Tuesday, September 15, 2026

NUKUU ZA LEO ZA NAIBU WAZIRI MHE. RGINA QWARAY WAKATI AKIZUNGUMZA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA BUCHOSA






 

NAIBU WAZIRI MHE. QWARAY AWAAGIZA WAAJIRI KUTATUA CHANGAMOTO ZA WATUMISHI KWA WAKATI


Na. Antonia Mbwambo na  Lusungu Helela 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina  Qwaray, amewaagiza waajiri kuhakikisha changamoto na stahiki za watumishi wa umma zinashughulikiwa kwa wakati, hatua inayolenga kuongeza ufanisi na kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Mhe. Qwaray ametoa agizo hilo leo Septemba 15, 2026  wakati akizungumza na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa mkoani Mwanza  kwa lengo la  kusikiliza changamoto za watumishi na kujadili namna ya kuboresha utendaji katika Utumishi wa Umma.

Amesema masuala yanayohusu kupandishwa vyeo, uhamisho, malimbikizo ya mishahara na mafao yanapaswa kushughulikiwa kwa wakati na mamlaka husika, badala ya kuendelea kucheleweshwa.

"Nawaagiza waajiri wote kuhakikisha changamoto na stahiki za watumishi, ikiwemo kupandishwa vyeo, uhamisho, malimbikizo ya mishahara na mafao, zinashughulikiwa kwa wakati,” amesema  Mhe Qwaray.

Aidha, amesisitiza kuwa madai ya watumishi yanapaswa kuhakikiwa ipasavyo na kuwasilishwa yakiwa na nyaraka zote muhimu ili kuwezesha malipo kufanyika kwa wakati.

Katika hatua nyingine, Mhe. Qwaray amezitaka Mamlaka za Ajira na Nidhamu kusimamia haki na wajibu wa watumishi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma, huku akiwataka kuachana na utendaji wa mazoea.

Amesema mambo yaliyo ndani ya mamlaka za waajiri na Mamlaka za Ajira na Nidhamu yanapaswa kushughulikiwa katika ngazi husika badala ya kuendelea kuwasilishwa Ofisini kwake.

Aidha, Mhe. Qwaray amesisitiza umuhimu wa watumishi kutumia mifumo ya kidijitali iliyobuniwa  na Serikali katika kusimamia utendaji na kupata huduma za kiutumishi.

Mifumo hiyo ni pamoja na e-Watumishi, Watumishi Portal, e-Utendaji (PEPMIS) na e-Mrejesho, ambayo imeimarishwa kwa ajili ya kurahisisha upatikanaji wa huduma, kuongeza uwajibikaji na kutoa fursa kwa wananchi na watumishi kuwasilisha maoni, pongezi, malalamiko na mapendekezo.

Amesema matumizi sahihi ya mifumo hiyo ni sehemu ya jitihada za kujenga Utumishi wa Umma unaozingatia haki, wajibu, uwajibikaji, ufanisi na matumizi ya teknolojia.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Buchosa, Bw. Benson Mihayo amesema changamoto za watumishi zitaendelea kushughulikiwa kutokana na bajeti iliyopo huku akibainisha kuwa mwitikio wa watumishi katika suala  ujazaji PEPMIS limekuwa na mwitikio mkubwa ukilinganisha na hapo awali  hali inayopelekea malalamiko ya watumishi kupungua wakati wa upandaji wa madaraja. 

Naye Mbunge wa Buchosa, Mhe. Erick Shigongo ametumia fursa hiyo kuwashukuru Watumishi wa Halmashauri ya Buchosa kwa huduma bora wanazoendelea kutoa kwa wananchi wa Halmashauri hiyo.

" Hatua ya maendeleo unayoyaona leo hapa Buchosa ni kutokana na uwepo wa watumishi wazalendo waliojitoa kwa lengo la kuwahudumia wananchi" amesisitiza Mhe. Shigongo 

 

Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akiwa na baadhi ya viongozi wakimsikiliza  Katibu Tawala wa wilaya hiyo  Bw. Cuthbert Midala  mara  baada ya  kumaliza   kuzungumza leo na Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Buchosa iliyopo mkoani Mwanza

 

Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akizungumza na  watumishi wa Ofisi ya Halmashauri ya Buchosa  Mkoani Mwanza mara  baada ya kuwasili leo mkoani humo kwa lengo la kuzungumza na kusikiliza changamoto zinazowakabili watumishi na kuzitafutia ufumbuzi 

 



3.    Watumishi wa Ofisi ya Halmashauri ya Buchosa iliyopo  Mkoani Mwanza wakiwa kwenye maombi kabla ya  Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray kuanza kuzungumza nao

 


Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya   Mkoa wa  Mwanza mara  baada ya kuwasili leo mkoani humo kwa lengo la kuzungumza na kusikiliza changamoto zinazowakabili watumishi na kuzitafutia ufumbuzi    
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akizungumza na  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CP Salum Hamduni  mara  baada Naibu Waziri huyo  kuwasili mkoani humo kwa lengo la kuzungumza na kusikiliza changamoto zinazowakabili watumishi na kuzitafutia ufumbuzi.  

