Tuesday, November 14, 2023

MHE. SIMBACHAWENE AIPONGEZA MENEJIMENTI YA OFISI YAKE KWA KUSIMAMIA KIKAMILIFU UJENZI WA OFISI MPYA

 Na. Rainer Budodi na Veronica Mwafisi-Dodoma

Tarehe 15 Novemba, 2023

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene ameipongeza menejimenti ya ofisi yake kwa kusimamia kwa makini ujenzi wa jengo la ofisi hiyo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma. 

Amesema jitihada hizo za kusimamia kwa dhati ujenzi wa jengo hilo kubwa na lenye mvuto katika mji huo wa Serikali zinashamilisha dhamira ya Serikali ya kuhamishia makao makuu ya nchi na Serikali Dodoma.

Pamoja na kuipongeza menejimenti ya ofisi yake kwa kusimamia ipasavyo ujenzi wa jengo hilo la kisasa ambalo mpaka sasa umefikia asilimia 95, Mhe. Simbachawene ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo na kuongeza kuwa, watumishi wa ofisi yake wako tayari kuingia na kutekeleza majukumu yao ndani ya jengo hilo.

Aidha, amemsisitiza Mkandarasi kukamilisha ujenzi huo sehemu ndogo iliyobaki kwa ustadi na ufanisi mkubwa ili kuhakikisha thamani halisi ya fedha iliyotolewa na Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inaonekana.

Naye, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi amemuomba Waziri Mhe. George Simbachawene kufikisha salaam za shukurani na pongezi kwa Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kusimamia utekelezaji wa dhamira ya waasisi wa taifa hili na viongozi wote waliopita kuhusu kuhamishia makao makuu ya nchi na Serikali Jijini Dodoma kwa kuendelea kutoa maelekezo na fedha za kutekeleza ujenzi wa majengo na miundombinu wezeshi katika ofisi yake.

Aidha, amesisitiza utayari wa watumishi wa ofisi yake kuhamia katika ofisi hizo mpya na kuendelea kutekeleza majukumu yao ya kutoa huduma bora kwa watumishi wa umma na wananchi kwa jumla.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na Watendaji wa ofisi yake mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililopo katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma


Sehemu ya Watendaji wa ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la ofisi hiyo katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (katikati) akifurahia jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la ofisi hiyo katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (Wa pili kutoka kushoto) akiwasili katika jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililopo katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (Wa tatu kutoka kushoto) akijadili jambo na Watendaji wa Ofisi yake wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililopo katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma. Kulia kwake ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi.


Watendaji wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la Ofisi ya Rais-UTUMISHI katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.

Mwonekano wa jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambalo lipo katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.



No comments:

Post a Comment