Tuesday, December 3, 2024

NAIBU KATIBU MKUU, DAUDI ATAJA SABABU ZA WANANCHI KUTOTUMIA MIFUMO RASMI KUWASILISHA MALALAMIKO SERIKALINI


 


Na. Lusungu Helela- Dodoma

 

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala  Bora, Bw. Xavier Daudi amesema Wananchi walio wengi wamekuwa wakitumia mitandao ya Kijamii kufikisha malalamiko yao kwenye Taasisi za Serikali kutokana na  baadhi ya  Watumishi wa Umma kuvujisha siri za wateja wao pindi wananchi hao wanapotumia mifumo rasmi kutoa mrejesho

 

Amesema vitendo hivyo vimekuwa vikiwakatisha tamaa Wananchi wenye nia njema ya kuona Serikali inakuwa kinara wa kutoa huduma bora kwa wananchi wake.

 

Bw. Daudi ametoa kauli hiyo leo Jumanne Disemba 3, 2024 jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo maalum ya siku tatu kwa Maafisa Mrejesho kuhusu  uendeshaji wa mfumo wa e-Mrejesho katika Ofisi za Umma 

 

Amewataka Maafisa hao kutunza siri za wateja wao ili kuwafanya Wananchi kuwa huru kuwasilisha changamoto zinazowakabili  wakati wowote na mahali popote pasipo kulazimika kutumia mitandao ya kijamii 

Bw. Daudi ameongeza kuwa  Mfumo wa e-Mrejesho unampa fursa  mwananchi  kutuma  malalamiko, pongezi pamoja na maulizo kwa Serikali mahali popote na wakati wowote.

 

Kufuatia hatua hiyo Bw. Daudi amewataka Maafisa hao mara baada ya kurudi katika vituo vyao vya kazi wakahakikishe wanakuwa waadilifu na   wenye kutunza siri za ofisi na za  wateja wao ili kuwafanya wananchi kuwasilisha malalamiko yao kwenye njia rasmi

 

Aidha, Bw. Daudi amewataka Maafisa hao wakaimarishe Madawati au Ofisi za Mrejesho zilizopo katika Taasisi zao  ili kufanikisha ushughulikiaji mrejesho kwa ufanisi na kwa wakati katika Ofisi za Umma kwa vile   wameaminiwa kutekeleza jukumu hilo kwa ufanisi.

 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Usimamzi wa Utawala Bora kutoka USAID/PS3+ awamu ya pili Dkt. Emmanuel Malangalila amesema  wataendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania  katika kuhakikisha mfumo huo unatumika ipasavyo katika Serikali za Mitaa ambako ndiko kuna malalamiko makubwa kutoka kwa wananchi .

 

Mafunzo haya yanalenga kuona huduma zinazotolewa na Serikali zinafurahiwa na wananchi wote bila kujali rangi, kabila, mahali au hali yao ya kiuchumi waliyonayo amesisitiza Dkt. Malangalila

 

Hivi karibuni Tanzania ilipewa  tuzo ya Kimataifa ya ubunifu wa mfumo ya kidijitali wa Mrejesho (e-Mrejesho) nchini Korea Kusini na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) wakati wa Mkutano wa Umoja wa Jukwaa la Umoja wa Mataifa la Tuzo za Utumishi wa Umma (2024 UN Public Service Awards (UNPSF) kutokana na umadhubuti wake.

 

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala  Bora, Bw. Xavier Daudi akizungumza na Maafisa Mrejesho jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo maalum ya siku tatu kwa Maafisa hao kuhusu  uendeshaji wa mfumo wa e-Mrejesho katika Ofisi za Umma
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala  Bora, Bw. Xavier Daudi akiwa kwenye picha ya pamoja na Maafisa Mrejesho mara baada ya kufungua mafunzo maalum ya siku tatu kwa Maafisa hao kuhusu  uendeshaji wa mfumo wa e-Mrejesho katika Ofisi za Umma
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala  Bora, Bw. Xavier Daudi akisalimiana na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Utawala Bora kutoka USAID/PS3+ , Dkt. Emmanuel Malangalila mara baada ya kuwasili kwa ajili ya  kufungua mafunzo maalum ya siku tatu kwa Maafisa hao kuhusu  uendeshaji wa mfumo wa e-Mrejesho katika Ofisi za Umma, Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Bi. Leila Mavila 



Mkurugenzi wa Usimamizi wa Utawala Bora kutoka USAID/PS3+ , Dkt. Emmanuel Malangalila akizungumza na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Bi. Leila Mavila   mara baada ya kuwasili kwenye  mafunzo maalum ya siku tatu kwa Maafisa hao kuhusu  uendeshaji wa mfumo wa e-Mrejesho katika Ofisi za Umma.  


 Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Bi. Leila Mavila akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wawezeshaji wa Mafunzo   mara baada ya Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala  Bora, Bw. Xavier Daudi  kufungua   mafunzo maalum ya siku tatu kwa Maafisa hao kuhusu  uendeshaji wa mfumo wa e-Mrejesho katika Ofisi za Umma.  

