Thursday, October 10, 2024

KATIBU MKUU MKOMI AWATAKA WADAU KUTOA MAONI KATIKA MFUMO WA TATHMINI YA MAHITAJI YA RASILIMALIWATU ILI KUBORESHA UTENDAJI KATIKA UTUMISHI WA UMMA

 Na. Veronica Mwafisi-Dodoma

Tarehe 10 Oktoba, 2024

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi amesema Mfumo wa Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu utaisaidia Serikali kufanya msawazo katika Utumishi wa Umma ili kuwa na mtawanyo mzuri wa watumishi kwa lengo la kuboresha utendaji katika utumishi wa umma.

Bw. Mkomi ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha kujadili matokeo ya tathmini ya mahitaji ya rasilimaliwatu katika utumishi wa umma kwa Wakurugenzi wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kutoka Wizara zote, wataalamu wanaosimamia uandaaji na ujazaji wa mahitaji ya watumishi kutoka wizara zote pamoja na Wakurugenzi na wataalamu kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI.

Bw. Mkomi amesema kila Mkurugenzi anafahamu umuhimu wa mahitaji ya rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma na kuwasihi wafanye tathmini ya kutosha.

“Ukisema una watumishi wachache, tutakuuliza unahitaji watumishi wangapi? kwani unatakiwa uwe umefanya tathmini ya kutosha kwasababu inawezekana kumhitaji kwako mtumishi au kutokumhitaji kunatokana na matakwa yako na si mfumo unaokufahamisha kuwa mtumishi huyu ni wa ziada.” Bw. Mkomi amesema.

Bw. Mkomi amesema msawazo katika utumishi wa umma unahitajika kufanywa katika maeneo mawili ikiwemo mjini ili kutokuwa na watumishi wa ziada ambao hawana majukumu ya kutosha katika maeneo yao ya kazi lakini pia msawazo huo utasaidia kuunganisha familia.

Bw. Mkomi ameongeza kuwa, msawazo hautaweza kufanyika bila kuwa na taarifa halisi ya mahitaji na idadi ya watumishi waliopo katika maeneo husika hivyo, ni vizuri washiriki wakaangalia namna ya kufanya kwani inatakiwa kujua watumishi wangapi wanahitajika wapi, wakafanye nini na baada ya kujua hayo itapatikana nafasi nzuri ya kuboresha. 

“Niwatake mshiriki kikamilifu kwa kuipokea taarifa hiyo, kuichambua na kutoa mapendekezo yatakayosaidia kuboresha Mfumo huo utakaowezesha kuwa na mtawanyo mzuri wa watumishi katika Taasisi za Umma.” Bw. Mkomi amesisitiza.

Akitoa neno la utangulizi, Mkurugenzi wa Uendelezaji Taasisi, Bw. Nolasco Kipanda ameelezea lengo la kikao kazi hicho kuwa ni kujadili matokeo ya tathmini ya Rasilimaliwatu katika Taasisi za Umma ili kupata maoni toka kwa wadau hao na kuboresha mfumo huo katika Utumishi wa Umma kwa masilahi mapana ya taifa.  

Kikao kazi hicho kilichoanza leo kinafanyika kwa muda wa siku mbili ambapo mada mbalimbali zitawasilishwa ikiwemo Matokeo ya Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma, matokeo ya Wizara na vigezo kwa upande wa Wizara na Makundi ya Taasisi.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akifungua kikao kazi cha Wakurugenzi wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Maafisa Utumishi kutoka serikalini kilicholenga kujadili Matokeo ya Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma jijini Dodoma leo.


Sehemu ya Wakurugenzi wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Maafisa Utumishi kutoka serikalini wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi kilicholenga kujadili Matokeo ya Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma jijini Dodoma leo.

Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Taasisi, Bw. Nolasco Kipanda akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (hayupo pichani) kufungua kikao kazi cha Wakurugenzi wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Maafisa Utumishi kutoka serikalini kilicholenga kujadili Matokeo ya Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma jijini Dodoma leo.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (kulia) akiwa katika kikao kazi cha Wakurugenzi wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Maafisa Utumishi kutoka serikalini kabla ya kufungua kikao hicho kilicholenga kujadili Matokeo ya Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma jijini Dodoma leo. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji  Taasisi, Bw. Nolasco Kipanda 

Baadhi ya Wakurugenzi wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi wakati akifungua kikao kazi cha Wakurugenzi wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Maafisa Utumishi kutoka serikalini kilicholenga kujadili Matokeo ya Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma jijini Dodoma leo.

