Na. Antonia Mbwambo
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya
Rais - UTUMISHI SACP. Ibrahim Mahumi amesema Serikali imeamua kufanya mapitio
na maboresho makubwa ya kanuni za kudumu katika Utumishi wa Umma kutokana na
mabadiliko na ukuaji wa sanyansi na teknolojia ambayo imeathiri eneo la Utawala
na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma.
SACP. Mahumi
alisema
hayo Oktoba 2, 2025 katika ukumbi wa Halmashauri ya Jijini Dodoma wakati wa kufungua
kikao kazi cha Wadau cha kuhakiki rasimu ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma Toleo la Nne la mwaka
2025. Kikao kazi hicho kilihusisha Wakurugenzi na Mameneja wa Utawala na
Usimamizi wa Rasilimaliwatu kutoka katika taasisi mbalimbali za umma.
“Mwitiko huu ni ishara tosha
kuwa maoni thabiti yatapatikana kwa kuzingatia kuwa ninyi ndio mnaopata changamoto
wakati wa utekelezaji wa kanuni hizi, hivyo maoni yenu kama wadau ni muhimu
katika kuboresha Kanuni hizi za kudumu katika Utumishi wa Umma” alisema
SACP. Mahumi.
SACP.
Mahumi alisema kuwa kwa sasa kuna sheria nyingi zinazosimamia
maeneo ya Utumishi wa Umma ikiwemo Sheria ya Utumishi wa Umma, Sheria ya
Mahusiano Kazini, Sheria za hifadhi ya jamii hivyo mawazo yenu yanatakiwa
kuleta muunganiko mzuri kati ya Sera, Sheria
na Kanuni za kudumu katika Utumishi wa Umma.
Aidha SACP. Mahumi alisisitiza
wadau hao kutoa maoni kwa kuzingatia Dira ya Taifa ya 2050 ili kuwa na
muunganiko wa kanuni hizo na kuleta urahisi kwa watumishi wa umma hasa pale
wanapofanya marejeo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Cyrus Kapinga amehitimisha mjadala
huo kwa kuwashukuru washiriki wa kikao hicho kwa mawazo waliyotoa na kuahidi
kuwa yote yaliyojadiliwa yamepokelewa na yatafanyiwa kazi.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala
wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, na Utawala
Bora SACP. Ibrahim Mahumi akitoa hotuba ya ufunguzi wa kikao
kazi cha Wadau cha kuhakiki Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma Toleo la
Nne la mwaka 2025 kilichofanyika
katika ukumbi wa Halmashauri ya Jijini Dodoma .
Wakurugenzi
na Mameneja kutoka Taasisi mbalimbali za Umma wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi (hayupo
pichani), iliyolenga kufungua kikao
kazi cha Wadau cha kuhakiki Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma Toleo la Nne la mwaka
2025 Jijini Dodoma .
Mkurugenzi wa Kitengo cha
Huduma za Sheria,Ofisi ya Rais – UTUMISHI,Bi Hilda
Kabissa akiwasihi wadau wa rasimu ya kanuni za kudumu katika Utumishi wa Umma
kutoa maoni yatakayosaidia kuboresha rasimu ya kanuni hizo kwa manufaa ya Taifa.
Mkurugenzi wa Idara ya
Uendelezaji Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais – UTUMISHI, Bi Leila Mavika (aliyesimama)
akifafanua jambo kuhusu rasimu ya kanuni za kudumu
katika Utumishi wa Umma katika kikao kazi cha kuhakiki rasimu ya Kanuni hizo
jijini Dodoma.
Mkurugenzi
wa Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Cyrus Kapinga
akitoa maneno ya shukrani kwa wadau mbalimbali wa kikao kazi cha kuhakiki rasimu
ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa
Umma Toleo la Nne la mwaka 2025 kwa ushiriki wao alipokuwa akihitimisha kikao
kazi hicho ambacho kilicholenga kupata maoni ya kuboresha kanuni hizo,
Mwenyekiti wa kikao cha wadau
wa kuhakiki rasimu ya kanuni za kudumu katika utumishi wa Umma ambaye ni
Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi Makumbusho ya Taifa, Bw. Zakariyya Kera (aliyesimama),
akitoa ufafanuzi wa jambo alipokuwa akipokea maoni ya maboresho ya kanuni hizo
kutoka kwa washiriki wa kikao hicho (hawapo pichani) mnamo tarehe 2,
oktoba,2025 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki ambao ni
Wakurugenzi wa Rasilimaliwatu wakiunga mkono hoja mbalimbali zilizokuwa
zikitolewa na wadau wa kuhakiki rasimu ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma Toleo la Nne la mwaka
2025 (hawapo pichani) kilichofanyika tarehe 2,oktoba,2025 katika ukumbi wa
Halmashauri ya Jijini Dodoma .
Mwakilishi wa Meneja sehemu ya
Utawala Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Bi Hawa Goronya akitoa
maoni juu ya maboresho ya Kanuni za kudumu za Utumishi wa Umma katika kikao kazi
cha Wadau cha kuhakiki Kanuni hizoToleo la Nne la mwaka 2025 kilichofanyika
oktoba 2,2025 jijini Dodoma.
Mchumi Mwandamizi, Bw. Mwendesha Makelemelo kutoka Ofisi ya Rais – UTUMISHI,akitoa wasilisho la maboresho ya Kanuni za kudumu katika Utumishi wa Umma kwenye kikao kazi cha wadau (hawapo pichani) kilichofanyika oktoba 2,2025 katika ukumbi wa Halmashauri ya jiji uliopo Mtumba Dodoma.


No comments:
Post a Comment