 

Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Bi. Leila Mavila  akizungumza na Maafisa Mrejesho jijini Dodoma kabla Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala  Bora, Bw. Xavier Daudi  kufungua mafunzo maalum ya siku tatu kwa Maafisa hao kuhusu  uendeshaji wa mfumo wa e-Mrejesho katika Ofisi za Umma 
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala  Bora, Bw. Xavier Daudi akiwa kwenye meza kuu na baadhi ya Wakurugenzi mara baada ya kuwasili kwa ajili ya  kufungua mafunzo maalum ya siku tatu kwa Maafisa hao kuhusu  uendeshaji wa mfumo wa e-Mrejesho katika Ofisi za Umma, Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Bi. Leila Mavila 
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala  Bora, Bw. Xavier Daudi akiwa  na baadhi ya Wakurugenzi mara baada ya kuwasili kwa ajili ya  kufungua mafunzo maalum ya siku tatu kwa Waratibu wa Mrejesho 

Monday, December 2, 2024

MKANDARASI SUMA JKT AHIMIZWA KUKAMILISHA JENGO LA eGA KWA MUJIBU WA MKATABA

 Na. Veronica Mwafisi-Dodoma

Tarehe 03 Desemba, 2024

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amemtaka Mkandarasi SUMA JKT anayejenga ofisi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) kukamilisha haraka ujenzi wa jengo la ofisi hiyo kwa mujibu wa mkataba kwa kuwa  eGA ni kiini cha uendeshaji wa Serikali katika kujenga mifumo imara itakayoboresha utoaji wa huduma Serikalini.

Mhe. Simbachawene amesema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi katika Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) iliyolenga kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la ofisi hiyo jijini Dodoma.

“eGA ni kiini cha uendeshaji wa Serikali mtandao hivyo, tuna wajibu wa kurahisisha utendaji kazi wa taasisi za Serikali kwa lengo la kuboresha huduma zinazotolewa kwa wananchi, hivyo tumieni nguvu nyingi kukamilisha ujenzi huu kwa mujibu wa mkataba na kwa wakati,” Mhe. Simbachawene amesisitiza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Mhandisi Benedict Ndomba amesema, Serikali ya Awamu ya Sita kipaumbele chake kikubwa ni kuwa na Serikali ya Kidijitali ili kutoa huduma bora na kwa wakati, hivyo kukamilika kwa jengo hilo kwa wakati kutaisaidia Serikali kufikia malengo yake ya kujenga mifumo imara itakayoboresha utoaji wa huduma Serikalini.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza wakati alipofanya ziara ya kikazi katika Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) iliyolenga kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la ofisi hiyo jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Mhandisi Benedict Ndomba (wa sita kutoka kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (aliyevaa tai nyekundu) wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi iliyolenga kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) jijini Dodoma. Wengine ni Viongozi na Watendaji mbalimbali.

Mwakilishi kutoka ofisi ya Mshauri elekezi (TBA), Bw. Tsere Willium (aliyenyanyua mkono) akimweleza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (wa kwanza kulia) maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) unaoendelea wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo jijini Dodoma. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Mhandisi Benedict Ndomba


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akielekea kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) unaoendelea jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Ofisi ya Rais-IKULU, Bi. Ened Munthali (kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) unaoendelea jijini Dodoma.


Mwonekano wa jengo la ofisi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) linaloendelea kujengwa jijini Dodoma.

 




WATUMISHI WA OFISI YA RAIS, UTUMISHI WANOLEWA KUHUSU MFUMO WA e-UTENDAJI

 Na. Lusungu Helela -Dodoma

 Mkurugenzi Msaidizi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw.  Priscus Tairo ametoa wito kwa watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI kuchukua muda wao kujifunza kwa undani Mfumo  wa Usimamizi wa Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma ili kuwa msaada kwa watumishi walio nje ya Ofisi hiyo ambao wamekuwa wakihitaji kupata mafunzo ya mfumo huo ili waweze kuutekeleza kwa ufanisi.  

 Bw. Tairo ametoa kauli hiyo  leo Jumatatu Disemba 02, 2024 Ofisi ya Rais-UTUMISHI iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma wakati akitoa  mafunzo ya kuwajengea uwezo Watumishi wa Ofisi hiyo,  ikiwa ni muendelezo wa kutoa mafunzo elekezi ya kila wiki kwa Watumishi  hao  kwa  lengo la  kuboresha utendaji kazi kwa Watumishi wa Umma nchini.

 Bw. Tairo amesema Mfumo huu ni mpya, hivyo unahitaji watumishi wengi wenye uwezo wa kutoa msaada wa kiufundi kwa ukaribu, haraka na ufanisi ili kuleta matokeo yaliyokusudiwa.

 Amesema endapo Watumishi wa Ofisi hiyo wataweza kuufahamu vizuri jinsi mfumo huo wa e- unavyotenda kazi utawawezesha kutoa msaada kwa watumishi wengine wakati wowote na mahali popote lengo likiwa ni  kuifanya Serikali iweze kubaini mwenendo halisi wa utendaji kazi wa watumishi wa umma nchini.

 Kufuatia hatua hiyo, Bw. Tairo  amewataka Watumishi wa Ofisi hiyo kutumia muda wao  mwingi kujinoa katika eneo hilo kwani Watumishi wa nje ya Ofisi hiyo wana imani kubwa na watumishi wa Ofisi hii  bila kujali wanatoka katika idara inayojihusisha na mafunzo hayo.

 

Mwakilishi kutoka Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Charles Shija akizungumza mara baada ya kumalizika mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa ofisi hiyo yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw.  Priscus Tairo akitoa  mafunzo ya kuwajengea uwezo kuhusu Mfumo  wa Usimamizi wa Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma kwa  Watumishi wa Ofisi hiyo, ikiwa ni muendelezo wa kutoa mafunzo elekezi ya kila wiki kwa Watumishi  hao  kwa  lengo la  kuboresha utendaji kazi 

 













 Baadhi  ya Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi hao katika masuala ya utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

 


Mtumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw.  Dickson Isaya   akiwasilisha hoja wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi hao katika utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.