Monday, September 14, 2026

MRADI WA TANZANIA YA KIDIJITALI UMELETA MAPINDUZI MAKUBWA YA MAWASILIANO YA KIMTANDAO YALIYORAHISISHA UTOAJI WA HUDUMA KWA UMMA

Na. Veronica Mwafisi-Dar es Salaam

Mradi wa Tanzania ya Kidijitali (DTP) umeleta mapinduzi makubwa ya mawasiliano ya kimtandao yaliyorahisisha utoaji wa huduma za serikali kwa wananchi.

Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Priscus Kiwango ameyasema hayo alipokuwa akimwakilisha Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wakati wa kikao kilicholenga kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Bw. Kiwango amesema kupitia DTP, miradi mingi imetekelezwa na kuleta mafanikio makubwa ikiwemo minara ya simu iliyopelekwa kwenye maeneo mengi ya vijijini ambayo mawasiliano yalikuwa hayapatikani na kwa sasa yanapatikana kwa ubora wa 3G na 4G.

Vilevile amesema, mradi huo umeweka Mawasiliano ya kimtandao kwenye Taasisi za Serikali ikiwemo kwenye Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa ajili ya kutumia mifumo mbalimbali ya serikali kidijitali.

Bw. Kiwango ameongeza kuwa, mradi huo umeleta mafanikio makubwa ya kuunganishwa kwa mifumo mingi ya Serikali ambayo ilikuwa ni maelekezo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kubadilishana taarifa kwa taasisi za umma.

Aidha Bw. Kiwango amesema, kupitia mradi huo, Mfumo unaotumika na Taasisi za Umma Kupima Utendaji Kazi wa Watumishi wa Umma (PEPMIS) umetekelezeka.


Bw. Kiwango ametaja mafanikio mengine ya mradi huo wa DTP kuwa ni kupatikana kwa Mfumo wa Daftari la Huduma za Serikali (GSD) unaowawezesha wananchi, wafanyabiashara na wageni kupata taarifa mbalimbali za huduma za serikali katika Wizara, Idara, Wakala, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa hivyo, kurahisisha utoaji wa huduma kwa umma kwa njia ya kidijiti.

 

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi huo ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bw. Bakari Mwamgugu, amesema lengo kuu la mradi huo ni kupeleka mawasiliano sehemu ambazo hazikuwa na mawasiliano na kuboresha huduma bora kwa mwananchi kidijitali.

 

Ameongeza kuwa, Minara 304 imeboreshwa kutokana na mabadiliko ya teknolojia kutoka kwenye 2G Kwenda kuwa na 3G na 4G.

 

Mradi wa Tanzania ya Kidijitali ulianza mwaka 2021 na unatarajia kukamilika mwaka huu 2026.


Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye ni Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Priscus Kiwango akizungumza wakati wa kikao kilicholenga kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washiriki wa kikao kilicholenga kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali wakimsikiliza Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye ni Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini, Bw. Priscus Kiwango (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam.


Mwakilishi kutoka Benki ya Dunia, Bw. Paul Seadin akizungumza wakati wa kikao kilicholenga kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali kilichofanyika jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya washiriki wa kikao kilicholenga kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali wakimsikiliza Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye ni Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini, Bw. Priscus Kiwango (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya washiriki wa kikao kilicholenga kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali wakifuatilia jambo wakati wa kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya washiriki wa kikao kilicholenga kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali wakifuatilia jambo wakati wa kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya washiriki wa kikao kilicholenga kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali wakijadili jambo wakati wa kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi Msaidizi wa Anuai za Jamii, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bi. Mwanaamani Mtoo (kushoto) akifuatilia jambo wakati wa kikao cha kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali kilichofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa Kituo cha Utafiti, Ubunifu na Uendelezaji wa Serikali Mtandao, Dkt. Jaha Mvulla.


Baadhi ya washiriki wa kikao kilicholenga kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali wakifuatilia jambo wakati wa kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam.


Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye ni Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Priscus Kiwango (waliokaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora (waliosimama) baada ya kikao kilicholenga kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali kilichofanyika jijini Dar es Salaam.


Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye ni Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Priscus Kiwango (waliokaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki (waliosimama) wa kikao kilicholenga kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali kilichofanyika jijini Dar es Salaam.


Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakifuatilia jambo wakati wa kikao cha kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali kilichofanyika jijini Dar es Salaam


Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye ni Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Priscus Kiwango (waliokaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kikao kilicholenga kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali kilichofanyika jijini Dar es Salaam.