Friday, January 20, 2023

MHE. JENISTA AELEKEZA MILIONI 103 ZITOLEWE NA TASAF KUKAMILISHA UJENZI WA KIVUKO CHA WAENDA KWA MIGUU MTAA WA ENGOSENGIU ARUSHA

 

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na wananchi na walengwa wa TASAF Mtaa wa Engosengiu katika Halmashauri ya Jiji la Arusha, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF iliyopo katika halmashauri hiyo ya jiji.

 

Sehemu ya wananchi na walengwa wa TASAF wa Mtaa wa Engosengiu Halmashauri ya Jiji la Arusha wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa ziara ya waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika halmashauri hiyo ya jiji.

 
 

 
Mwonekano wa kivuko cha waenda kwa miguu kinachojengwa na TASAF Mtaa wa Engosengiu katika Halmashauri ya Jiji la Arusha
 

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Said Mtanda akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama kuzungumza na wananchi na walengwa wa TASAF wa Mtaa wa Engosengiu Halmashauri ya Jiji la Arusha, wakati wa ziara ya kikazi ya waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Wilaya ya Arusha.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akisikiliza taarifa ya ujenzi wa kivuko cha waenda kwa miguu kinachojengwa na TASAF Mtaa wa Engosengiu katika Halmashauri ya Jiji la Arusha alipotembelea eneo ambalo kivuko hicho kinajengwa.    

 

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akielekea eneo atakalozungumza na wananchi na walengwa wa TASAF Mtaa wa Engosengiu katika Halmashauri ya Jiji la Arusha, mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kivuko cha waenda kwa miguu kinachojengwa na TASAF katika mtaa huo.


 

Mkazi wa Mtaa wa Engosengiu Halmashauri ya Jiji la Arusha Bi. Rahel Mushi akimueleza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) kuhusu changamoto ya kivuko cha waenda kwa miguu wanayokabiliana nayo wakazi wa eneo hilo.

No comments:

Post a Comment