Na. Rainer Budodi- Dodoma
Tarehe 2 Novemba, 2023
Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama ameitaka
Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa kuongeza jitihada zaidi katika kutafuta
kumbukumbu na nyaraka kutoka taasisi mbalimbali za umma na kuzihifadhi mahali
salama na katika ubora unaotakiwa kwa manufaa ya vizazi vilivyopo na vijavyo.
Dkt. Mhagama amesema hayo
leo Novemba 2, 2023 jijini Dodoma wakati wa ziara ya Kamati hiyo katika Ofisi
ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa kuona namna Idara hiyo inavyotunza
kumbukumbu na nyaraka za Taifa.
Aidha, kwa niaba ya
Kamati, Dkt. Mhagama ameipongeza Idara hiyo kwa kufanya kazi kubwa ya kuhifadhi
Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa ikiwa ni pamoja na historia ya mambo muhimu ya
kitaifa na kimataifa kwa kuzingatia misingi na maadili ya utumishi wa umma.
“Sisi kama Kamati tumeona
na kushuhudia miundombinu mizuri na matumizi bora ya TEHAMA katika uhifadhi wa
kumbukumbu na nyaraka hizi, hongereni sana na kwa mantiki hii tunajivunia kuwa
na hazina kubwa ya taarifa” alisema Dkt. Mhagama.
Vilevile Dkt. Mhagama amemsisitiza
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Ridhiwani Kikwete kuhakikisha ofisi yake inaisimamia vyema Idara ya
Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa katika zoezi la kuhifadhi nyaraka ambazo
zimekusanywa hivi karibuni ili ziwe kwenye utaratibu mzuri kama zilivyo
nyingine kwa lengo la kuepuka upotevu wowote wa nyaraka hizo.
Kwa upande wake Naibu
Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete ameishukuru Kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba
na Sheria kwa kupanga ziara hiyo muhimu na kutoa maelekezo ambayo yatafanyiwa
kazi kwa haraka na kutoa mrejesho.
“Ujio wenu hapa
umeambatana na maelekezo muhimu sana kwetu ili kuimarisha shughuli zinazofanywa
na Idara hii kwa ustawi wa Serikali na Taifa kwa jumla, nasi tuko tayari
kutekeleza maelekezo hayo kwa haraka na ufanisi” alisema Mhe. Kikwete.
Mhe. Kikwete ameongeza
kuwa ofisi yake itasimamia na kutekeleza maelekezo hayo kwa kuwa tayari
Serikali imeshatoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali katika
Idara hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akizungumza na sehemu ya Viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Watendaji wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa wakati wa ziara ya kamati hiyo katika Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na
Sheria wakifuatilia wasilisho la taarifa ya utendaji kazi wa Idara ya
Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa wakati wa ziara ya kikazi katika Ofisi hiyo
jijini Dodoma.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.
Ridhiwani Kikwete akitoa neno la shukrani kwa Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa ziara ya kamati hiyo katika
Ofisi ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.
Wajumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na Viongozi wa Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakielekea katika ghala
la utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya
kikazi katika Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.
Wajumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na Viongozi wa Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia maelezo ya Mtunza
Kumbukumbu Msaidizi Bi. Rehema Mwiga (Wa kwanza kulia) kuhusu nyaraka mbalimbali
zinazotunzwa katika ghala hilo wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hiyo ilipotembelea
Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.
Ridhiwani Kikwete akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa ziara ya kikazi ya
kamati hiyo ilipotembelea Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini
Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi akiwaonesha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria moja ya nyaraka zilizopo katika ofisi yake wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hiyo jijini Dodoma.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwa pamoja
na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria
wakitazama moja ya nyaraka zilizopo katika Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za
Taifa wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hiyo jijini Dodoma.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.
Ridhiwani Kikwete (kulia) akiteta jambo na Kaimu Katibu Mkuu, Bw. Xavier Daudi
wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria
katika Ofisi ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.
Wajumbe wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakiwa katika picha ya pamoja
na Viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
na Watendaji wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa wakati ziara ya kikazi katika
Idara hiyo jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment