Tuesday, October 6, 2026

WAZIRI KIKWETE AHITIMISHA MICHEZO YA SHIMIWI 2026, AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUJAZA PEPMIS NA KUSIMAMIA MIFUMO YA UTENDAJI KAZI

Na. Veronica Mwafisi-Moshi

07 Oktoba, 2026.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amewataka Watumishi wa Umma waliokuwa katika michezo ya SHIMIWI watakaporudi katika maeneo yao ya kazi, kufanya kazi kwa kusimamia mifumo ya utekelezaji wa majukumu mbalimbali waliyokasimiwa ikiwemo ujazaji wa Mfumo wa Upimaji wa Utendaji kazi (PEPMIS).

Waziri Kikwete amezungumza hayo leo tarehe 07 Oktoba, 2026 wakati akihitimisha rasmi michezo ya SHIMIWI iliyofanyika katika Mkoa wa Kilimanjaro.

“Nitoe wito kwenu watumishi wenzangu, leo tunapohitimisha rasmi michezo hii ya SHIMIWI, mtakaporudi katika maeneo yenu ya kazi  hakikisheni mnasimamia Mifumo ya utekelezaji wa majukumu yenu ikiwemo ujazaji wa PEPMIS,” amesema Mhe. Kikwete

Waziri Kikwete amesema, taasisi zote za Serikali zina utaratibu mzuri wa kumpima kila mtumishi kiutendaji hivyo, mafanikio ya mtu mmoja mmoja, Idara na taasisi kwa ujumla yatasaidia kujua utendaji wa Serikali nzima.

Ameongeza kuwa, ni vema kujenga ushirikiano kwa washiriki wa michezo hiyo ya SHIMIWI ambao utawasaidia katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali katika maeneo yao ya kazi.

“Mkusanyiko huu mkubwa wa Watumishi wa Umma unatusaidia kuwa na uelewa wa masuala mbalimbali pamoja na kujenga ushirikiano utakaoleta mafanikio kwenye maeneo yenu ya kazi,” ameongeza Mhe. Kikwete

Aidha, Mhe. Ridhiwani amesisitiza suala la usimamizi wa Rasilimalifedha kwa Viongozi wa Klabu mbalimbali na kutaka kila ofisi kutenga bajeti kwa ajili ya mipango ya mwaka unaofuata.

Akihitimisha hotuba yake, Mhe. Ridhiwani amesema kutokana na Kaulimbiu ya SHIMIWI 2026, inayosema Watumishi Tupo Tayari kwa AFCON 2027, kila mtumishi katika sekta aliyopo ahakikishe anaunga mkono mashindano hayo kwa ustawi wa Taifa letu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Watumishi wa Umma wakati akifunga Mashindano ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kutoka kushoto) akifurahia kuwakabidhi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kombe la ushindi wa jumla mara baada ya Waziri huyo kufunga Mashindano ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro. Aliyevaa koti jeusi ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili.


Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati Waziri huyo alipokuwa akifunga Mashindano ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro.


Sehemu ya Watumishi wa Umma ambao ni wanamichezo kutoka katika Wizara mbalimbali wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati Waziri huyo alipokuwa akifunga Mashindano ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia) akimkabidhi kombe la mshindi wa kwanza kwa upande wa Netiboli Nahodha wa timu ya Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Elizabeth Fusi mara baada ya Waziri huyo kufunga Mashindano ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia) akimkabidhi kombe la ushindi mmoja wa watumishi walioshinda mara baada ya Waziri huyo kufunga Mashindano ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro.


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili (kushoto) akifurahia mara baada ya timu ya netiboli kutoka Ofisi hiyo kupata kombe la ushindi wa kwanza kwa upande wa Netiboli wakati wa kufungwa Mashindano ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa SHIMIWI, Bw. Daniel Mwalusamba  kabla ya Waziri huyo kufunga Mashindano ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro.


Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambao ni wanamichezo walioshiriki Mashindano ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI)  wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) kufunga mashindano hayo yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro


Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambao ni wanamichezo walioshiriki Mashindano ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI)  wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) kufunga mashindano hayo yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kufunga Mashindano ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) akisalimiana na Viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Chuo cha Polisi Tanzania (CCP MOSHI).


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa tatu kutoka kushoto) akifurahia jambo na Watendaji wa Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) na Viongozi mbalimbali kutoka katika Wizara mara baada ya Waziri huyo kufunga Mashindano ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI)


Watumishi wa Umma kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakifurahia ushindi mara baada ya kukabidhiwa kombe la ushindi wakati wa kufungwa kwa Mashindano ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa tatu kutoka kulia) akisikiliza maelezo ya awali kabla ya kushuhudia mchezo wa kuvuta kamba kabla ya Waziri huyo kufunga Mashindano ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro.


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili (aliyevaa koti jeusi) akifuatilia kwa umakini mchezo wa kuvuta kamba wakati wa Mashindano ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro. Wa nne kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka katika Ofisi ya Rais-UTUMISHI. Wengine ni Wakurugenzi na Watumishi kutoka katika Wizara mbalimbali.


Viongozi na Watendaji wa Wizara na Taasisi mbalimbali wakishuhudia mchezo wa kuvuta kamba wakati wa Mashindano ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) kabla ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) kufunga mashindano hayo yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro.











 

MADAI YA FIDIA NI USIMAMIZI WA RASILIMALIWATU SI FADHILA: KATIBU MKUU MKOMI

Uzembe na ucheleweshaji wa taarifa unaofanywa na baadhi ya Maafisa Rasilimaliwatu Serikalini unaathiri mchakato wa kushughulikia madai ya fidia kwa mfanyakazi wakati anapopata ajali, ugonjwa au kifo anapokuwa katika utekelezaji wa makumu ya kikazi.

Maneno hayo yalisemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Juma Mkomi Oktoba 7, 2026 wakati akifungua mafunzo yaliyoandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa Maafisa Rasilimaliwatu na Wahasibu wa Wizara, Taasisi za Umma zilizopo Dodoma na Wilaya zote za Mkoa Dodoma kuhusu taratibu za kuwasilisha na kushughulikia madai ya fidia kwa wafanyakazi yaliyofanyika katika ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma.

Bw. Mkomi alisema kuwa hapendi kuona mfanyakazi kwa bahati mbaya anapata ajali au ugonjwa unaotokana na kazi lakini kutokana na kutokuwepo kwa taarifa sahihi, nyaraka muhimu au uelewa wa taratibu, anashindwa kupata haki yake kwa wakati.

“Mafunzo haya ni muhimu kwenu Maafisa Rasilimaliwatu kwa kuwa ndio kiungo kati ya mwajiri, mfanyakazi na mifumo mbalimbali inayohusika na usimamizi wa rasilimaliwatu, ninaamini baada ya mafunzo haya mtakuwa na uelewa wa hatua za kuchukua pale mfanyakazi anapopata ajali au ugonjwa unaotokana na kazi au anapofariki kutokana na mazingira yanayohusiana na kazi na kuharakisha upatikanaji wa fidia” alisema Bw. Mkomi.

Aliongeza kuwa, kuwasilisha taarifa sahihi, zenye ukamilifu na kwa wakati ni jambo muhimu katika mchakato wa fidia. Hivyo, mafunzo hayo ni muhimu kwa kuwa yanagusa moja kwa moja ustawi wa watumishi, usimamizi wa rasilimaliwatu, uwajibikaji wa mwajiri na utekelezaji wa haki za wafanyakazi.

Bw. Mkomi alisisitiza kuwa Taasisi zote za Umma ambazo kwa mujibu wa taratibu ni waajiri, zina wajibu wa kuhakikisha zinatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria na taratibu zinazohusu fidia kwa wafanyakazi.

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ni chombo kinachohakikisha wafanyakazi wanaopata madhara mathalani ajali au ugonjwa uliosababishwa na kazi wanapata fidia na huduma stahiki kwa mujibu wa sheria. Vilevile mfuko unaweka ulinzi wa mfanyakazi na wategemezi wake, uzuiaji wa ajali na magonjwa yatokanayo na kazi, pamoja na wajibu wa mwajiri katika kumlinda mfanyakazi

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma,  Bw. Juma Mkomi akizungumza na Maafisa Rasilimaliwatu na Wahasibu kutoka Wizara na Taasisi za Umma Mkoa wa Dodoma kwenye Mafunzo kuhusu taratibu za kuwasilisha na kushughulikia madai ya fidia kwa wafanyakazi yaliyofanyika Oktoba 7, 2026 katika ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma.

Maafisa Rasilimaliwatu na Wahasibu wa Wizara na Taasisi za Umma zilizopo Dodoma wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (hayupo pichani) wakati akifungua Mafunzo kuhusu taratibu za kuwasilisha na kushughulikia madai ya fidia kwa wafanyakazi katika ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma

Maafisa Rasilimaliwatu na Wahasibu wa Wizara na Taasisi za Umma zilizopo Dodoma wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (hayupo pichani) wakati akifungua Mafunzo kuhusu taratibu za kuwasilisha na kushughulikia madai ya fidia kwa wafanyakazi katika ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma

Maafisa Rasilimaliwatu na Wahasibu wa Wizara na Taasisi za Umma zilizopo Dodoma wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (hayupo pichani) wakati akifungua Mafunzo kuhusu taratibu za kuwasilisha na kushughulikia madai ya fidia kwa wafanyakazi katika ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma



Maafisa Rasilimaliwatu na Wahasibu wa Wizara na Taasisi za Umma zilizopo Dodoma wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (hayupo pichani) wakati akifungua Mafunzo kuhusu taratibu za kuwasilisha na kushughulikia madai ya fidia kwa wafanyakazi katika ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma mara baada ya Katibu Mkuu huyo kuwasili katika Ofisi ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kufungua mafunzo kwa Maafisa Rasilimaliwatu na Wahasibu kuhusu taratibu za kuwasilisha na kushughulikia madai ya fidia kwa wafanyakazi Jijini Dodoma.


Maafisa Rasilimaliwatu na Wahasibu wa Wizara na Taasisi za Umma zilizopo Dodoma wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (hayupo pichani) wakati akifungua Mafunzo kuhusu taratibu za kuwasilisha na kushughulikia madai ya fidia kwa wafanyakazi katika ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma 



 

MHE. KIKWETE AZIELEKEZA MAMLAKA ZA NIDHAMU KUZINGATIA USIRI WA TAARIFA BINAFSI ZA WATUMISHI WAKATI WA KUJADILI AJENDA ZA MASHAURI YA KINIDHAMU

Na Veronica Mwafisi – Tanga

Tarehe 06 Oktoba, 2026

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amefungua kikao kazi cha Maafisa Rasilimaliwatu na Maafisa Sheria jijini Tanga na kutoa maelekezo mahususi katika kulinda ustawi wa Utumishi wa Umma na taifa kwa ujumla.

Akifungua kikao kazi hicho leo tarehe 6 Oktoba, 2026, Mhe. Kikwete amesema katika siku za karibuni kumeibuka tabia ya baadhi ya Mamlaka za Nidhamu kutoa taarifa za mashauri ya kinidhamu kwenye vyombo vya habari kinyume na Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma.

Kufuatia tabia hiyo, Mhe. Kikwete amezielekeza Mamlaka zote za nidhamu katika Taasisi kuzingatia usiri wa taarifa binafsi za watumishi wakati wa kujadili ajenda za mashauri ya kinidhamu.

Amesema pia katika mchakato wa kushughulikia masuala ya nidhamu, kama ilivyoelekezwa katika Sheria na Kanuni, watu wote ambao hawatokuwa wanahusika katika mchakato wa uendeshaji wa mashauri ya nidhamu hawatapaswa kuwepo wala kujua kile kilichoendelea katika ushughulikiwaji wa shauri hilo.

Vilevile amesema Mamlaka za nidhamu hazipaswi kutangaza maamuzi ya mashauri ya nidhamu katika vyombo vya habari kama inavyojitokeza mara kwa mara katika baadhi ya Halmashauri na badala yake zinapaswa kufuata utaratibu ulioainishwa katika Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma kupitia Kanuni D. 28 ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma Toleo la mwaka 2009.

“Ninatambua kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI tayari wameshatoa maelekezo kupitia barua. Na mimi kama Msimamizi wa Utumishi wa Umma kupitia hadhara hii nimetoa melekezo yangu, ni mategemeo yangu kwamba maelekezo haya yatatekelezwa ipasavyo na tutaendelea kulinda hadhi na heshima ya Utumishi wa Umma,” ameongeza.

Amewataka Maafisa Utumishi hao kuwa wabunifu katika kutatua changamoto za Watumishi wa Umma, akisisitiza pamoja na kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo lakini busara pia itumike, wakiona wanashindwa kufanya hivyo ni vema wakawasiliana na Ofisi ya Rais-UTUMISHI kuona namna ya kufanya.

Amesema, Serikali inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2025 imeweka wazi malengo yake kuhakikisha mazingira ya Utumishi yanakuwa bora kupitia kaulimbiu ya “KAZI NA UTU.” “Mtoe haki kwa wakati ili kuwapatia ari Watumishi wa Umma kufanya kazi.” ameongeza

Aidha, ameendelea kuhimiza matumizi ya kidijitali katika Utumishi wa Umma. “Serikali tumefanikiwa sana, naendelea kuwashukuru wataalamu wa e-GA na Maafisa TEHAMA sasa hivi hakuna kukutana kutana.”

Katika hatua nyingine Mhe. Kikwete amesisitiza utoaji huduma unaozingatia wananchi katika maeneo makuu manne ambayo ni upatikanaji (accessibility), uitikivu (responsiveness), uwazi (transparency) na uwajibikaji (accountability) katika utoaji huduma.

Amesema katika upatikanaji wa huduma, Serikali inalenga kuhakikisha Taasisi za umma zinasikiliza maoni na kurekebisha taratibu zao ili kutatua changamoto halisi kwa haraka, kutoa taarifa kwa uwazi ili wananchi waelewe jinsi maamuzi yanavyofanywa na jinsi rasilimali za umma zinavyotumika na Watumishi wa umma wanapaswa kuwajibika kwa wananchi. “Hii yote ni kuhakikisha kuwa kuna ushirikiano mkubwa kati ya Mtoa huduma ambaye ni Mtumishi wa Umma na Mpokea huduma ambaye ni Mwananchi.” Ameongeza.

