Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa ofisi hiyo, Bibi Hilda
Kabissa amepongeza Taasisi Simamizi za Maadili ya Utendaji na
Mamlaka Simamizi za Maadili ya Kitaaluma kwa kuendelea kusimamia tabia na
mienendo ya kimaadili ya watumishi wanaowasimamia.
“Ninawapa pongezi kwa kuwa mmetoa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi
wenu mahala pa kazi ili waweze kuzingatia maadili katika utoaji wa huduma kwa
umma” alisema Bibi Hilda.
Bibi. Kabissa ametoa pongezi hizo wakati akifungua kikao kazi cha sita (6) cha kubadilishana uzoefu na taarifa baina ya Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Taasisi Simamizi za
Maadili ya Utendaji na Mamlaka Simamizi za Maadili ya Kitaaluma kilichofanyika
katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira jijini Dodoma.
Bibi. Kabisa
aliongeza kuwa pongezi hizo anazowapa viongozi
wa taasisi hizo ziwe chachu ya kuongeza ubunifu zaidi na kuweka mikakati
endelevu ya kuboresha misingi ya maadili ya utendaji na maadili ya kitaaluma,
ili kuimarisha utendaji kazi Serikalini”.
Vilevile, alibainisha kuwa kazi ya kusimamia maadili ya watumishi wa
umma si rahisi lakini kwa kuwa taasisi hizo ziliwajengea uwezo watumishi wao, imekuwa
kazi rahisi kwao kusimamia maadili kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na
Miongozo hivyo kupunguza vitendo vya rushwa kwa watumishi wa umma katika utoaji
wa huduma.
Kadhalika, Bibi.
Kabissa amewataka washiriki wa kikao kazi
hicho kuboresha mbinu mbalimbali za usimamizi na utatuzi wa changamoto wanazokutana
nazo katika usimamizi wa maadili kwa watumishi wa umma ili kuleta ustawi wa
wananchi.
Kwa upande
wake, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Felister
Shuli akitoa maelezo ya awali amesema, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma ina jukumu la kusimamia maadili ya utendaji katika Utumishi wa Umma,
ambapo njia mojawapo ya utekelezaji wa jukumu hilo ni kushirikiana na wadau
mbalimbali wanaohusika na usimamizi wa maadili zikiwemo Taasisi Simamizi za
Maadili ya Utendaji pamoja na Mamlaka Simamizi za Maadili ya Kitaaluma.
Mkurugenzi
Shuli amesema, katika kikao kazi hicho wanatarajia kufundishwa mada tano (5)
zitakazoakisi Usimamizi wa Maadili ya Utendaji, na Maadili ya Kitaaluma katika
Utumishi wa Umma.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Ofisi ya Rais–UTUMISHI na Utawala Bora, Bibi. Hilda Kabissa, akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha kubadilishana uzoefu na taarifa baina ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Taasisi Simamizi za Maadili ya Utendaji na Mamlaka Simamizi za Maadili ya Kitaaluma kilichofanyika katika Ukumbi wa Sekretarieti ya Ajira, jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wa kikao kazi cha kubadilishana uzoefu na taarifa baina ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Taasisi Simamizi za Maadili ya Utendaji na Mamlaka Simamizi za Maadili ya Kitaaluma wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Ofisi ya Rais–UTUMISHI, Bibi. Hilda Kabissa (hayupo pichani) wakati akifungua kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Sekretarieti ya Ajira, jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bi. Felister Shuli akijibu baadhi ya hoja
zilizowasilishwa na washiriki wa kikao kazi cha kubadilishana
uzoefu na taarifa baina ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Taasisi Simamizi za Maadili ya Utendaji na Mamlaka Simamizi za
Maadili ya Kitaaluma kilichofanyika katika Ukumbi wa Sekretarieti ya Ajira,
jijini Dodoma.
Katibu Msaidizi, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi
wa Umma, Bw. Salvatory Kilasara akiwasilisha mada kuhusu Misingi ya Maadili ya
Viongozi wakati wa kikao kazi cha kubadilishana uzoefu na taarifa baina ya Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Taasisi Simamizi za
Maadili ya Utendaji na Mamlaka Simamizi za Maadili ya Kitaaluma kilichofanyika
katika Ukumbi wa Sekretarieti ya Ajira, jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wa kikao kazi cha kubadilishana uzoefu na taarifa baina ya Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Taasisi Simamizi za
Maadili ya Utendaji na Mamlaka Simamizi za Maadili ya Kitaaluma wakifuatilia
mada mbalimbali wakati wa kikao
hicho kilichofanyika
katika Ukumbi wa Sekretarieti ya Ajira, jijini Dodoma.
Mbunifu Majengo, Bw.
Joseph Ringo (aliyesimama) akiwasilisha maoni yake wakati wa kikao kazi
kilicholenga kubadilishana
uzoefu na taarifa baina ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Taasisi Simamizi za Maadili ya Utendaji na Mamlaka Simamizi za
Maadili ya Kitaaluma kilichofanyika katika Ukumbi wa Sekretarieti ya Ajira,
jijini Dodoma.
Afisa Habari Mkuu,
Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Rocky Setembo akitoa utambulisho wa washiriki
wa kikao kazi cha kubadilishana
uzoefu na taarifa baina ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Taasisi Simamizi za Maadili ya Utendaji na Mamlaka Simamizi za
Maadili ya Kitaaluma kilichofanyika katika Ukumbi wa Sekretarieti ya Ajira,
jijini Dodoma.
Mkurugenzi Kitengo cha Udhibiti wa Ndani-TAKUKURU,
Bi. Leonalda Ngaiza (aliyesimama) akisisitiza jambo wakati akitoa maoni kwenye
kikao kazi cha kubadilishana
uzoefu na taarifa baina ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Taasisi Simamizi za Maadili ya Utendaji na Mamlaka Simamizi za
Maadili ya Kitaaluma kilichofanyika katika Ukumbi wa Sekretarieti ya Ajira,
jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Ukuzaji wa Maadili, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Ally Ngowo akitoa maelezo ya utangulizi na
kuwakaribisha washiriki wa kikao kazi cha kubadilishana uzoefu na taarifa baina ya Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Taasisi Simamizi za
Maadili ya Utendaji na Mamlaka Simamizi za Maadili ya Kitaaluma kilichofanyika
katika Ukumbi wa Sekretarieti ya Ajira, jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Ofisi ya
Rais–UTUMISHI, Bibi. Hilda Kabissa (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya
pamoja mara baada ya kufungua kikao kazi cha kubadilishana uzoefu na taarifa baina ya Ofisi ya

No comments:
Post a Comment