Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Tarehe 28 Oktoba, 2025
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora imewapongeza Watumishi wa Ofisi hiyo waliofikia ukomo katika
Utumishi wa Umma kutokana na utumishi uliotukuka kwa kutekeleza majukumu yao
kwa ufanisi ambao umechangia kutolewa kwa huduma bora katika Idara walizokuwa
wakifanyia kazi.
Akitoa pongezi hizo kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi
ya Rais-UTUMISHI, leo tarehe 27 Oktoba, 2025, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, SACP. Ibrahim Mahumi amesema kufikisha umri wa
miaka 60 sio mchezo, ni jambo la kumshukuru Mungu.
“Hongereni sana, mmeondoka katika Utumishi wa
Umma mkiwa na sifa nzuri katika kulitumikia taifa na mkiwa na afya njema ni
mfano mzuri wa kuigwa na tunaoendelea kufanya kazi,” amesema SACP. Mahumi.
SACP. Mahumi amemshukuru Katibu Mkuu-UTUMISHI
kupitia Idara ya Utawala kwa kuanzisha utamaduni wa kukutana kila Jumatatu na
kuwa na ubunifu mbalimbali wa kuwaweka watumishi pamoja kwa lengo la kuboresha
utendaji.
“Tangu jambo hili la kukutana pamoja kila siku ya
Jumatatu kupata elimu ya kuboresha utendaji kumekuwa na mabadiliko makubwa ya
kiutendaji, nawasihi tuendelee kuyatumia mafunzo haya kuboresha utendaji
zaidi.” Amesisitiza.
Akitoa neno la shukrani, Mtumishi Mstaafu wa Ofisi
hiyo, Bw. Jerome Nchimbi amesema, ndani ya miaka 8 aliyofanya kazi katika ofisi
hiyo amejfunza masuala mengi ya Kiutumishi pamoja na kufundishwa upendo, ushirikiano
na kuwajali watu.
Kwa upande wake, Mstaafu mwingine, Bi. Godliver
Byemerwa ametoa wito kwa Watumishi wa ofisi hiyo kuendelea kuwahudumia Wananchi
kwa moyo wa upendo na ufanisi mkubwa kwa kuwa ofisi hiyo ni kioo cha jamii.
Aidha, Ofisi hiyo
imewapongeza Watumishi waliozaliwa mwezi Oktoba na kuwatakia heri katika maisha
yao ya Utumishi wa Umma ili kuwatumikia wananchi pamoja na kuongeza tija katika
utendajikazi.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa
Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, SACP. Ibrahim Mahumi (wakwanza
kulia) akitoa nasaha kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI kwa
Watumishi wa ofisi hiyo waliostaafu na Watumishi wanaoadhimisha Siku ya
Kuzaliwa katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma
Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI
wakimsikiliza Mkurugenzi
wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma wa ofisi hiyo, SACP.
Ibrahim Mahumi (hayupo pichani) wakati akitoa nasaha kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI kwa watumishi wa
ofisi hiyo waliostaafu na Watumishi wanaoadhimisha Siku ya Kuzaliwa katika
ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Sehemu ya
Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakiwasikiliza Watumishi wastaafu
Bw. Jerome Nchimbi na Bi. Godliver
Byemerwa (hawapo pichani) wa ofisi hiyo walipokuwa wakitoa
shukrani kwa Viongozi na Watumishi mara baada ya kufikia ukomo katika Utumishi
wa Umma.
Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifurahia jambo wakati Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma wa ofisi hiyo, SACP.
Ibrahim Mahumi (hayupo pichani) alipokuwa akitoa nasaha kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI kwa Watumishi wa
ofisi hiyo waliostaafu na Watumishi wanaoadhimisha Siku ya Kuzaliwa katika
ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Sehemu ya Watumishi wa Ofisi
ya Rais-UTUMISHI, waliostaafu na Watumishi wanaoadhimisha Siku ya Kuzaliwa
wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, SACP.
Ibrahim Mahumi (hayupo pichani) alipokuwa akitoa nasaha kwa niaba ya
Katibu Mkuu-UTUMISHI kwa Watumishi hao katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali
Mtumba, jijini Dodoma.
Sehemu ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma wa ofisi hiyo, SACP.
Ibrahim Mahumi (hayupo pichani) wakati akitoa nasaha kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI kwa watumishi wa ofisi hiyo
waliostaafu na Watumishi wanaoadhimisha Siku ya Kuzaliwa katika ofisi hiyo
iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Sehemu ya Wakurugenzi na
Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, wa ofisi hiyo, SACP.
Ibrahim Mahumi (hayupo pichani) wakati akitoa nasaha kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI kwa watumishi wa
ofisi hiyo waliostaafu na Watumishi wanaoadhimisha Siku ya Kuzaliwa katika
ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Mtumishi Mstaafu wa Ofisi
ya Rais-UTUMISHI, Bw. Jerome Nchimbi akitoa neno la shukrani kwa Wakurugenzi na
Watumishi wa ofisi hiyo baada ya kuhitimisha Utumishi wake wa Umma.
Sehemu ya Wakurugenzi na
Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, SACP.
Ibrahim Mahumi (hayupo pichani) wakati akitoa nasaha kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI kwa watumishi wa
ofisi hiyo waliostaafu na Watumishi wanaoadhimisha Siku ya Kuzaliwa katika
ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Sehemu ya Watumishi wa Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Mkurugenzi wa
Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma wa ofisi hiyo, SACP.
Ibrahim Mahumi (hayupo pichani) wakati akitoa nasaha kwa niaba ya
Katibu Mkuu-UTUMISHI kwa watumishi wa ofisi hiyo waliostaafu na Watumishi wanaoadhimisha
Siku ya Kuzaliwa katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini
Dodoma.
Mtumishi Mstaafu wa Ofisi
ya Rais-UTUMISHI, Bi. Godliver Byemerwa akitoa neno la shukrani kwa Wakurugenzi
na Watumishi wa ofisi hiyo baada ya kuhitimisha Utumishi wake wa Umma.
Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakimsikiliza Mkurugenzi wa
Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma wa ofisi hiyo, SACP.
Ibrahim Mahumi (hayupo pichani) wakati akitoa nasaha kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI kwa watumishi wa
ofisi hiyo waliostaafu na Watumishi wanaoadhimisha Siku ya Kuzaliwa katika
ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment