Na. James
K. Mwanamyoto-Dodoma
Tarehe
28 Mei, 2022
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini kuhakikisha wanaondoa utamaduni wa baadhi ya Watumishi wa Umma kufanya kazi kwa mazoea ili wananchi wapate huduma bora katika taasisi zote za umma nchini.
Mhe. Ndejembi ametoa wito huo jijini
Dodoma, kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa kufunga Kikao Kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa
Rasilimaliwatu Serikalini.
Mhe. Ndejembi amesema, Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeweka mipango mizuri katika Utumishi wa Umma lakini kama baadhi ya watumishi wataendelea na utamaduni wa kufanya kazi kwa mazoea ni wazi kuwa Serikali haitoweza kutimiza lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi.
“Ninyi wasimamizi wa Rasilimaliwatu ndio wenye jukumu kubwa la kuisaidia Serikali kubadili utamaduni wa kufanya kazi wa mazoea katika taasisi zenu,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.
Ameongeza kuwa, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akieleza azma ya Serikali yake ya kuujenga Utumishi wa Umma wenye kuwajibika bila kushurutishwa, hivyo amewataka wasimamizi hao wa rasilimaliwatu kuondoa utendaji kazi wa mazoea katika maeneo yao ya kazi ili kumsaidia Mhe. Rais kutimiza azma yake.
Akizungumza na washiriki wa kikao kazi hicho, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa amewaeleza wasimamizi hao wa raslimaliwatu serikalini kuwa, wajibu wao ni kusimamia vizuri rasilimaliwatu ili kuwezesha utoaji wa huduma kwa wananchi kama ilivyoainishwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025.
Waziri Bashungwa amesema wasimamizi hao wa rasilimaliwatu wamejifunza mengi katika kikao kazi hicho, hivyo ametaka kuiishi kwa vitendo kaulimbiu ya kikao kazi hicho inayosema “UTUMISHI WA UMMA WENYE UADILIFU, NIDHAMU, UBUNIFU, WELEDI NA UWAJIBIKAJI WA HIARI KWA USTAWI WA TAIFA”.
Mhe. Bashungwa amewakumbusha wasimamizi hao wa rasilimaliwatu kuwa, wao ndio mameneja wa rasilimaliwatu katika Taasisi za Umma hivyo hakuna namna yoyote ambayo kaulimbiu hiyo itatekelezwa ipasavyo bila mchango wao wa kiutendaji.
Kikao Kazi hicho cha siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu chenye lengo la kuboresha utendaji kazi Serikalini kiliandaliwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kushirikiana Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Innocent
Bashungwa akifunga kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara
na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma
kilichofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa
Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI,
Mhe. Innocent Bashungwa (hayupo pichani) alipokuwa akifunga kikao kazi cha siku mbili cha watumishi hao
kilichofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi atoa maelezo ya awali kabla ya
kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Innocent Bashungwa kufunga kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo
vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma
kilichofanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Dkt. Laurean
Ndumbaro akielezea namna kikao cha siku mbili cha
Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika
Utumishi wa Umma kilivyofanyika kabla ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Innocent
Bashungwa kufunga kikao kazi hicho kilichofanyika jijini
Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Innocent
Bashungwa akiteta na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi
kabla ya kufunga kikao kazi cha siku mbili
cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika
Utumishi wa Umma kilichofanyika jijini Dodoma.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Innocent Bashungwa akitunuku
tuzo kwa mwakilishi wa taasisi ya serikali kwa kutambua utendaji kazi bora
uliofanywa ka taasisi hiyo kabla ya kufunga kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu
wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi
wa Umma kilichofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika
Utumishi wa Umma, ACP. Ibrahim Mahumi akiwasilisha mada kuhusu tathmini ya
utekelezaji wa Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara kwenye kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya
Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichofanyika
jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi, Bw. Nolasco
Kipanda akiwasilisha mada kwenye kikao kazi cha
siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa
Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA Serikalini, Bw. Priscus Kiwango
akiwasilisha mada kuhusu usimamizi na matumizi ya TEHAMA Serikalini wakati wa kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya
Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichofanyika
jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Mishahara na Masilahi, Bibi Mariam
Mwanilwa akiwasilisha mada kuhusiana na Miundo ya Maendeleo ya Utumishi wakati
wa kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya
Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichofanyika jijini
Dodoma.