Tuesday, October 3, 2017

MHE. KAIRUKI AZINDUA RASMI BODI YA MISHAHARA NA MASILAHI KATIKA UTUMISHI WA UMMA



Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Bibi Mariam Mwanilwa akitoa maelezo ya utangulizi kuhusu majukumu ya Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma kabla ya kuzinduliwa rasmi kwa Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb), kuzungumza na Wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma kabla ya kuizindua rasmi Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma (hawapo pichani) kabla ya kuizindua rasmi Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akiwa katika kikao na  Wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma kabla ya kuizindua rasmi Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akimkabidhi vitendea kazi Mwenyekiti wa Bodi ya Mishahara na Masilahi Katika Utumishi wa Umma, Bw. Donald Ndagula kabla ya kuizindua rasmi Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.


Mwenyekiti wa Bodi ya Mishahara na Masilahi Katika Utumishi wa Umma, Bw. Donald Ndagula akitoa neno la shukrani mara baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) kuizindua rasmi Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Masilahi Katika Utumishi wa Umma na Watendaji wa Bodi ya Mishahara na Masilahi Katika Utumishi wa Umma mara baada ya kuizindua rasmi Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment