Wednesday, February 5, 2025

OFISI YA RAIS-UTUMISHI NA AFISI YA RAIS, KATIBA, SHERIA, UTUMISHI NA UTAWALA BORA (SMZ) YAFANYA KIKAO KAZI CHA MASHIRIKIANO KUHUSU MASUALA YA UTUMISHI



Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Cyrus Kapinga akizungumza wakati wa kikao kazi cha kuimarisha ushirikiano katika masuala ya kiutumishi kati ya ofisi hiyo na Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora (SMZ) kilichofanyika jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti, Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora (SMZ), Bw. Said Salim akizungumza wakati wa kikao kazi cha kuimarisha ushirikiano katika masuala ya kiutumishi kati ya ofisi hiyo na Ofisi ya Rais-UTUMISHI kilichofanyika jijini Dodoma.


Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora (SMZ) wakiwa kwenye kikao kazi kilicholenga kuimarisha ushirikiano katika masuala ya kiutumishi kilichofanyika jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Magufuli (aliyenyoosha mkono) akichangia hoja wakati wa kikao kazi cha ofisi hiyo na Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora (SMZ) kilicholenga kuimarisha ushirikiano katika masuala ya kiutumishi kilichofanyika jijini Dodoma.


Sehemu ya Wakurugenzi kutoka Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora (SMZ) wakifuatilia kikao kazi kilicholenga kuimarisha ushirikiano katika masuala ya kiutumishi kati ya ofisi hiyo na Ofisi ya Rais-UTUMISHI kilichofanyika jijini Dodoma.

Sehemu ya Wakurugenzi kutoka Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora (SMZ) wakifuatilia kikao kazi kilicholenga kuimarisha ushirikiano katika masuala ya kiutumishi kati ya ofisi hiyo na Ofisi ya Rais-UTUMISHI kilichofanyika jijini Dodoma.


Katibu Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma – Zanzibar, Bi. Asma Jidawy (wa kwanza kushoto) akiwasilisha hoja wakati wa kikao kazi kilicholenga kuimarisha ushirikiano katika masuala ya kiutumishi kwa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora (SMZ) kilichofanyika jijini Dodoma.

Sehemu ya Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifuatilia kikao kazi kilicholenga kuimarisha ushirikiano katika masuala ya kiutumishi kati ya ofisi hiyo na Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora (SMZ) kilichofanyika jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, SACP. Ibrahim Mahumi akifafanua hoja wakati wa kikao kazi kilicholenga kuimarisha ushirikiano katika masuala ya kiutumishi kati ya ofisi hiyo na Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora (SMZ) kilichofanyika jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA Serikalini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Priscus Kiwango akielezea kuhusu mifumo mbalimbali ya kiutumishi inayotumika katika utendaji kazi wakati wa kikao kazi cha ofisi hiyo na Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora (SMZ) kilichofanyika jijini Dodoma.

 

 




WAELIMISHA RIKA OFISI YA RAIS-UTUMISHI WATAKIWA KUTOA ELIMU KUHUSU UIMARISHAJI WA AFYA KWA WATUMISHI

 Na. Mwandishi Wetu-Dodoma

Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Uendelezaji Sera, Sehemu ya Anuai za Jamii, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Mwanaamani Mtoo ametoa wito kwa Waelimisha Rika wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI kutoa elimu kwa watumishi walio kwenye Idara na Vitengo vya Ofisi hiyo namna ya kutunza na kuimarisha afya ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi kwa masilahi mapana ya  taifa.

Bi. Mtoo ametoa wito huo jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo yaliyotolewa kwa Waelimisha Rika hao yaliyolenga kuwajengea uwezo katika kutekeleza majukumu yao.

Amesema kuwa Waelimisha Rika katika ofisi ni watu muhimu hivyo mafunzo hayo yatawasaidia kufahamu mbinu mbalimbali za kutumia katika utoaji wa elimu na namna ya kuimarisha afya za watumishi wenzao ili ziwasaidie katika kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa kuzingatia utunzaji ya afya bora.

