Thursday, January 26, 2023

TASAF KUJENGA JENGO JIPYA LA KUTOA HUDUMA ZA KITABIBU KATIKA KITUO CHA AFYA CHA DONGE VIJIBWENI ZANZIBAR

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na wananchi na wanufaika wa TASAF wa Shehia ya Donge Pwani iliyopo Wilaya ya Unguja Kaskazini B, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar.

 

Sehemu ya wananchi na wanufaika wa TASAF wa Shehia ya Donge Pwani iliyopo Wilaya ya Unguja Kaskazini B wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar.

 

 

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Dkt. Khalid Mohamed ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Donge akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Mhe. Jenista Mhagama kuzungumza na wananchi na wanufaika wa TASAF wa Shehia ya Donge Pwani iliyopo Wilaya ya Unguja Kaskazini B, wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe. Jenista Mhagama iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar.


 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akikagua jengo la huduma ya mama na mtoto linalojengwa na TASAF katika Kituo cha Afya cha Dongo Vijibweni, kilichopo Wilaya ya Unguja Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar.


 

Mwonekano wa jengo la huduma ya mama na mtoto linalojengwa na TASAF katika Kituo cha Afya cha Dongo Vijibweni, kilichopo Wilaya ya Unguja Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar.


Mmoja wa wakazi wa Shehia ya Donge Pwani, Bi. Yabi Abdallah akitoa shukrani kwa TASAF kwa kujenga jengo la huduma ya mama na mtoto litaboresha utoaji wa huduma za afya ya uzazi kwa akina mama wa Shehia hiyo.

 

 


 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi na wanufaika wa TASAF wa Shehia ya Donge Pwani iliyopo Wilaya ya Unguja Kaskazini B, mara baada ya waziri huyo kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku mbili ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar.

No comments:

Post a Comment