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael  akizungumza na washiriki wa mafunzo ya wadau ya siku mbili yenye lengo la kuwajengea uwezo wa Ufuatiliaji na Tathmini watendaji wa Serikali yanayofanyika jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya wadau ya siku mbili yenye lengo la kuwajengea uwezo wa Ufuatiliaji na Tathmini watendaji wa Serikali wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael (hayupo pichani) yanayofanyika jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Nolasco Kipanda akitoa neno la utangulizi wakati wa mafunzo ya wadau ya siku mbili yenye lengo la kuwajengea uwezo wa Ufuatiliaji na Tathmini watendaji wa Serikali yanayofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa “Centre for Learning on Evaluation and Results CLEAR-AA” kutoka Chuo cha Witwatersrand nchini Afrika Kusini, Prof. Dugan Fraser akiwasilisha mada wakati wa mafunzo ya wadau ya siku mbili yenye lengo la kuwajengea uwezo wa Ufuatiliaji na Tathmini watendaji wa Serikali yanayofanyika jijini Dodoma.


Tuesday, October 29, 2019

WATENDAJI SERIKALINI WATAKIWA KUFANYA MAJADILIANO NA VYAMA VYA WAFANYAKAZI KWA AJILI YA USTAWI WA WATUMISHI



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na wajumbe wa Mkutano wa Baraza Kuu la Nne la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma Tanzania Bara wakati akifungua mkutano huo jana jijini Dodoma.

Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa Baraza Kuu la Nne la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma Tanzania Bara wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) (Hayupo pichani) wakati akifungua mkutano huo jana jijini Dodoma.

Makamu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Nne la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma Tanzania Bara, Bi. Leah Ulaya akimshukuru Mhe. Mkuchika (Hayupo pichani) mara baada ya kufungua rasmi mkutano wa baraza hilo jana jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa  Mkutano wa Baraza Kuu la Nne la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma Tanzania Bara mara baada ya kufungua rasmi mkutano wa Baraza hilo jana jijini Dodoma.

Friday, October 25, 2019

MKURABITA YATAKIWA KUHAKIKISHA HATIMILIKI ZA KIMILA ZINATUMIKA KUWAPATIA MIKOPO WANUFAIKA WA MPANGO HUO ILI WAJIENDELEZE KIUCHUMI




Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Brigedia Jenerali Nicodemus Mwangela akimkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) katika mkoa wake jana kabla ya Naibu Waziri huyo kuanza ziara ya kikazi mkoani humo ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA).

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na baadhi ya Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba na Tunduma mkoani Songwe jana wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) na kuzungumza na watumishi.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akimsikiliza Mkuu wa Idara ya Ardhi, Bw. Kelvin Joseph alipokuwa akitoa maelezo ya utekelezaji wa Mradi wa urasimishaji mashamba ya wakulima katika Kijiji cha Naming’ongo wilayani Momba Mkoa wa Songwe wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo jana ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA). Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Juma Irando.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akitoa maelekezo ya namna ya kuwaunganisha wanufaika wa MKURABITA na taasisi za fedha ili waweze kupata mikopo na kujiinua kiuchumi wakati Naibu Waziri huyo aliposimama kukagua utekelezaji wa Mradi wa urasimishaji mashamba ya wakulima katika Kijiji cha Naming’ongo wilayani Momba Mkoa wa Songwe katika ziara yake ya kikazi mkoani humo jana ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA). 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na wanufaika wa  Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) wa Kijiji cha Naming’ongo wilayani Momba Mkoa wa Songwe wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo jana ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Mpango huo.



Friday, October 18, 2019

WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUENDANA NA WAKATI KIUTENDAJI



Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanri akielezea historia fupi ya Mkoa wa Tabora kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg walipomtembelea ofisini kwake jana kabla ya kutembelea Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Tabora kwa lengo la kuona maendeleo ya chuo hicho kilichojengwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Sweden mwaka 1970. Kushoto kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mjini, Mhe. Kitwala Komanya.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanri na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg kuingia Chuo cha Utumishi wa Umma Kampasi ya Tabora jana kwa lengo la kuona maendeleo ya chuo hicho kilichojengwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Sweden mwaka 1970. Kulia kwa Mkuu wa Mkoa ni Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Emmanuel Shindika.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb), Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanri na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg wakiungana na wanafunzi na watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Tabora na wageni wengine kucheza muziki uliokuwa ukitumbuizwa na bendi ya Msange JKT wakati wageni hao walipotembelea Chuo cha Utumishi wa Umma Kampasi ya Tabora jana kwa lengo la kuona maendeleo ya chuo hicho kilichojengwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Sweden mwaka 1970. Kulia kwa Mkuu wa Mkoa ni Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Emmanuel Shindika.

