Thursday, October 5, 2017

MHE. KAIRUKI AZINDUA BODI YA TATU YA SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (hawapo pichani) kabla ya kuizindua rasmi Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb), kuzungumza na Wajumbe wa Bodi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kabla ya kuizindua rasmi Bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam.

 Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Xavier Daudi, akitoa maelezo ya utangulizi kuhusu majukumu ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kabla ya kuzinduliwa rasmi kwa Bodi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma  jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bibi Rose Lugembe (aliyevaa miwani) pamoja na Wajumbe wengine wa Bodi hiyo wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) alipokuwa akizungumza nao wakati wa uzindua wa Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment