Na. Antonia Mbwambo na Veronica Mwafisi -Dodoma
Tarehe 29 Oktoba, 2025
Watendaji Wakuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora leo tarehe 29.10.2025 wameshiriki zoezi la kupiga kura katika
Vituo mbalimbali na kuchagua Viongozi katika ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani.
Akishiriki zoezi hilo katika Kituo cha Kupiga Kura cha Msangalale
Mashariki, Kata ya Dodoma Makulu, jijini Dodoma, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi ametoa wito kwa Watumishi wa
Umma na Wananchi kujitokeza kuchagua viongozi wanaowahitaji kwa maendeleo ya Taifa.
“Namshukuru Mungu nimeshikiri salama zoezi hili muhimu la Kikatiba, nipende
kutoa wito kwa Watumishi wa Umma na Wananchi kwa ujumla kushikiriki pia kwani
ni haki yao ya msingi.” Bw. Mkomi amesisitiza.
Amesema hali katika Kituo hicho ni ya utulivu na wananchi wamekua
wakimiminika kwenda kupiga kura hivyo amewasisitiza kila mwenye haki ya
kushiriki zoezi hilo afanye hivyo.
Aidha, Bw. Mkomi amewapongeza Waratibu wa zoezi hilo katika Kituo hicho
kwa kuonyesha ushirikiano kwa wananchi wanaoenda kushiriki katika zoezi hilo na
kuhakikisha kila mwenye sifa anashiriki kikamilifu.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bw. Xavier Daudi
ameshiriki zoezi hili muhimu katika Kituo cha Mwatano, Kata ya Miyuji, Jijini
Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akiweka
fomu ya kupiga Kura katika sanduku la Kura mara baada ya kushiriki zoezi hilo
la Uchaguzi Mkuu wa Viongozi
katika ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani leo tarehe 29 Oktoba, 2025 katika Kata ya Dodoma
Makulu, Mtaa wa Msangalale jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi akiweka fomu ya kupiga Kura katika sanduku la Kura
mara baada ya kushiriki zoezi hilo la Uchaguzi Mkuu wa Viongozi katika ngazi ya
Rais, Wabunge na Madiwani leo tarehe 29 Oktoba, 2025 katika Kata ya Miyuji, Mtaa
wa Mwatano jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (aliyesimama) akipokea fomu ya kushiriki
kupiga Kura kutoka kwa Wasimamizi wa Uchaguzi katika zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Viongozi katika ngazi ya Rais, Wabunge na
Madiwani leo tarehe 29 Oktoba,
2025 katika Kata ya Dodoma Makulu, Mtaa wa Msangalale jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi (aliyesimama) akisubiri kupatiwa fomu ya kushiriki kupiga Kura kutoka kwa Wasimamizi wa Uchaguzi katika zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Viongozi katika ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani leo tarehe 29 Oktoba, 2025 katika Kata ya Miyuji, Mtaa wa Mwatano jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akionesha jina lake katika orodha ya wapiga Kura iliyobandikwa katika
kituo hicho kabla ya kushiriki kupiga kura katika zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Viongozi katika ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani leo tarehe 29 Oktoba, 2025 katika Kata ya Dodoma Makulu, Mtaa wa Msangalale
jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi akishiriki kupiga Kura katika zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Viongozi katika ngazi
ya Rais, Wabunge na Madiwani leo tarehe 29 Oktoba, 2025 katika Kata ya Miyuji, Mtaa
wa Mwatano jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akionesha kadi yake ya kupiga Kura kabla
ya kushiriki zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Viongozi katika ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani leo tarehe 29 Oktoba, 2025 katika
Kata ya Dodoma Makulu, Mtaa wa Msangalale jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi akihakiki jina na picha yake kwenye daftari la kudumu
kabla ya kushiriki zoezi la kupiga Kura katika Uchaguzi Mkuu wa Viongozi katika ngazi ya
Rais, Wabunge na Madiwani leo tarehe 29 Oktoba, 2025 katika Kata ya Miyuji, Mtaa
wa Mwatano jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akipakwa wino mara baada ya
kushiriki kupiga Kura katika zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Viongozi kwenye ngazi ya Rais, Wabunge na
Madiwani leo tarehe 29 Oktoba,
2025 katika Kata ya Dodoma Makulu, Mtaa wa Msangalale jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi (wa kwanza kushoto) akipokea fomu ya
kushiriki kupiga Kura kutoka kwa Wasimamizi wa Uchaguzi katika zoezi la
Uchaguzi Mkuu wa Viongozi katika ngazi
ya Rais, Wabunge na Madiwani leo tarehe 29 Oktoba, 2025 katika Kata ya Miyuji, Mtaa wa Mwatano jijini
Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi akionesha
kidole kilichopakwa wino mara baada ya kushiriki kupiga Kura katika zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Viongozi kwenye ngazi ya Rais, Wabunge na
Madiwani leo tarehe 29 Oktoba,
2025 katika Kata ya Miyuji, Mtaa wa Mwatano jijini Dodoma.






No comments:
Post a Comment