Thursday, October 2, 2025

OFISI YA RAIS YAAHIDI KUONGEZA KASI KATIKA UTOAJI WA HUDUMA KWA UMMA.

Na Eric Amani, Dodoma

Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu-Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Musa Magufuli amesisitiza kuwa ofisi hiyo itaongeza kasi zaidi ya utoaji wa huduma bora kwa umma.

Msisitizo huo ameutoa leo Oktoba 1,2025 wakati watumishi wa Idara yake walipokuwa na kazi maalumu ya kupokea wateja wa ndani na nje ya ofisi hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika katika ofisi hiyo Mtumba Jijini Dodoma.

“Sisi kama Ofisi ya Rais-UTUMISHI tunawajibika kuwa na weledi na kuzingatia uadilifu katika utoaji wa huduma kwa umma wakati wote” alisema Magufuli.

Aidha, Bw. Magufuli aliongeza kuwa ofisi hiyo itaendelea kuimarisha mifumo ya utoaji huduma, ikiwemo matumizi ya mifumo ya TEHAMA ili kuongeza uwazi, uwajibikaji na kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi.

Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja hufanyika kila mwaka duniani kote, kwa lengo la kuhimiza taasisi mbalimbali kuongeza ubunifu na ubora katika kuwahudumia wateja wao.

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Ofisi ya Rais - UTUMISHI Bw. Musa Magufuli (Wa pili kutoka Kulia) akitetea jambo na Maafisa wa Ofisi hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja Oktoba 1, 2025 Mtumba Dodoma.
Mhasibu Mkuu Ofisi ya Rais - UTUMISHI Bi. Tumwimbilege Ilomo akipokea zawadi kutoka kwa Afisa Tawala Yustina Dyabene wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja iliyofanyika katika ofisi hiyo Oktoba 1, 2025 Jijini Dodoma.


Mkurugenzi Idara ya Mikataba ya Utendaji Kazi na Serikalini Ofisi ya Rais - UTUMISHI Bi. Zainabu Kutengezah (aliyesimama katikati) akimuhudimia mtumishi wa Ofisi hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja Ocktoba 1, 2025 Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Idara ya Utawala na Usimamizi wa Raisilimali Watu Ofisi ya Rais - UTUMISHI Bw. Musa Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Afisa wa ofisi hiyo Ndg. Mohamed Suleiman wataki wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja iliyofanyika katika ofisi hiyo Oktoba 1, 2025 Jijini Dodoma.
Picha ya pamoja ya watumishi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja Oktoba 1, 2025 Mtumba Jijini Dodoma.
Afisa Rasilimali Watu Mwandamizi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi Catherine Massawe akitoa huduma kwa mmoja wa wateja waliofika katika ofisi hiyo, wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja Oktoba 1, 2025.


No comments:

Post a Comment