“Mhe. Rais anataka sisi watoa huduma tuwe karibu na wananchi, tunahitaji utulivu na uadilifu katika kutatua kero za wananchi. Mtumishi wa Umma anatakiwa kuwa na nyaraka muhimu katika kutekeleza majukumu yake ikiwemo Katiba ya Nchi, Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu –UTUMISHI, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili amesema Ofisi ya Rais-UTUMISHI kama msimamizi na mtunzaji Mkuu wa Sheria ya Utumishi wa Umma, imekuwa na jukumu la kukutana ili kukumbushana Taratibu na Sheria kwa lengo la kuwekana sawa katika uzingatiwaji wa Sheria.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Hilda Kabisa amesema jumla ya watumishi 218 kutoka Sekretarieti za Mikoa, Taasisi za Umma na Mamlaka za Serikali za Mitaa wamealikwa kushiriki kikao kazi hicho.

Mada mbalimbali zimewasilishwa katika kikao kazi hicho ikiwemo Usimamizi wa Maadili na Malalamiko katika Utumishi wa Umma, Ushughulikiaji wa Mashauri ya Nidhamu katika Utumishi wa Umma, Ushughulikiaji wa Malimbikizo ya Mishahara kwa Watumishi wa Umma waliopandishwa vyeo, waliofukuzwa kazi na kurejeshwa katika Utumishi wa Umma na Mamlaka za Rufaa, Ushughulikiaji na Ulipaji wa Mafao kwa Watumishi wa Umma baada ya kustaafu, Ushughulikiaji wa Uhamisho, Upandishwaji Vyeo na Ubadilishwaji Kada katika Utumishi wa Umma.

Kikao kazi hicho kimelenga kubaini na kutambua changamoto za Utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma Sura ya 298 na Kanuni zake za mwaka 2022. Na kinawashirikisha Maafisa Rasilimaliwatu na Wanasheria kufanya kazi kwa pamoja ili kuimarisha utendaji kazi na kuboresha utoaji wa huduma kwa Watumishi wa Umma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu kilicholenga kutambua changamoto za utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298 na Kanuni zake kilichofanyika leo tarehe 06 Oktoba, 2026 jijini Tanga.



Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa hao   kilicholenga kutambua changamoto za utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298 na Kanuni zake kilichofanyika leo tarehe 06 Oktoba, 2026 jijini Tanga.


Mwakilishi wa Katibu Mkuu–UTUMISHI ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) kufungua kikao kazi cha Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu kilicholenga kutambua changamoto za utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298 na Kanuni zake kilichofanyika leo tarehe 06 Oktoba, 2026 jijini Tanga.


Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa hao   kilicholenga kutambua changamoto za utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298 na Kanuni zake kilichofanyika leo tarehe 06 Oktoba, 2026 jijini Tanga.


Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa hao   kilicholenga kutambua changamoto za utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298 na Kanuni zake kilichofanyika leo tarehe 06 Oktoba, 2026 jijini Tanga.


Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Bi. Hilda Kabissa akielezea malengo ya Kikao kazi cha Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu kabla ya Mgeni Rasmi ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete kufungua kikao kazi hicho kilicholenga kutambua changamoto za utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298 na Kanuni zake kilichofanyika leo tarehe 06 Oktoba, 2026 jijini Tanga.


Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa hao   kilicholenga kutambua changamoto za utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298 na Kanuni zake kilichofanyika leo tarehe 06 Oktoba, 2026 jijini Tanga.


Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa hao   kilicholenga kutambua changamoto za utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298 na Kanuni zake kilichofanyika leo tarehe 06 Oktoba, 2026 jijini Tanga.


Sehemu ya Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Ofisi hiyo, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akifungua kikao kazi cha Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu kilicholenga kutambua changamoto za utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298 na Kanuni zake kilichofanyika leo tarehe 06 Oktoba, 2026 jijini Tanga.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi na Maafisa kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na IKULU mara baada ya Waziri huyo kufungua kikao kazi cha Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu kilicholenga kutambua changamoto za utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298 na Kanuni zake kilichofanyika leo tarehe 06 Oktoba, 2026 jijini Tanga. Waliokaa wengine ni Viongozi mbalimbali waliohudhuria kikao kazi hicho.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu mara baada ya kufungua kikao kazi cha Maafisa hao kilicholenga kutambua changamoto za utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298 na Kanuni zake kilichofanyika leo tarehe 06 Oktoba, 2026 jijini Tanga. Waliokaa wengine ni Viongozi mbalimbali waliohudhuria kikao kazi hicho.