Baadhi ya Maafisa kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi wakati akifungua kikao kazi cha Wakurugenzi wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Maafisa Utumishi kutoka serikalini kilicholenga kujadili Matokeo ya Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma.

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Felista Shuli akijibu moja ya hoja iliyowasilishwa wakati wa kikao kazi cha Wakurugenzi wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Maafisa Utumishi kutoka serikalini kilicholenga kujadili Matokeo ya Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma jijini Dodoma leo.

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Felista Shuli akijibu moja ya hoja iliyowasilishwa wakati wa kikao kazi cha Wakurugenzi wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Maafisa Utumishi kutoka serikalini kilicholenga kujadili Matokeo ya Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma jijini Dodoma leo.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha Wakurugenzi wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Maafisa Utumishi kutoka serikalini mara baada ya kufungua kikao hicho kilicholenga kujadili Matokeo ya Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma jijini Dodoma leo. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Taasisi, Bw. Nolasco Kipanda.

Sehemu ya washiriki wa kikao kazi cha kujadili Matokeo ya Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi hicho kilichofanyika jijini Dodoma leo.

Afisa Tawala Mwandamizi, Idara ya Uendelezaji Taasisi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Waziri Mkumbo akiwasilisha mada kwa Wakurugenzi wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Maafisa Utumishi kuhusu Matokeo ya Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma wakati wa kikao kazi cha kujadili matokeo ya tathmini hiyo kilichofanyika jijini Dodoma leo.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Wizara ya Kilimo, Bw. Philbert Lutale akichangia mada wakati wa kikao kazi cha Wakurugenzi wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Maafisa Utumishi kutoka serikalini kilicholenga kujadili Matokeo ya Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma jijini Dodoma leo.

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Wizara ya Fedha, ambaye ni Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Wakurugenzi wa Idara ya Rasilimaliwatu wa Wizara zote, Bw. Lusius Mwenda (kulia) akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi cha Wakurugenzi hao na Maafisa Utumishi kutoka serikalini kilicholenga kujadili Matokeo ya Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma jijini Dodoma leo. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Taasisi, Bw. Nolasco Kipanda.


WAZIRI SIMBACHAWENE AWASIHI WATUMISHI KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA



 

VIONGOZI WAKUU WA OFISI YA RAIS, UTUMISHI NA UTAWALA BORA WAPOKEA VIKOMBE VYA USHINDI









 

Wednesday, October 9, 2024

WAZIRI SIMBACHAWENE APOKEA VIKOMBE VYA USHINDI




Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amewapongeza Viongozi na wanamichezo wa Ofisi yake kwa kupambana na kutwaa vikombe viwili vya ubingwa katika michezo inayosimamiwa na Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI).

 Mhe. Simbachawene ametoa pongezi Oktoba 8, 2024 wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika Jengo la Ofisi za Utumishi, Mtumba jijini Dodoma kwa lengo la kupokea Vikombe vya ushindi katika mchezo wa mpira wa miguu na mashindano ya baiskeli ya SHIMIWI. 

"Niwapongeze kwa kuleta heshima kubwa katika Ofisi hii, ubingwa wa mpira wa miguu na ushindi wa nafasi ya kwanza kwenye mashindano ya baiskeli unadhihirisha dhamana yetu ya kusimamamia Watumishi wa Umma na kuwa mfano kwa kila jambo lililo jema" alisema Mhe. Simbachawene.

 

Amesisitiza kuwa, ushindi wa vikombe viwili ni hatua kubwa lakini kubwa zaidi ni kitendo cha kubeba kombe la mpira wa miguu. Kombe la mpira wa miguu linaleta maana zaidi kuliko waliochukua vikombe vingine.

 Aidha, Mhe. Simbachawene ametumia fursa hiyo kumpongeza Katibu Mkuu-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi kwa kuwa chachu ya kuimarisha michezo Ofisini amemuomba kuendelea kuwa na ari hiyo ili kujenga afya njema za watumishi mahala pa kazi. 

 Naye Naibu Waziri Mhe. Sangu amewapongeza wanamichezo hao kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kupambana ili kufikia malengo yaliyokuwa yamewekwa ya kuleta ushindi.