“Ninyi ni watu muhimu sana katika ofisi zetu, naamini mafunzo haya yatawajengea uwezo mkubwa wa kutoa elimu na kuwaelekeza watumishi wenzenu namna ya kutunza na kuimarisha afya iliyo bora, na hapa niwakumbushe kuzingatia lishe iliyo bora ili muweze kutekeleza majukumu ya taifa,” Bi. Mtoo amesema.

Akiwasilisha mada kuhusu lishe bora, Afisa Lishe kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Bi. Nusrat Rubambura amesisitiza masuala ya kuzingatia katika kuimarisha afya ikiwemo kufanya mazoezi, kunywa maji ya kutosha pamoja na kula vyakula mchanganyiko kutoka katika makundi sita ikiwemo nafaka, mizizi na ndizi za kupika, asili ya wanyama, jamii ya kunde, mbogamboga, matunda na Mafuta salama.

Akizungumza kwa niaba ya Waelimisha Rika hao, Mwenyekiti wa Waelimisha Rika Bw. Kokolo Lusanda ameahidi watashirikiana katika kutoa elimu kwa watumishi wenzao ili kuzingatia utunzaji wa afya zao na kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

 

Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Uendelezaji Sera, Sehemu ya Anuai za Jamii, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Mwanaamani Mtoo akisisitiza jambo wakati akifungua mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo Waelimisha Rika wa Idara na Vitengo vya ofisi hiyo ili kupambana na Afua za VVU, UKIMWI na Magonjwa Sugu Yasiyoambukiza mahali pa kazi.


Sehemu ya Waelimisha Rika, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo Waelimisha Rika wa Idara na Vitengo vya ofisi hiyo ili kupambana na Afua za VVU, UKIMWI na Magonjwa Sugu Yasiyoambukiza mahali pa kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba.


Afisa Lishe kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Bi. Nusrat Rubambura (aliyesimama) akiwasilisha mada kuhusu lishe bora wakati wa mafunzo kwa Waelimisha Rika wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI yaliyolenga kuwajengea uwezo Waelimisha Rika wa Idara na Vitengo vya ofisi hiyo ili kupambana na Afua za VVU, UKIMWI na Magonjwa Sugu Yasiyoambukiza mahali pa kazi.


Sehemu ya Waelimisha Rika, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Uendelezaji Sera, Sehemu ya Anuai za Jamii, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Mwanaamani Mtoo (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo Waelimisha Rika wa Idara na Vitengo vya ofisi hiyo ili kupambana na Afua za VVU, UKIMWI na Magonjwa Sugu Yasiyoambukiza mahali pa kazi.

 

Sehemu ya Waelimisha Rika, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo Waelimisha Rika wa Idara na Vitengo vya ofisi hiyo ili kupambana na Afua za VVU, UKIMWI na Magonjwa Sugu Yasiyoambukiza mahali pa kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba.


Tuesday, February 4, 2025

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAZINOA TAASISI ZA MALIASILI NA UTALII KUHUSU KUANDAA DAFTARI LA HUDUMA ZA SERIKALI


Na.Lusungu Helela- Dodoma

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeanza kuwanoa Watumishi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu kuandaa Daftari la kielektroniki la Huduma za Serikali kwa Taasisi zote za Serikali kwa lengo  la kuwawezesha wananchi na wadau mbalimbali  kupata  taarifa za huduma zote zinazotolewa  na Taasisi za Serikali kwenye chanzo kimoja.

 

Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - UTUMISHI, SACP. Ibrahim Mahumi wakati akifungua kikao kazi kuhusu Daftari la Huduma za Serikali kilichowakutanisha baadhi ya Watumishi kutoka Taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii,

 

SACP Mahumi amesema Daftari hilo ni muendelezo wa utengenezaji wa mifumo ya kuiwezesha serikali kutoa huduma bora kwa wananchi.

 

Kufuatia hatua hiyo SACP. Mahumi amewataka Watumishi hao kuzingatia mafunzo ya uandaaji wa daftari hilo kwani litakuwa chachu ya kuboresha utoaji wa huduma katika Taasisi za Wizara hiyo.

 

Amewasihi Watumishi hao kutambua kuwa Mteja ndiyo mlengwa mkuu wa daftari hilo hivyo wahakikishe huduma zote zinazotolewa  na Taasisi zao  zinaainishwa na kuingizwa  kwenye daftari hilo kwa usahihi wa hali ya juu.

 

Akitolea mfano wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) SACP. Mahumi amesema ili Mwananchi aweze kupata huduma katika taasisi hiyo ni lazima awe na taarifa za kutosha  kwa kuzingatia huduma zinazotolewa,  gharama na muda utakaotumika kupata huduma hizo.

 

Katika hatua nyingine, SACP. Mahumi amewataka washiriki wa mafunzo hayo wakawe mabalozi na wakatumie muda kuwafundisha watumishi wengine ili waweze kujua umuhimu wa  daftari hilo.

 

Awali, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Patrick Marcelline, ameushukuru uongozi wa Ofisi Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kwa mafunzo hayo muhimu, na kuahidi kuwa Wizara itayatumia Mafunzo hayo kama nyenzo muhimu ya kuboresha huduma zake kwa maslahi mapana ya Uhifadhi na Utalii na Taifa kwa ujumla

 

Kikao kazi hicho cha siku tatu cha uandaaji wa Daftari la Huduma za Serikali kinawezeshwa na timu ya wataalam wabobezi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

 

Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, UTUMISHI, SACP.Ibrahim Mahumi akizungumza wakati akifungua kikao kazi kuhusu uandaaji wa Daftari la Huduma za Serikali kilichowakutanisha baadhi ya Watumishi kutoka Taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii

 


Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, UTUMISHI, SACP.Ibrahim Mahumi  akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Patrick Marcelline   mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kufungua kikao kazi kuhusu uandaaji wa Daftari la Huduma za Serikali kilichowakutanisha baadhi ya Watumishi kutoka Taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii

 

Baadhi ya Watumishi kutoka Taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii wakimsikiliza Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, UTUMISHI, SACP. Ibrahim Mahumi akizungumza wakati akifungua kikao kazi kuhusu uandaaji wa Daftari la Huduma za Serikali

 



Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Patrick Marcelline akizungumza kabla ya kumkaribisha Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, UTUMISHI, SACP. Ibrahim Mahumi kuzungumza na Watumishi wakati akifungua kikao kazi kuhusu uandaaji wa Daftari  la Huduma za Serikali

 

 




Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, UTUMISHI, SACP.Ibrahim Mahumi akiwa kwenye picha ya pamoja na Watumishi kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii mara baada  kufungua kikao kazi kuhusu uandaaji wa Daftari  la Huduma za Serikali

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAPATIWA ELIMU YA KINGA NA TAHADHARI DHIDI YA MAJANGA YA MOTO

 Na. Mwandishi Wetu

Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wameaswa kuchukua tahadhari dhidi ya majanga ya moto pamoja na matumizi sahihi ya namba ya dharula 114 ili kutunza jengo la ofisi hiyo na kuendelea kutoa huduma kwa wateja wanaofika ofisini hapo bila kuwa na shaka yoyote.

Wito huo umetolewa na Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Bw. Iddi Chanyika wakati wa mafunzo kwa watumishi wa ofisi hiyo yanayotolewa kila Jumatatu ya wiki kwa lengo la kujenga uelewa wa masuala ya kiutumishi ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.

Bw. Chanyika ameeleza kuwa, Ofisi ya Rais-UTUMISHI inapokea wateja wengi kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali za kiutumishi hivyo, ili kulinda usalama wa wateja wanaoingia na kutoka kwa ajili ya kupata huduma hizo ni muhimu kuchukua tahadhari hasa katika kuangalia usalama wa jengo la ofisi hiyo.

