Wednesday, February 8, 2017

UTUMISHI YATOA UFAFANUZI KUHUSU MWONGOZO WA KUDHIBITI VVU,UKIMWI NA MAGONJWA SUGU YASIYOAMBUKIZWA MAHALI PA KAZI KATIKA UTUMISHI WA UMMA KATIKA KIPINDI CHA MORNING TRUMPET KINACHORUSHWA NA AZAM TV

Mtangazaji wa Kipindi cha “Morning Trumpet” kinachorushwa na AZAM TV, Bw. Faraja Sendegeya (kushoto) akifanya mahojiano na Mkurugenzi kutoka Kitengo cha Anuai za Jamii cha Ofisi ya Rais -Utumishi Bi. Anne Mazalla . Kipindi hicho kililenga kutoa elimu kwa umma juu ya masuala anuai za jamii na kilirushwa mapema leo.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Anuai za Jamii Bi. Anne Mazalla wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma (wa pili kutoka kulia) akifafanua jambo kuhusiana na masuala mbalimbali ya Anuai za Jamii wakati wa Kipindi cha “Morning Trumpet “ kinachorushwa na AZAM TV kilichofanyika mapema leo. Wengine ni Kamishna kutoka Idara ya Uhamiaji Bi. Salome Kahambwa (wa pili kutoka kushoto),Mtangazaji wa kipindi hicho Bw. Faraja Sendegeya (kushoto) na mgeni wa kipindi Bi. Noela Mahuvi (kulia).

Thursday, February 2, 2017

MHE. KAIRUKI AZINDUA RASMI, OFISI YA RAIS –UTUMISHI NA UTAWALA BORA ILIYOPO MAKAO MAKUU YA NCHI DODOMA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na Vyombo vya Habari kabla ya kuzindua rasmi utoaji wa huduma wa ofisi yake iliyopo Makao Makuu ya Nchi Dodoma. Wengine ni baadhi ya Watumishi wa ofisi hiyo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akikata utepe kuzindua rasmi ofisi yake iliyopo Makao Makuu ya Nchi Dodoma. Wanaoshuhudia ni watumishi wa ofisi hiyo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Bw. Mathias Kabunduguru mara baada ya kuzindua rasmi huduma za ofisi hiyo.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Prof. Idris Kikula akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) mara baada ya kumtembelea waziri huyo ofisini kwake. Wanaoshuhudia ni baadhi ya waandishi wa habari na watumishi wa ofisi hiyo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akijionea moja ya shubaka linalotumika  kutunzia majalada katika masijala ya ofisi yake, mara baada ya kuzindua utoaji wa huduma wa ofisi hiyo iliyopo Makao Makuu ya Nchi Dodoma. Wanaoshuhudia ni baadhi ya watumishi wa ofisi hiyo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Prof. Idris Kikula.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa ofisi yake iliyopo  Makao Makuu ya Nchi Dodoma, mara baada ya kuzindua rasmi utoaji wa huduma wa ofisi hiyo. Aliyejumuika nao ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Prof. Idris Kikula (Wapili kutoka kulia).

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Prof. Idris Kikula akizungumza na Vyombo vya Habari mara baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) kuzindua rasmi ofisi yake iliyopo katika jengo la Kitivo cha Sanaa na Sayansi Jamii lililopo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Muonekano halisi  wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora iliyopo katika jengo la Kitivo cha Sanaa na Sayansi Jamii Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), mara baada ya ofisi hiyo kuzinduliwa rasmi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb).