Wednesday, February 27, 2019

WAAJIRI WANAOKWAMISHA USHUGHULIKIAJI WA RUFAA ZA MASHAURI YA WATUMISHI WA UMMA KUCHUKULIWA HATUA ZA KINIDHAMU



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akisalimiana na Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bi. Immaculate Ngwale alipowasili Ofisi za Tume ya Utumishi wa Umma, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam kuzungumza na watumishi wa Tume hiyo.

Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji Mstaafu Dkt. Stephen Bwana akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) kuzungumza na watumishi wa Tume wakati wa kikao kazi kilichofanyika Ofisi ya Tume ya Utumishi wa Umma, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Katibu, Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Richard Odongo.

Kaimu Katibu, Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Richard Odongo akitoa neno la utangulizi wakati wa kikao kazi kati ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma kilichofanyika Ofisi za Tume ya Utumishi wa Umma, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi kati yake na watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma, kilichofanyika Ofisi za Tume ya Utumishi wa Umma, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma Jaji Mstaafu, Dkt. Stephen Bwana.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akizungumza  na Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma kabla ya kuanza kikao kazi kati yake na watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma, Ofisi za Tume ya Utumishi wa Umma, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu, Tume ya Utumishi wa Umma, Bi. Rosy Elipenda akitoa neno la shukrani kwa niaba ya watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma wakati wa kikao kazi kati ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma, kilichofanyika Ofisi za Tume ya Utumishi wa Umma, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.

TAHADHARI KUHUSU VITENDO VYA UDANGANYIFU NA UTAPELI


SERIKALI YAISHUKURU CHINA KWA KUIPATIA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA KOMPYUTA MPAKATO 20



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Wang Ke alipowasili Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania kukabidhi kompyuta kwa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika kwenye ukumbi wa chuo hicho jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano ya kompyuta kwa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika kwenye ukumbi wa chuo hicho jijini Dar es Salaam.

Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Henry Mambo akitoa neno la utangulizi wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya kompyuta kwa Chuo chake yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Wang Ke akizungumza kabla ya kukabidhi kompyuta kwa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), Dkt. Charles Msonde.

Baadhi ya watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) (hayupo pichani) katika hafla fupi ya makabidhiano ya kompyuta kwa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika kwenye ukumbi wa chuo hicho jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akimkabidhi zawadi Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Wang Ke baada ya hafla fupi ya makabidhiano ya kompyuta kwa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika kwenye ukumbi wa chuo hicho jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akipokea moja ya kompyuta mpakato kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Wang Ke katika hafla fupi ya makabidhiano ya kompyuta kwa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika kwenye ukumbi wa chuo hicho jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro.

Tuesday, February 26, 2019

AFISA UTUMISHI MKURANGA AONYWA KUTUMIA CHEO CHAKE VIBAYA KUOMBA RUSHWA YA NGONO KWA WATENDAJI WA VIJIJI



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.

Baadhi ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani), wakati wa kikao kazi cha watumishi hao na Naibu Waziri huyo chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisikiliza hoja mbalimbali zilizowasilishwa na  watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, wakati wa kikao kazi na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji. 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisisitiza uadilifu kwa  watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, wakati wa kikao kazi na watumishi hao  chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji. 

Monday, February 25, 2019

WATUMISHI WA UMMA NCHINI MARUFUKU KUTUMIKA KISIASA



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kabla ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF Wilayani Kisarawe. 

Baadhi ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani), wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao chenye  lengo la kuhimiza uwajibikaji, kabla ya Naibu Waziri huyo  kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF Wilayani Kisarawe. 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mhe. Jokate Mwegelo, wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa Halmashauri hiyo chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji. 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na wananchi na wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa kijiji cha Kitanga wilayani Kisarawe wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani humo. 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akishuhudia baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na wanufaika wa TASAF katika kijiji cha Kitanga wilayani Kisarawe wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani humo. Aliyeambatana naye ni  Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mhe. Jokate Mwegelo.

MHE.MKUCHIKA ATOA SIKU 34 KWA AFISA UTUMISHI HALMASHAURI YA WILAYA YA KILWA KUWEKA TAARIFA SAHIHI ZA WATUMISHI KWENYE MFUMO WA HCMIS



Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Dkt. Bora Haule akitoa utambulisho wa makundi ya watumishi waliohudhuria kikao kazi kati ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kilichofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii, wilayani Kilwa.


Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe.Christopher Ngubiagai akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) kuzungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Kilwa katika kikao kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii, wilayani Kilwa.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi (hawapo pichani) katika kikao kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii, wilayani Kilwa. Kushoto ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Dkt. Bora Haule na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe.Christopher Ngubiagai (kulia kwake).


Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii, wilayani Kilwa


Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Bi. Jovita Buyobe akijibu hoja wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Kilwa kilichofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii, wilayani Kilwa.

Sunday, February 24, 2019

MHE.MKUCHIKA APONGEZA WANUFAIKA WA TASAF WA KIJIJI CHA MKWANYULE WILAYANI KILWA KWA KUTUMIA VIZURI FEDHA ZA TASAF KUJIKWAMUA KIUCHUMI



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akizungumza na wanufaika wa TASAF wa kijiji cha Mkwanyule wilayani Kilwa katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mkwanyule wilayani humo. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Christopher Ngubiagai.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Christopher Ngubiagai akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), kuzungumza na wanufaika wa TASAF wa kijiji cha Mkwanyule wilayani Kilwa (hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mkwanyule wilayani humo.

Wakazi wa kijiji cha Mkwanyule wilayani Kilwa wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) (hayupo pichani) katika mkutano wa Waziri huyo na wanufaika wa TASAF uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mkwanyule wilayani Kilwa.

Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kusini, Mhe. Selemani Bungara akiishukuru serikali kwa kuufikisha Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wilayani kwake wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na wanufaika wa TASAF uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mkwanyule wilayani humo.

Mmoja wa wanufaika wa TASAF mkazi wa kijiji cha Mkwanyule Bi. Mwanahamisi Ally Ukwenda akishuhudia namna alivyonufaika na TASAF wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na wanufaika wa TASAF uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mkwanyule wilayani Kilwa. Kushoto kwake ni mnufaika mwenzie Bi. Atili Masoud Swalehe.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) (kulia) akikagua mradi wa mbuzi unaomilikiwa na Bw. Hassan Charahani (kushoto) mara baada ya kumaliza mkutano kati yake na wanufaika wa TASAF uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mkwanyule wilayani Kilwa.

SERIKALI HAITOMUACHA SALAMA MTUMISHI YEYOTE ATAKAEKULA FEDHA ZA UMMA KWA MASILAHI BINAFSI


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao  chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao, mara baada ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF Wilayani Bagamoyo.

Baadhi ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani), wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao chenye  lengo la kuhimiza uwajibikaji, mara baada ya  kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF Wilayani Bagamoyo.

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe. Zainab R. Kawawa akimueleza  Dkt. Mwanjelwa hatua alizochukua dhidi ya changamoto ya ubadhirifu wa fedha za umma wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa Halmashauri hiyo chenye  lengo la kuhimiza uwajibikaji,  mara baada ya  kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF Wilayani Bagamoyo.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb)  na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe. Zainab R. Kawawa wakisikiliza maelezo ya kiutumishi toka kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Bw. Shabani Milao wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa Halmashauri hiyo chenye  lengo la kuhimiza uwajibikaji.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisisitiza nidhamu katika matumizi ya fedha za umma  kwa  watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao chenye lengo la  kuhimiza uwajibikaji.