Aidha Bw. Chanyika ameipongeza Ofisi ya Rais-UTUMISHI kwa kuwa na vifaa mbalimbali vya tahadhari kwa ajili ya kujikinga na madhara ya moto yanayoweza kutokea. 

“Niipongeze ofisi hii kwa kuzingatia usalama wa jengo kwani nimeona mna vifaa kwa ajili ya tahadhari dhidi ya moto vikiwemo ving’amua moto,’’ amesema Bw. Chanyika

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mipango, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Cosmas Ngangaji ametoa shukrani kwa niaba ya Watumishi wa ofisi hiyo kwa mafunzo mazuri ambayo yatasaidia kuongeza umakini katika utunzaji wa majengo ya ofisi hiyo na kuahidi kuchukua tahadhari zote zinazohusu kinga dhidi ya majanga ya moto.

Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakimsikiliza Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Bw. Iddi Chanyika (kushoto) wakati akielezea namna ya kuchukua tahadhari dhidi ya majanga ya moto kwenye mafunzo ya kuwajengea uelewa watumishi hao yaliyofanyika Mtumba jijini Dodoma.

Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo kuhusu namna ya kuchukua tahadhari dhidi ya majanga ya moto yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Bw. Iddi Chanyika (aliyesimama) akielezea matumizi ya kizima moto cha aina ya unga mkavu wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa kuhusu tahadhari dhidi ya majanga ya moto kwa watumishi hao yaliyofanyika Mtumba jijini Dodoma.


Afisa Tawala Mwandamizi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. George Ndatta akifanya zoezi kwa vitendo la kuzima moto kwa kutumia gesi ya ukaa wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa kuhusu tahadhari dhidi ya majanga ya moto kwa watumishi hao yaliyofanyika Mtumba jijini Dodoma.

Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo kuhusu namna ya kuchukua tahadhari dhidi ya majanga ya moto yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Baadhi ya Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakimsikiliza Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Bw. Iddi Chanyika (kulia) wakati akifafanua jambo kwenye mafunzo ya uelewa kuhusu kuchukua tahadhari dhidi ya majanga ya moto yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Cosmas Ngangaji akitoa shukrani kwa Maafisa kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mara baada ya kumaliza kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa ofisi hiyo kuhusu kuchukua tahadhari dhidi ya majanga ya moto yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango na Bajeti, Bi. Julieth Magambo (aliyeinama) akifanya zoezi kwa vitendo la kufungua kizima moto cha aina ya unga mkavu wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa kuhusu tahadhari dhidi ya majanga ya moto kwa watumishi hao yaliyofanyika Mtumba jijini Dodoma. Anayemwelekeza ni Mkaguzi kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Bw. Steven Katte.








Monday, February 3, 2025

WAZIRI SIMBACHAWENE AIPONGEZA MENEJIMENTI YA OFISI YAKE KUBUNI SIKU MAALUM “UTUMISHI DAY GALA” ASISITIZA ITUMIKE KUWAKUMBUSHA WATUMISHI KUTIMIZA WAJIBU

Na Mwandishi Wetu - Dodoma 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ameipongeza menejimenti ya Ofisi yake kwa kuwa wabunifu katika masuala mbalimbali ya kiutumishi ikiwemo kubuni tukio la "Utumishi Day Gala”.

Mhe. Simbachawene ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki hii jijini Dodoma katika Siku maalum ya "Utumishi Day Gala 2025” iliyoandaliwa na menejimenti ya Ofisi yake kwa lengo la kubadilishana uzoefu ili kuboresha utendaji kazi hasa katika kutoa huduma bora kwa wananchi.

Amesema Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora itabaki kuwa Ofisi Kiongozi kutokana na bunifu mbalimbali ambazo imekuwa ikifanya kwa lengo la kuhakikisha Watumishi wake wanakuwa vinara wa kutoa huduma bora kwa wananchi.

