Na. Veronica Mwafisi - Geita
Tarehe 28 Januari, 2023
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka
Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kusimamia kikamilifu miradi
inayotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kama wanavyosimamia
miradi mingine ya maendeleo.
Mhe.
Ndejembi amewahimiza wakurugenzi hao, wakati akizungumza na Watendaji wa
Halmashauri ya Mji Geita na Halmashauri ya
Wilaya ya Geita
alipokuwa akihitimisha ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji
kwa watumishi wa umma pamoja na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani
Geita.
Mhe. Ndejembi amehimiza miradi
ya TASAF kusimamiwa vizuri kama inavyosimamiwa miradi mingine ya maendeleo
kwani miradi yote inatekelezwa na Serikali chini ya uongozi makini wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye
amedhamiria kuliletea taifa maendeleo.
Mhe. Ndejembi amesema, katika
utekelezaji wa miradi ya TASAF inaonyesha kuwa wakurugenzi na watendaji wa
halmashauri hawashiriki kikamilifu katika usimamizi na badala yake huwaachia
waratibu na watendaji wa TASAF.
“Usimamizi wa miradi ya TASAF unapaswa kupewa
kipaumbele, hivyo wakurugenzi ni lazima waisimamie miradi hii kikamilifu kwa
sababu fedha inayotumika upatikanaji wake unatokana na jitihada za Rais wa
Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.
Mhe. Ndejembi amefafanua kuwa,
miradi ya TASAF ikisimamiwa kikamilifu kama ambavyo inavyosimamiwa miradi
mingine ikiwemo ya elimu, afya na miundombinu ni dhahiri kuwa, watanzania
watanufaika na taifa litapiga hatua katika mendeleo.
Kwa upande wake, Makamu
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mji Geita, Mhe. Joseph Lugaila amemshukuru
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na
wasaidizi wake kwa kuwezesha utekelezaji wa miradi mingi ya maendeleo katika
Mkoa wa Geita.
Aidha, Mhe. Lugaila
amemshukuru Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi kwa kufanya ziara ya kikazi katika mkoa
wa Geita yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma na kukagua utekelezaji
wa miradi ya TASAF.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi (katikati) akizungumza
na
Watendaji wa Halmashauri ya Mji Geita na
Halmashauri ya Wilaya ya Geita wakati
wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kukagua utekelezaji
wa miradi ya TASAF mkoani Geita.
Sehemu
ya
Watendaji wa Halmashauri ya Mji Geita na
Halmashauri ya Wilaya ya Geita wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (katikati
meza kuu) mara baada ya Naibu Waziri huyo kukagua miradi ya TASAF wakati wa
ziara yake ya kikazi mkoani Geita.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Msangi Tsetonga akifafanua jambo kwa Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu
Waziri Ndejembi, iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri
ya Mji Geita na
Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi (wapili kutoka kulia) akielekea kukagua madarasa ya shule
ya Msingi Kivukoni yaliyopo katika Halmashauri ya Mji Geita wakati wa ziara
yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Geita, wengine
ni watendaji wa mkoa huo.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi (aliyenyanyua mikono) akizungumza na wananchi wa Mtaa
wa Nyanza mara baada ya kukagua madarasa na vyoo vya shule ya Kivukoni
vilivyojengwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) mkoani Geita.
Mwonekano
wa darasa lililopo shule ya Msingi Kivukoni katika Halmashauri ya Mji Geita,
lililojengwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
No comments:
Post a Comment