Mkufunzi Msaidizi wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Tabora, Bw. Alex Massengo akiwaonyesha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb), Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanri na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg matukio mbalimbali katika picha yakiwemo yanayohusu ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Sweden katika kujenga Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Tabora wakati wageni hao walipotembelea Chuo cha Utumishi wa Umma Tawi la Tabora jana kwa lengo la kuona maendeleo ya chuo hicho.

Mkuu wa Idara ya Uhazili,  Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Tabora, Bw. Given Simkwai akiwaonyesha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb), Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanri na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg umuhimu wa  matumizi ya hati  mkato wakati wageni hao walipotembelea Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Tabora jana kwa lengo la kuona maendeleo ya chuo hicho kilichojengwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Sweden mwaka 1970.

Meneja wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Tabora, Bi. Felister Akonaay akiwaonyesha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg kibao kinachoonyesha ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Sweden katika kujenga Chuo cha Utumishi wa Umma, Tawi la Tabora wakati wageni hao walipotembelea Chuo hicho jana kwa lengo la kuona maendeleo yake.

Tuesday, October 15, 2019

SWEDEN YAIPONGEZA SERIKALI YA TANZANIA KWA KUFANYA VIZURI KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA




Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akimkaribisha Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg alipotembelea Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Kampasi ya Dar es Salaam jana kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya Utumishi wa Umma kwa nchi za Sweden na Tanzania.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg wakishuhudia jinsi mashine ya kupiga chapa inavyofanya kazi mara baada ya Balozi kutembelea Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC)  jana kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya Utumishi wa Umma kwa nchi za Sweden na Tanzania. Wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Emmanuel Shindika


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg wakionyesha zawadi ya ramani ya Afrika yenye nembo ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania baada ya Balozi huyo kukabidhiwa zawadi hiyo na Naibu Waziri kuonyesha ushirikiano mwema baina ya Tanzania na Sweden katika masuala ya utumishi wa umma wakati Balozi aliotembelea chuoni hapo jana kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya Utumishi wa Umma kwa nchi za Sweden na Tanzania.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg wakicheza wimbo unaosifu utendaji kazi wa Marais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia Awamu ya Kwanza mpaka sasa wa kwaya ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania  wakati Balozi aliotembelea chuoni hapo jana kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya Utumishi wa Umma kwa nchi za Sweden na Tanzania. Kushoto kwa Balozi ni Kaimu Katibu Mkuu Utumishi, Bw. Mick Kiliba.

Monday, October 14, 2019

KKKT YAIPONGEZA SERIKALI KWA KULETA MAENDELEO NA KUTOA USHIRIKIANO KATIKA HUDUMA ZA KIJAMII NCHINI




Askofu wa Dayosisi ya Kusini, Awamu ya Sita Dkt. George Mark Fihavango akiipongeza Serikali kwa kuleta maendeleo nchini mara baada ya kusimikwa kuwa askofu wa Dayosisi hiyo katika Ibada takatifu iliyofanyika Mjini Njombe na kuongozwa na Mkuu wa KKKT, Askofu Dkt. Frederick Shoo (hayupo pichani).


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli katika ibada ya kumsimika Askofu wa Dayosisi ya Kusini, Awamu ya Sita Dkt. George Mark Fihavango iliyofanyika Mjini Njombe na kuongozwa na Mkuu wa KKKT, Askofu Dkt. Frederick Shoo (hayupo pichani). 

Baadhi ya waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na madhehebu mengine wakishiriki ibada ya kumsimika Askofu wa Dayosisi ya Kusini, Awamu ya Sita Dkt. George Mark Fihavango iliyofanyika Mjini Njombe na kuongozwa na Mkuu wa KKKT, Askofu Dkt. Frederick Shoo (hayupo pichani). 


Mkuu wa KKKT, Askofu Dkt. Frederick Shoo akimpongeza Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali yake kwa kuwaletea watanzania maendeleo, pongezi hizo amezitoa mbele ya waumini wa KKKT na madhehebu mengine wakati wa ibada ya kumsimika Askofu wa Dayosisi ya Kusini, Awamu ya Sita Dkt. George Mark Fihavango iliyofanyika mjini Njombe.

Sunday, October 13, 2019

KUMBUKUMBU YA MIAKA 20 YA KIFO CHA BABA WA TAIFA, MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE


SERIKALI KUZIPATIA RUZUKU KAYA ZOTE MASKINI NCHINI BAADA YA KURIDHISHWA NA MAENDELEO WANUFAIKA WA TASAF


Na James K. Mwanamyoto-Nyasa
Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) imeahidi kuzinufaisha kaya zote maskini nchini baada ya kuridhishwa na namna wananchi katika vijiji vilivyonufaika na Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini walivyoboresha maisha yao na kujikwamua katika lindi la umaskini liliokuwa likiwakabili.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) wakati akizungumza na wanufaika na wananchi wa kijiji cha Nangombo wilayani Nyasa akiwa katika ziara yake ya kikazi yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Mpango huo wilayani humo.
Mhe. Mkuchika amefafanua kuwa, iwapo wanufaika wasingetumia ruzuku vizuri kuboresha maisha, Serikali isingesita kusimamisha utekelezaji wa Mpango huu wa Kunusuru Kaya Maskini nchini.
“Hongereni wanufaika wa TASAF kijiji cha Nangombo na maeneo mengine kwa kutumia ruzuku kuboresha maisha yenu, kujenga nyumba bora, kununua vifaa vya shule kwa ajili ya watoto na kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi," Mhe. Mkuchika amepongeza.
Mhe. Mkuchika ameongeza kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano imeridhika na mafanikio yaliyopatikana, hivyo itaendeleza vita dhidi ya umaskini, lengo likiwa ni kuboresha maisha ya kaya zote maskini nchini.
Akiwasilisha taarifa ya kijiji cha Nangombo kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, Afisa Mtendaji wa kijiji hicho, Bw. Joseph P. Ngogi amesema watoto 66 wa shule wananufaika na ruzuku inayotolewa hivyo imeongeza mahudhurio shuleni na kliniki kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano, aidha kaya 65 zimeboresha makazi yao kwa kujenga ama kukarabati na kuezeka kwa bati.
Mmoja wa wanufaika wa Mpango wa TASAF kijiji cha Nangombo, Bi. Mariana Mkwaila amesema ruzuku anayoipata imemuwezesha kuwanunulia watoto wake sare za shule, viatu na madaftari ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba kubwa ambayo anatarajia kuizeka kwa bati hivi karibuni.
Naye, Bi. Elizabeth Damian amesema, alikuwa akiishi maisha ya kimaskini kwenye nyumba ya nyasi kabla ya kuingizwa kwenye Mpango, lakini baada ya kuanza kupokea ruzuku ameweza kufuga kuku, mbuzi na kufyatua tofali zilizomuwezesha kujenga nyumba iliyoezekwa kwa bati.
Mhe. Mkuchika amehitimisha ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma kwa kuitembelea Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma na kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wilayani humo.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nangombo wilayani Nyasa katika ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma na kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wilayani humo.


Baadhi ya wananchi na wanufaika wa TASAF wa kijiji cha Nangombo wilayani Nyasa wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Hayupo pichani) katika ziara ya kikazi ya Waziri huyo mkoani Ruvuma yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma na kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wilayani humo.


Mmoja wa wanufaika wa TASAF wa Kijiji cha Nangombo wilayani Nyasa, Bi. Mariana Aidani Mkwaila akitoa shuhuda ya namna alivyonufaika na ruzuku anayoipata kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji hicho.


Mnufaika  wa TASAF wa Kijiji cha Nangombo wilayani Nyasa, Bi. Elizabeth Damiani akitoa shuhuda ya namna alivyonufaika na ruzuku anayoipata kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji hicho.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akiagana na mmoja wa wanufaika wa TASAF wa kijiji cha Nangombo wilayani Nyasa mbele ya nyumba inayojengwa na mnufaika huyo kupitia ruzuku anayoipata.


Wananchi na wanufaika wa TASAF wa kijiji cha Nangombo wilayani Nyasa wakiwa katika mkutano wa  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Hayupo pichani) uliofanyika katika kijiji hicho kwa lengo la kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wilayani humo.