Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene leo amemtembelea na kufanya
mazungumzo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya M. Kikwete nyumbani
kwake Kawe Jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hayo, Mhe. Simbachawene amefikisha
salaam za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
ambaye ameahidi kuendelea kuwa pamoja na Viongozi Wakuu Wastaafu wa Kitaifa kwa
maendeleo ya taifa.
Mhe. Simbachawene amesema Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ina jukumu la kutunza Viongozi Wakuu Wastaafu
Kitaifa na Wenza wao, hivyo yuko tayari kuendelea kutekeleza jukumu hilo
alilopewa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ufanisi.
Hali kadhalika, Mhe. Dkt. Kikwete amemshukuru Mhe.
Simbachawene kwa ujio huo na kupongeza utaratibu uliopo wa kuwatembelea Wiongozi
Wakuu Wastaafu wa Kitaifa kwa kuwa unawapa faraja, unaonesha thamani na mchango
wao kwa maendeleo ya taifa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiteta na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete nyumbani kwake Kawe Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment