Wednesday, October 11, 2017

WAZIRI MKUCHIKA (MB) AKABIDHIWA OFISI LEO, WAZIRI KAIRUKI AWAAGA WATENDAJI NA WATUMISHI WA ILIYOKUA OFISI YAKE.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro  akimkaribisha aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) katika ofisi yake ya awali, wakati wa hafla ya kukabidhi ofisi hiyo kwa anayechukua nafasi yake ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma  na Utawala Bora Mhe. Kapt.(Mstaafu) George Mkuchika aliyeapishwa mapema wiki hii.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akitoa neno la utangulizi kabla ya aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) kukabidhi ofisi kwa Waziri mteule wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma  na Utawala Bora, Mhe. Kapt. (Mstaafu) George Mkuchika (Mb).

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt. (Mstaafu) George Mkuchika  (Mb) na aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) pamoja na watendaji wa ofisi hiyo wakati wa hafla makabidhiano ya ofisi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt.(Mstaafu) George Mkuchika (Mb) akizungumza kabla ya kukabidhiwa ofisi na Waziri aliyekuwa akisimamia majukumu ya ofisi hiyo, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) mapema leo.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt. (Mstaafu) George Mkuchika akipokea taarifa ya makabidhiano ya ofisi toka kwa aliyekuwa Waziri wa ofisi hiyo, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) mapema leo. Mhe. Kairuki (Mb) sasa ni Waziri wa Wizara ya Madini.

Aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza kabla ya kukabidhi ofisi rasmi kwa Waziri mteule wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma  na Utawala Bora Mhe. Kapt.(Mstaafu) George Mkuchika (Mb).

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt. (Mstaafu) George Mkuchika (Mb) akizungumza na Vyombo vya Habari ofisini kwake mara baada ya kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa Waziri wa ofisi hiyo, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) mapema leo.


No comments:

Post a Comment