Na Eric Amani, Mtumba Dodoma
Tarehe 11.10.2025
Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kipindi cha mwaka wa fedha 2024/25 na
2025/26, imetoa vibali vya ajira 86,500 ili kuhakikisha Wizara, Idara, Taasisi
za Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa zinakuwa na
watumishi wa kutosha kutekeleza majukumu yake ya kuwahudumia wananchi
kikamilifu.
Akizungumza
na Vyombo vya Habari leo Oktoba 11, 2025 jijini Dodoma, Katibu Mkuu Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi amesema ajira
hizo zinahusu kada mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya, Kilimo, UhandisI na sekta
nyingine.
Katibu
Mkuu Mkomi amefafanua kuwa katika mwaka wa fedha 2024/25 Serikali ilitoa kibali
cha nafasi 45,000 za ajira mpya kwa Taasisi mbalimbali na utekelezaji wake
ulianza tarehe 29 Aprili, 2025 na kufuatia kutolewa kwa kibali hicho, mchakato
wa kujaza nafasi hizo umefanyika na hadi sasa nafasi 30,863 zimejazwa na
wahusika wamepangiwa vituo vya kazi. Aidha, nafasi 6,701 usaili umefanyika na
wahusika watapangwa vituo vya kazi ndani ya Mwezi Oktoba, 2025 na nafasi 7,436
ujazaji wake utakamilika Mwezi Novemba, 2025 na wasailiwa kupangwa vituo vya
kazi mwezi huo huo.
Ameongeza
kuwa katika mwaka wa fedha 2025/26, Serikali iliidhinisha nafasi 41,500 za
ajira mpya kwa Taasisi mbalimbali zikiwemo nafasi 12,176 za Walimu na nafasi
10,280 za kada za Afya ambapo utekelezaji wake unaanza mara moja.
Kufuatia
kutolewa kwa vibali hivyo, Katibu Mkuu Mkomi ameielekeza Sekretarieti ya Ajira
katika Utumishi wa Umma kuanza mchakato wa kujaza nafasi hizo za mwaka 2025/26
pamoja na kukamilisha mchakato wa nafasi zote za Mwaka 2024/25.
Vile
vile Bw. Mkomi ametoa maelekezo kwa waajiri wote kutoa ushirikiano kwa
Sekretarieti ya Ajira ili kuhakikisha lengo la ujazwaji wa nafasi za ajira
linatimia.
“Ili
kuhakikisha Sekretarieti ya Ajira inatekeleza jukumu hili ipasavyo,
ninawaelekeza Waajiri kutoa ushirikiano. Aidha, ninawaelekeza Waajiri ambao
Sekretarieti ya Ajira imekasimu madaraka ya uendeshaji wa mchakato wa ajira kwa
baadhi ya kada, kuhakikisha wanaendesha usaili huu mara moja ili kujaza nafasi
walizoidhinishiwa kwa kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni za uendeshaji wa
usaili katika Utumishi wa Umma,” Katibu Mkuu Mkomi amesisitiza.
Katika
kuhakikisha gharama za kufanya usaili zinapungua na unafanyika kwa wakati, Bw.
Mkomi ameielekeza Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kuwa zoezi la
usaili lifanyike kila Mkoa Tanzania Bara na vituo vilivyoandaliwa mahsusi wa
upande wa Zanzibar ili kutoa fursa kwa waombaji kutoka katika maeneo husika
kuomba na hatimaye kusailiwa
Pia
amesema waombaji watakaofaulu usaili lakini wakashindwa kupangiwa kazi baada ya
usaili wawekwe katika kanzidata na waendelee kupangiwa kazi kwa kadri nafasi za
ajira mpya zitakapokuwa zinapatikana.
Amesema
waombaji hao watapangiwa kazi katika Taasisi zitakazokuwa na nafasi popote hapa
nchini na kuongeza kuwa barua za kupangiwa vituo vya kazi kwa wasailiwa
watakaofualu usaili zipatikane katika “Mfumo wa Ajira Portal” kupitia akaunti
za wahusika.
Katibu Mkuu Mkomi ameongeza kuwa, Serikali itaendelea kutoa vibali vya ajira kulingana na mahitaji ya sekta mbalimbali ili kuhakikisha huduma bora kwa wananchi zinapatikana.
Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akizungumza
wakati wa Mkutano wake na Waandishi wa Habari kuhusu utoaji wa Vibali vya Ajira
kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 na Mwaka 2025/26 uliofanyika katika Ofisi hiyo,
Jijini Dodoma.
Sehemu
ya Wakurugenzi wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wake na Waandishi
wa Habari kuhusu utoaji wa Vibali vya Ajira kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 na Mwaka
2025/26 uliofanyika katika Ofisi hiyo, Jijini Dodoma.
Baadhi
ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw.
Juma Mkomi (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wake na waandishi hao kuhusu utoaji
wa Vibali vya Ajira kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 na Mwaka 2025/26 uliofanyika
jijini Dodoma. Wengine ni Wakurugenzi wa Idara na Vitengo wa Ofisi hiyo.
Sehemu
ya Wakurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wake na
Waandishi wa Habari kuhusu utoaji wa Vibali vya Ajira kwa Mwaka wa Fedha
2024/25 na Mwaka 2025/26 uliofanyika katika Ofisi hiyo, Jijini Dodoma.
Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (meza kuu)
akizungumza wakati wa Mkutano wake na Waandishi wa Habari kuhusu utoaji wa Vibali
vya Ajira kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 na Mwaka 2025/26 uliofanyika katika Ofisi
hiyo, Jijini Dodoma. Wengine ni Sehemu ya Wakurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi
kutoka Ofisi hiyo.
Baadhi
ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw.
Juma Mkomi (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wake na waandishi hao kuhusu utoaji
wa Vibali vya Ajira kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 na Mwaka 2025/26 uliofanyika
jijini Dodoma. Wengine ni Wakurugenzi wa Idara na Vitengo wa Ofisi hiyo.






No comments:
Post a Comment