Na. Lusungu Helela- Kilolo
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete amesikitishwa na wimbi kubwa la wafanyakazi hususan walimu wanaotuma maombi ya kutaka kuhama katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, Mkoani Iringa.
Mhe.Kikwete ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Watumishi wa Halmashuuri ya Kilolo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi Mkoani humo ya kuzungumza na kusikiliza kero za watumishi na kuzitafutia ufumbuzi.
Amesema Watumishi walio wengi wanaotaka kuhama wamekuwa wakitaja sababu zinazofanana jambo ambalo lina walakini huku akisema kuna matatizo ya kiuongozi katika Halmashauri hiyo .
Ametaja moja ya sababu zinazopelekea Watumishi hao kutaka kuhama ni pamoja na kupuuzwa na kutokusikilizwa pindi watumshi hao wanapokuwa na changamoto.
'" Kuna watumishi hapa hawajapandishwa vyeo kwa muda miaka tisa na wengine hapa licha ya kujiendeleza kielimu mishahara yao haijabadilika lakini ninyi Maafisa Utumishi wenye jukumu la kufuatilia UTUMISHI na kuwapa majibu mpo tu, hili sio sawa hata kidogo" amesisitiza Mhe.Kikwete.
Amefafanua kuwa katika Halmashauri hiyo Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala wamekuwa miungu watu badala ya kuwa suluhisho la matatizo yanayowakabili watimishi wanaowasimamia.
Amesema licha ya watumishi wengi wanaotaka kuhama kutaja sababu inayofanana, kuwa ni uwepo wa baridi kali na hivyo kusumbuliwa na "athma" jambo ambalo si kweli, ukweli ni kwamba hakuna mahusiano mazuri kati ya Watumishi na Uongozi wa Halmashauri hiyo.
Kufuatia hatua hiyo Mhe.Kikwete amemtaka Mkurugenzi kufanyia kazi changamoto zinazowakabili watumishi hao ikiwemo kufanya vikao vya mara kwa mara na watumishi kwa ajili ya kuwasikiliza pamoja na kuzingatia stahili zao ikiwepo posho za likizo.
Katika hatua nyingine Mhe.Kikwete amewatak Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala kuwa kimbilio la watumishi badala ya kuwa vikwazo katika kufanyia kazi changamoto za watumishi.
" Kazi yenu Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala ni kusikiliza, kupendekeza watumishi wenu katika kupandishwa vyeo lakini mlio wengi mmekuwa ni watu wenye roho mbaya na mnaopenda kuwakomoa wenzenu, acheni hizo " amesisitiza Mhe.Kikwete
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo, Estomin Kyando ametumia nafasi hiyo kumshukuru Naibu Waziri Kikwete kwa kufika kwa ajili ya kuzungumza na watumishi anawaongoza huku akiahidi kufanyia kazi maelekezo yote aliyoyatoa ili watumishi waweze kufurahi kufanya kazi katika Halmashauri hiyo.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo mkoani Iringa ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi ya kuzungumza na kusikiliza changamoto zinazowakabili watumishi hao.
Sehemu ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete alipokuwa akizungumza nao ambapo ameahidi kushirikiana nao katika kutatu changamoto mbalimbali zinazowakabili
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akifurahia jambo kbala ya kuanza kuzungumza na na Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo mkoani Iringa ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi ya kuzungumza na kusikiliza changamoto zinazowakabili watumishi hao.
Mtumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa, Felister Mnyawami akizungumza mbele ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati alipotoa nafasi ya watumishi hao kuzungumza changamoto zao zinazowakabili ili aweze kuzitafutia ufumbuzi.
No comments:
Post a Comment