Na Antonia Mbwambo- Dodoma.
Tarehe 13/10/2025
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI ambaye
ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bw. Xavier Daudi ametoa wito kwa Watumishi
wa Umma nchini kubadilika kimtazamo katika utendaji ili kufikia malengo ya Dira
ya Taifa ya Maendeleo 2050 ikiwemo matumizi sahihi ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (TEHAMA).
Kaimu Katibu Mkuu Bw. Daudi amesema, Watumishi
wa Umma kubadilika kimtazamo katika utendaji ni jambo muhimu kwani kunakuwa na
ufanisi wa wa kazi unaowezesha kuwa na Taifa jumuishi lenye ustawi, haki na
linalojitegemea.
“Ninatoa wito kwenu, msitekeleze majukumu yenu
kwa mazoea, kupitia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, mbadilike kiutendaji ili
kuendana na mabadiliko yakiwemo ya kidijiti kwa kuleta ubunifu na mawazo chanya
yatakayoiwezesha serikali kufikia malengo yake ya kutoa huduma bora kwa
wananchi kupitia matumizi sahihi ya mifumo ya TEHAMA,” Bw. Daudi alisema.
Kwa upande wake Meneja Mawasiliano Serikalini
kutoka Tume ya Taifa ya Mipango (NPC), Bw. Titus Kaguo wakati akiwasilisha mada
kwa watumishi hao kuhusu Malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, amesema mabadiliko
makubwa ya Sayansi na Teknolojia ni kichocheo kikubwa cha maendeleo katika
Taifa letu ambapo Dira hii imelenga kuwa kufikia mwaka 2050, asilimia 70 ya Watanzania
watakuwa wanatumia mifumo ya TEHAMA na asilimia 80 ya huduma mbalimbali za kiserikali zitakuwa zikitolewa
kidiji ili kuleta Ufanisi katika Utendaji.
Wakurugenzi wa Idara na vitengo mbalimbali kutoka Ofisi ya
Rais-UTUMISHI wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na mwezeshaji ambaye ni
Meneja Mawasiliano Serikalini kutoka Tume ya Taifa ya Mipango (NPC), Bw. Titus
Kaguo (hayupo pichani) leo tarehe13/10/2025 katika mafunzo ambayo hutolewa kila
siku ya jumatatu kwenye Ofisi hiyo iliyopo Mtumba
jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi (aliyesimama mbele) akizungumza na watumishi wa Ofisi hiyo baada ya wasilisho la mada ya Malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 lililotolewa leo tarehe13/10/2025 na Meneja Mawasiliano Serikalini kutoka Tume ya Taifa ya Mipango (NPC), Bw. Titus Kaguo katika mafunzo ya kuwajengea watumishi wa Ofisi hiyo uwezo wa kiutendaji, ambayo hutolewa kila siku ya jumatatu kwenye Ofisi hiyo iliyopo Mtumba jijini Dodoma.
Meneja Mawasiliano Serikalini kutoka
Tume ya Taifa ya Mipango (NPC), Bw. Titus Kaguo (aliyesimama mbele) akiwasilisha mada
ya Malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 katika
mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji watumishi wa Ofisi ya
Rais-UTUMISHI,yaliyofanyika leo tarehe 13/10/2025 katika Ofisi hiyo iliyopo
Mtumba jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi (wa
kwanza kushoto aliyevaa miwani) akifurahia jambo alipokuwa akifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa katika mafunzo ya kuwajengea uwezo
wa kiutendaji watumishi wa Ofisi hiyo ambayo hufanyika kila siku ya jumatatu
katika Ofisi hiyo Mtumba Dodoma.
Watumishi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakifuatilia mada
iliyokuwa ikiwasilishwa na mwezeshaji ambaye ni Meneja Mawasiliano Serikalini
kutoka Tume ya Taifa ya Mipango (NPC), Bw. Titus Kaguo (hayupo pichani) kwenye
mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji watumishi wa Ofisi hiyo ambayo
hufanyika kila siku ya jumatatu katika Ofisi hiyo Mtumba Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi
akiteta jambo na Mkurugenzi wa Mipango wa Ofisi hiyo Bw. Cosmas Ngangaji wakati
wa mafunzo ya kuwajengea watumishi wa Ofisi hiyo uwezo wa kiutendaji
yaliyofanyika katika eneo la Ofisi hiyo lililopo Mtumba jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Idara na vitengo pamoja na
watumishi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifuatilia mada iliyokuwa
ikiwasilishwa na mwezeshaji ambaye ni Meneja Mawasiliano Serikalini kutoka Tume
ya Taifa ya Mipango (NPC), Bw. Titus Kaguo (hayupo pichani) leo
tarehe13/10/2025 katika mafunzo ambayo hutolewa kila siku ya jumatatu kwenye
Ofisi hiyo iliyopo Mtumba jijini Dodoma.
Meneja Mawasiliano Serikalini kutoka Tume ya Taifa ya
Mipango (NPC), Bw. Titus Kaguo (aliyesimama mbele, mwenye miwani) akitoa
ufafanuzi na majibu ya maswali yaliyokuwa yakiulizwa na watumishi baada ya kuhitimisha
wasilisho la mada ya Malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 lililotolewa
katika eneo la Ofisi ya Rais-UTUMISHI leo tarehe 13/10/2025 jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment