Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Tarehe 23.09.2024
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi amewataka Wasimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini kuacha kuwa sababu ya Magonjwa Sugu Yasiyoambukizwa (MSY) kwa watumishi wa umma na kushindwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu.
Bw. Mkomi ameyasema hayo leo wakati akifungua semina elekezi ya siku moja kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kutoka mikoa 26 ya Tanzania Bara kuhusu Mwongozo wa Kudhibiti VVU, UKIMWI na Magonjwa Sugu Yasiyoambukizwa mahali pa kazi katika Utumishi wa Umma iliyofanyika katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.
Amesema baadhi ya Wasimamizi wa Rasilimaliwatu wamekuwa miungu watu na wababe kiasi cha kutowatendea haki watumishi katika masuala yao ya kiutumishi na kuchangia watumishi hao kupata Magonjwa Sugu Yasiyoambukizwa.
“Changamoto nyingine za Magonjwa Sugu Yasiyoambukizwa kwa Watumishi wa Umma yamekuwa yakisababishwa na baadhi yenu kwa kutowajibika kwa watumishi mnaowaongoza kwani mmekuwa wababe na kuogopwa sana, jambo hili sio sawa kwani kuwajibika kwa watumishi ni wajibu wenu.” Katibu Mkuu Mkomi amesisitiza.
Ameongeza kuwa, watumishi hawa ndio wanaosaidia katika kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo, hivyo ni lazima wasikilizwe, wasaidiwe na kutatua changamoto zao badala ya kuwa wababe kwani kwa kufanya hivyo watashindwa kufanya kazi kikamilifu na kurudisha nyuma mipango ya maendeleo.
“Tunapaswa kuwajibika kwa tunaowasimamia, tuwasimamie kwa karibu kama tumeshindwa kufanya hivyo basi tumeshindwa kazi” Ameongeza Bw. Mkomi.
Amesema Wasimamizi wa Rasilimaliwatu kuwa karibu na watumishi wanaowaongoza kunasaidia hata watumishi hao kuwashirikisha changamoto zinazowakabili hata zile za kiafya ili wasaidiwe na kuweza kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Katika hatua nyingine Katibu Mkuu Mkomi amewataka Makatibu Tawala Wasaidizi hao kuwahamasisha Watumishi wa Umma kujitokeza kupiga kura ili kuchagua viongozi watakaosimamia utekelezaji wa mipango mbalimbali ya serikali kwenye mitaa yao.
“Twendeni tukahamasishe watumishi wa umma, sisi ndio tunaowasimamia, wakajitokeze katika kupiga kura, tukiwaacha wafanye kazi zao bila kuwahamasisha wanaweza wakachangia kutokapatikana kwa viongozi walio bora,” Katibu Mkuu Mkomi amesisitiza.
Naye Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bi. Beatrice Kimoleta amesema Serikali imekuwa ikitekeleza miradi mingi ya maendeleo hivyo, ni muhimu rasilimaliwatu ikasimamiwa kwa usahihi ili iweze kutekeleza miradi hiyo kwa ufasaha.
“Semina hii ni muhimu kwani itasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuhakikisha rasilimaliwatu katika Serikali za Mitaa inakuwa yenye afya na yenye kuleta tija.” Bi. Kimoleta ameongeza.
Akitoa neno la Utangulizi kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu kufungua semina hiyo, Mkurugenzi wa Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Cyrus Kapinga amesema lengo la semina hiyo ni kupata ufahamu wa pamoja katika eneo la anuai za jamii na miongozo yote inayohusiana na eneo hilo.
Bw. Kapinga amesema changamoto za masuala ya anuai za jamii ni nyingi
hivyo ni lazima kukaa kwa pamoja ili kupeana ufahamu kwa lengo la kuwasaidia
watumishi wa umma kwa maendeleo ya taifa.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akizungumza na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wakati akifungua semina elekezi kuhusu Mwongozo wa Kudhibiti VVU, UKIMWI na Magonjwa Sugu Yasiyoambukizwa mahali pa kazi katika Utumishi wa Umma.
Sehemu ya Makatibu Tawala Wasaidizi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kutoka mikoa 26 ya Tanzania Bara wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi wakati akifungua semina elekezi kuhusu Mwongozo wa Kudhibiti VVU, UKIMWI na Magonjwa Sugu Yasiyoambukizwa mahali pa kazi iliyofanyika jijini Dodoma
Mkurugenzi wa
Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Cyrus Kapinga akizungumza wakati wa semina elekezi kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa
Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kuhusu Mwongozo wa Kudhibiti VVU, UKIMWI
na Magonjwa Sugu Yasiyoambukizwa mahali pa kazi iliyofanyika jijini Dodoma.
Kulia kwake ni Mkurugenzi Msaidizi Anuai za Jamii na Mratibu wa VVU,
Ukimwi na Magonjwa Yasiyoambukiza, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Mwanaamani Mtoo.
Wakurugenzi wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI
wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi wakati akizungumza na
Makatibu Tawala Wasaidizi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wakati
akifungua semina elekezi kuhusu Mwongozo wa Kudhibiti VVU, UKIMWI na Magonjwa
Sugu Yasiyoambukizwa mahali pa kazi.
Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bi. Beatrice Kimoleta akizungumza wakati wa semina elekezi kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kuhusu Mwongozo wa Kudhibiti VVU, UKIMWI na Magonjwa Sugu Yasiyoambukizwa mahali pa kazi iliyofanyika jijini Dodoma
Wakurugenzi wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI
wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma, Bw. Juma Mkomi wakati akizungumza na Makatibu Tawala Wasaidizi wa
Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wakati wa semina elekezi kuhusu Mwongozo
wa Kudhibiti VVU, UKIMWI na Magonjwa Sugu Yasiyoambukizwa mahali pa kazi.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wasaidizi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI mara baada ya kufungua semina elekezi kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu (hawapo pichani) kuhusu Mwongozo wa Kudhibiti VVU, UKIMWI na Magonjwa Sugu Yasiyoambukizwa mahali pa kazi katika Utumishi wa Umma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kutoka mikoa 26 ya Tanzania Bara mara baada ya kufungua semina elekezi kuhusu Mwongozo wa Kudhibiti VVU, UKIMWI na Magonjwa Sugu Yasiyoambukizwa mahali pa kazi katika Utumishi wa Umma.
Afisa Maendeleo ya Jamii, Ofisi ya Rais-UTUMISHI
Bi. Neema Range akiwasilisha mada wakati wa semina elekezi kuhusu Mwongozo wa
VVU, UKIMWI na Magonjwa Sugu
Yasiyoambukizwa (MSY) kwa Makatibu
Tawala Wasaidizi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kutoka mikoa 26 ya
Tanzania Bara.
Katibu Tawala Msaidizi, Utawala na Usimamizi wa
Rasilimaliwatu-Mkoa wa Singida, Bw. Stephen Pancras (wa kwanza kushoto)
akichangia mada wakati wa semina elekezi
kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Utawala na Usimamizi wa
Rasilimaliwatu kuhusu Mwongozo wa
Kudhibiti VVU, UKIMWI na Magonjwa Sugu Yasiyoambukizwa mahali pa kazi. Kushoto
kwake ni Wawezeshaji wa semina hiyo.
Wakurugenzi wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi wakati akizungumza na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wakati akifungua semina elekezi kuhusu Mwongozo wa Kudhibiti VVU, UKIMWI na Magonjwa Sugu Yasiyoambukizwa mahali pa kazi.
Sehemu ya Makatibu Tawala Wasaidizi wa Utawala na
Usimamizi wa Rasilimaliwatu kutoka mikoa 26 ya Tanzania Bara wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma
Mkomi wakati akifungua semina elekezi kuhusu
Mwongozo wa Kudhibiti VVU, UKIMWI na Magonjwa Sugu Yasiyoambukizwa mahali pa
kazi iliyofanyika jijini Dodoma
No comments:
Post a Comment