Ameongeza kuwa Ofisi hiyo imekuwa ikijipambanua katika masuala mbalimbali ambayo huwezi kukutana nayo katika Wizara yeyote isipokuwa Utumishi lengo likiwa ni kuhakikisha Watumishi wanajengewa mazingira bora na wezeshi katika kutoa huduma bora kwa wananchi.

Amesema utamaduni huo wa kukutana mara moja kwa kila mwaka unatoa motisha kwa watumishi na kuongeza ufanisi na uwabikaji katika kutekeleza majukumu yao 

Mhe. Simbachawene amesisitiza kuwa ni vema siku hiyo maalum ikatumika kuhamasisha na kuwakumbusha watumishi wa Ofisi hiyo kutimiza wajibu wao kwa kutoa huduma bora kwa wananchi kwani wananchi wakihudumiwa kwa furaha, amani na utumilivu vinatawala nchini.

"Nimebahatika kuwa Waziri katika Wizara tisa lakini huu utamaduni wa kukutana kwa pamoja kama leo hii tulivyokutana hapa tunafurahi kwa pamoja haikuwahi kutokea, hakika hili jambo linapaswa kuigwa na Wizara zingine" alisisitiza Mhe. Simbachawene 

Ameongeza kuwa "Unaweza kudhani umeshaona mambo yote kumbe hapana hili la "Utumishi Day Gala" kwangu mimi ni jipya hakika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya  Utumishi wa Umma na Utawala Bora ni Ofisi Kiongozi katika nyanja zote na ndivyo inavyotakiwa, hongereni sana Menejimenti kwa ubunifu huu" 

Naye Naibu Waziri wa Ofisi hiyo Mhe. Deus Sangu ametumia fursa hiyo kuipongeza timu ya Menejimenti kwa wazo hilo la "Utumishi Day Gala" huku akiwataka Watumishi kufurahia huku wakibadilisha mbinu za kuhakikisha kila mmoja anakuwa kinara wa kutoa huduma bora kwa wananchi.

Awali Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi amesema tukio hilo hufanyika mara moja kila mwaka ambapo Watumishi hukutana kwa pamoja ikiwa ni fursa adhimu  kwao kutokana majukumu mengi wanayoyatekeleza kuwapelekea kutokuonana kwa pamoja kama ilivyo kwa ''Utumishi Day Gala”

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na watumishi wa ofisi yake kwenye Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma katika siku maalum (UTUMISHI DAY GALA 2025) iliyoandaliwa na Menejimenti ya ofisi yake kwa lengo la kujenga umoja na kuongeza chachu ya utendaji kazi.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu akizungumza na watumishi wa ofisi yake jijini Dodoma katika siku maalum (UTUMISHI DAY GALA 2025) iliyoandaliwa na Menejimenti ya ofisi hiyo kwa lengo la kujenga umoja na kuongeza chachu ya utendaji kazi kwa watumishi wa ofisi yake.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) kuzungumza na watumishi wa ofisi hiyo katika siku maalum (UTUMISHI DAY GALA 2025) iliyoandaliwa kwa lengo la kujenga umoja na kuongeza chachu ya utendaji kazi kwa watumishi wa ofisi yake.

Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI waliohudhuria katika siku maalum (UTUMISHI DAY GALA 2025) iliyoandaliwa na menejimenti ya ofisi hiyo kwa lengo la kujenga umoja na kuongeza chachu ya utendaji kazi.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu (kulia) akifurahia jambo na  Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (kushoto) katika siku maalum (UTUMISHI DAY GALA 2025) iliyoandaliwa na menejimenti ya ofisi hiyo jijini Dodoma kwa lengo la kujenga umoja na kuongeza chachu ya utendaji kazi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (wa pili kutoka kushoto) akiwasili katika eneo lililoandaliwa kwa ajili ya siku maalum (UTUMISHI DAY GALA 2025) kwa lengo la kujenga umoja na kuongeza chachu ya utendaji kazi.