Na. Antonia Mbwambo na Veronica Mwafisi
Tarehe 09
Oktoba, 2025
Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi
amewakumbusha Watumishi wa Umma kupitia Vyombo mbalimbali vya Habari,
kuwajibika katika kutoa huduma Bora kwa Umma kwa kuzingatia Misingi ya Uadilifu
ili kuleta Ustawi kwa Wananchi.
Bw.
Mkomi ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu ushiriki
wa Watumishi wa Umma katika kuadhimisha Wiki ya
Huduma kwa Mteja iliyoanza tarehe 06 hadi 10, Oktoba 2025 yenye Kaulimbiu
isemayo “Dhamira Inayowezekana”.
Bw.
Mkomi amesema, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ni
simamizi katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Mteja, hivyo imeendelea kuzingatia misingi
yake ya maadili ikiwemo Uzalendo, Uadilifu, Ubora na Mteja Kwanza ikiwa ni sehemu ya
kusimamia Dira ya Ofisi inayofanya kuwa na Utumishi wa Umma wenye ufanisi na
uwajibikaji.
Vilevile
Katibu Mkuu Mkomi amewataka Watumishi wa Umma kutumia Wiki ya Huduma kwa Mteja kuwa
chachu ya mabadiliko katika utendaji kwa kutoa huduma bora na kujenga taswira
chanya kwenye ofisi kwa kuzingatia misingi ya maadili ili kupunguza malalamiko
na kujenga imani ya Wananchi kwa Serikali yao.
“Ustawi
wa Wananchi utapatikana kupitia utoaji wa huduma bora, unaozingatia maadili ya utendaji
na maadili ya taaluma walizonazo Watumishi wa Umma hivyo, wanapotoa huduma
wazingatie kuwa nadhifu, waaminifu, wakarimu, wenye heshima, wanaojali utu,
kuepuka vitendo vya rushwa na kujali watu wanaowahudumia,” Bw. Mkomi amesisitiza.
Katika
hatua nyingine alipokuwa akihitimisha hotuba yake, Katibu Mkuu Mkomi amesisitiza
Watumishi wa Umma na Wananchi kujitokeza katika Uchaguzi Mkuu wa Serikali
utakaofanyika tarehe 29 Oktoba, 2025 ili kutumia haki yao ya Kikatiba ya
kuchagua Viongozi watakaoiongoza nchi kwa ustawi wa Taifa.
Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akizungumza
wakati wa Mkutano wake na Waandishi wa Habari kuhusu ushiriki wa Watumishi wa
Umma katika kuadhimisha Wiki
ya Huduma kwa Mteja uliofanyika katika Ofisi hiyo, Jijini
Dodoma.
Sehemu
ya Wakurugenzi wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (hayupo
pichani) wakati wa Mkutano wake na Waandishi wa Habari kuhusu ushiriki wa Watumishi
wa Umma katika kuadhimisha Wiki
ya Huduma kwa Mteja uliofanyika katika Ofisi hiyo, Jijini
Dodoma.
Baadhi
ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw.
Juma Mkomi (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wake na waandishi hao kuhusu ushiriki
wa Watumishi wa Umma katika kuadhimisha Wiki ya
Huduma kwa Mteja katika Utumishi wa Umma uliofanyika jijini Dodoma.
Sehemu
ya Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (hayupo
pichani) wakati wa Mkutano wake na Waandishi wa Habari kuhusu ushiriki wa Watumishi
wa Umma katika kuadhimisha Wiki
ya Huduma kwa Mteja uliofanyika katika Ofisi hiyo, Jijini
Dodoma.
Mwandishi
wa Habari kutoka Gazeti la Mwananchi, Bw. Abel Chidawali (aliyesimama) akiuliza
swali kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi wakati wa Mkutano
wa Katibu Mkuu huyo na Waandishi wa Habari kuhusu ushiriki wa Watumishi wa Umma
katika kuadhimisha Wiki
ya Huduma kwa Mteja uliofanyika katika hiyo, Jijini Dodoma.
Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (meza kuu)
akizungumza wakati wa Mkutano wake na Waandishi wa Habari kuhusu ushiriki wa Watumishi
wa Umma katika kuadhimisha Wiki
ya Huduma kwa Mteja uliofanyika katika Ofisi hiyo, Jijini
Dodoma.
Waandishi
wa Habari wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma (katikati) mara baada ya Katibu Mkuu huyo
kuhitimisha Mkutano wake na Waandishi hao kuhusu ushiriki wa Watumishi wa Umma

No comments:
Post a Comment