Amesema kuwa, ushindi huo wa vikombe viwili unatokana na jitihada kubwa zilizofanywa na Katibu Mkuu, Bw.Juma Mkomi ya kuwa karibu na wachezaji hao na kuwapa hamasa na zaidi kuwawezesha ipasavyo. 

 Halikadhalika, ametoa pongezi za kipekee kwa Bw. Mkomi kwa kuwa kiungo muhimu sana kwa watumishi wa Ofisi hiyo, mathalani ukaribu wake kwa wachezaji umekuwa chanzo cha kufanya vizuri kwenye michezo ya SHIMIWI na ameombwa kuendelea kuwa na moyo huo ambao matokeo yake yanaonekana kwa kila mmoja mtumishi.

 Naye Katibu Mkuu Mkomi amewapongeza wachezaji hao huku akimshukuru Waziri Mhe. Simbachawene pamoja na Naibu Waziri Mhe. Deus Sangu kwa ushirikiano wao mkubwa walionao katika kupenda na kuthamini michezo. 

 "Nakushukuru Naibu Waziri Mhe. Sangu kwa kufika katika kambi za mashindano hayo na kutoa hamasa kubwa wa watumishi wetu, hamasa hiyo imeleta ushindi ambao tunafurahia hii leo” alisema Bw. Mkomi 

 Mashindano ya SHIMIWI yalihitimishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  Oktoba 5, 2024 Mkoani Morogoro.

 



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene, Naibu Waziri wa Ofisi hiyo Mhe. Deus Sangu pamoja na Katibu Mkuu, Bw. Juma Mkoni wakipokea vikombe kutoka kwa baadhi ya wachezaji wakati wa hafla fupi ya kupokea vikombe hivyo.

 






Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene, Naibu Waziri wa Ofisi hiyo Mhe.Deus Sangu  pamoja na Katibu Mkuu, Bw.Juma Mkoni wakiwa kwenye picha pamoja na baadhi ya Wachezaji wa mpira wa miguu pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi hiyo wakati wa hafla fupi ya kupokea vikombe hivyo.





Baadhi ya Wachezaji wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vikombe vya Mashindano ya SHIMIWI.

 

 

 

 

 

 

 

 


Tuesday, October 8, 2024

KITUO CHA HUDUMA KWA MTEJA - WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

 











WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

 










OFISI YA RAIS-UTUMISHI, KIMBILIO KWA HUDUMA ZA KIUTUMISHI

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Xavier Daudi amewapongeza watumishi wa Ofisi yake kwa kutoa huduma nzuri kwa Watumishi na Wananchi wenye uhitaji wa huduma na kuifanya Ofisi hiyo kuwa kimbilio wakati wote kwa huduma za Kiutumishi.

Kaimu Katibu Mkuu huyo ametoa pongezi hizo Oktoba 8, 2024 wakati alipowasili katika Ofisi hizo zilizopo Mtumba, Dodoma kutekeleza majukumu yake ya kila siku na kukutana na watumishi wake waliokuwa wakitoa huduma katika eneo la mapokezi.

“Hakikisheni mnatoa maelezo sahihi na huduma bora na haraka kwa kila Mtumishi au Mwananchi anayekuja kupata huduma katika Ofisi hii, uharaka na ufanisi wetu, utawapa wateja nafasi ya kuendelea na shughuli nyingine za kujenga uchumi wa nchi” amesema Bw. Daudi.

Vilevile, ameongeza kuwa, Wiki hii ni muhimu sana katika usimamizi wa utoaji huduma kwa umma kwa kuwa inasaidia kuimarisha uhusiano baina ya Ofisi na wateja, lakini zaidi kuwafikia Watumishi na Wananchi kwa njia mbalimbali na kutatua shida zao kwa ufanisi na haraka.

Aidha, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, UTUMISHI Bw. Mussa Magufuli amebainisha kuwa kupitia Wiki ya Huduma kwa Wateja, Ofisi  itahakikisha inakutana na wateja ili kupata maoni, mapendekezo ya kuboresha huduma na kutatua changamoto mbalimbali za kiutumishi zinazowakabili watumishi na wananchi.

Wiki ya Huduma kwa Wateja huadhimishwa kila mwaka katika wiki ya kwanza ya Oktoba. Kwa mwaka huu, wiki hii imeanza tarehe 7 na itahitimishwa tarehe 11 Oktoba, 2024.