Na. James K. Mwanamyoto-Dodoma
Tarehe 31 Machi, 2022
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista
Mhagama ameielekeza Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kushughulikia
malalamiko na tuhuma zinazowasilishwa na wananchi kuhusu Viongozi wa Umma
wanaokiuka maadili ili kuwa na viongozi waadilifu wanaotekeleza majukumu yao
kwa maendeleo ya taifa.
Mhe. Jenista
ameyasema hayo leo alipokutana na Menejimenti ya Sekretarieti hiyo kwa lengo la
kuhimiza uwajibikaji na kukagua ujenzi wa Ofisi za makao makuu ya Sekretarieti
ya Maadili ya Viongozi wa Umma jijini Dodoma.
Mhe.
Jenista amesema, kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu mwenendo wa baadhi
ya Viongozi wa Umma kwenye eneo la uadilifu, hivyo Sekretarieti ya Maadili ya
Viongozi ina jukumu kubwa la kuyapokea malalamiko hayo na kuyafanyia kazi ili
viongozi wawe na maadili na miiko ya uongozi unaotakiwa.
“Mnapokea
tuhuma zinazohusu ukiukwaji wa maadili ya viongozi, hivyo mna jukumu la kufanya
uchunguzi ili kuthibitisha ukweli wa tuhuma hizo na kuzifanyia kazi kwa mujibu
wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na.13 ya Mwaka 1995,” Mhe. Jenista
amesisitiza.
Aidha,
Mhe. Jenista ameitaka Sekretarieti hiyo kutoa elimu ya uzingatiaji wa maadili
kwa Viongozi wa Umma ili wasikiuke maadili na miiko ya uongozi kwa kutokuwa na
uelewa.
“Katika
kipindi hiki tujikite zaidi kutoa elimu ya uzingatiaji wa maadili ili viongozi
wetu wa umma waelewe umuhimu wa kuzingatia maadili katika utekelezaji wa
majukumu yao ya kila siku, hii inatokana na baadhi ya viongozi kukiuka maadili
kwa kutokuelewa na hatimaye kujihusisha na vitendo vya ukiukaji wa maadili.”
Mhe. Jenista amehimiza.
Amesema
azma ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan
inamtaka kila Mtanzania ajifunze kutii sheria bila shuruti na kama ni kiongozi basi
atii Sheria ya Maadili ya Viongozi bila kushurutishwa, hivyo suala ya utoaji wa
elimu ya uzingatiaji wa maadili haliepukiki ili kuwa na uongozi unaozingatia
utawala bora.
Kwa upande wake Kamishna
wa Sekretarieti ya Maadili wa Viongozi wa Umma, Mhe. Jaji Sivangilwa
Sikalalilwa Mwangesi amezitaja kazi za msingi za Sekretarieti hiyo kuwa ni
pamoja na kupokea matamko yanayotakiwa kutolewa na Viongozi wa Umma kwa mujibu
wa Katiba na Sheria, kupokea malalamiko na tuhuma za ukiukwaji wa Sheria ya
Maadili ya Viongozi wa Umma, kuanzisha na kufanya uchunguzi dhidi ya tuhuma za
ukiukwaji wa maadili na kufanya uhakiki wa Matamko na Rasilimali na Madeni
yanayotolewa na Viongozi wa Umma kwa mujibu wa Sheria.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Jenista Mhagama akizungumza na Menejimenti
ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma alipokutana na Menejimenti hiyo
kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji na kukagua ujenzi wa Ofisi za makao makuu ya
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma jijini Dodoma. Kulia kwake ni
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Mhe. Jaji Sivangilwa
Mwangesi na kushoto kwake ni Mkurugenzi Idara ya Ujenzi Wakala wa Majengo
Tanzania (TBA) Mhandisi Loishorwa Likimaitare.
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi, Mhe. Jaji Sivangilwa
Mwangesi akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Jenista Mhagama kuzungumza na Menejimenti hiyo kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji na kukagua ujenzi
wa Ofisi za makao makuu ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma jijini
Dodoma.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Jenista Mhagama akiwa katika kikao kazi na Menejimenti ya Sekretarieti ya Maadili ya
Viongozi wa Umma alipokutana na Menejimenti hiyo kwa lengo la kuhimiza
uwajibikaji na kukagua ujenzi wa Ofisi za makao makuu ya Sekretarieti ya
Maadili ya Viongozi wa Umma jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwasili eneo la Ujenzi wa Ofisi ya makao makuu ya Sekretarieti
ya Maadili ya Viongozi wa Umma unaoendelea jijini Dodoma wakati wa ziara yake
ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kukagua ujenzi huo. Kushoto kwake
ni Kamishna wa Sekretarieti wa Maadili ya Viongozi, Mhe. Jaji Sivangilwa
Mwangesi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama
akimsikiliza Meneja wa Mkoa Dodoma, Mbunifu Majengo (TBA) Bw. Victor Balthazar
alipokuwa akimuonesha mchoro wa jengo la ofisi ya
Sekretarieti ya Maadili Makao Makuu wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga
kukagua Mradi wa Ujenzi wa Jengo hilo jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akimsikiliza Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi, Mhe.
Jaji Sivangilwa Mwangesi alipokuwa akimuonesha miundombinu wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuhimiza
uwajibikaji na kukagua ujenzi wa ofisi hizo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akitoka kukagua jengo la la ofisi za makao makuu ya Sekretarieti ya
Maadili ya Viongozi wa Umma linaloendelea kujengwa jijini Dodoma na Mkandarasi
ambaye ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuhimiza
uwajibikaji na kukagua ujenzi wa ofisi hizo.
Muonekano wa jengo la ofisi za makao makuu ya Sekretarieti ya
Maadili ya Viongozi wa Umma linaloendelea kujengwa jijini Dodoma na Mkandarasi
ambaye ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)