Monday, October 30, 2017

WAFANYAKAZI 143 WA OFISI YA RAIS - UTUMISHI WAHAMIA DODOMA AWAMU YA PILI

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Dorothy Mwaluko akiagana na Kiongozi wa msafara wa magari yaliyobeba nyaraka na vitendea kazi vya ofisi hiyo ikiwa ni mwendelezo wa zoezi la Serikali kuhamia Dodoma. Jumla ya wafanyakazi 143 wameagwa katika awamu hii ya pili, ambapo awamu ya kwanza waliondoka wafanyakazi 78.

Gari lililobeba nyaraka na vitendea kazi vya Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, likijiandaa kuondoka katika viwanja vya ofisi hiyo iliyopo Magogoni jijini Dar es Salaam. Jumla ya wafanyakazi 143 wameagwa katika awamu hii ya pili, ambapo awamu ya kwanza waliondoka wafanyakazi 78.

Baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakiwapungia mikono ya kwaheri madereva wa magari yaliyobeba nyaraka na vitendea kazi vya ofisi hiyo ikiwa ni mwendelezo wa zoezi la kuhamia Dodoma. Jumla ya wafanyakazi 143 wameagwa katika awamu hii ya pili, ambapo awamu ya kwanza waliondoka wafanyakazi 78.

No comments:

Post a Comment