Na. Mwandishi Wetu
Septemba 5, 2024
“Nimekuja kujifunza na kuhimiza masuala ya uadilifu, uzalendo
na namna bora ya kutoa huduma kwa umma, kwa kuwa watumishi wa mamlaka hii wanawajibu
wa kusanifu, kujenga na kusimamia mifumo ya TEHAMA Serikalini ili Serikali iweze kutoa huduma kwa umma kwa
urahisi, haraka na gharama nafuu”.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu Septemba 5, 2024 jijini Dodoma
wakati alipotembelea ofisi za Mamlaka ya
Serikali Mtandao (eGA) lengo la kujifunza namna taasisi hiyo inavyofanya
kazi na kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao.
Mhe. Sangu alieleza kuwa Mamlaka ya Serikali ni muhimu sana kwa ustawi
wa taifa, hivyo watumishi wake hawanabudi kuzingatia misingi ya uadilifu na
uzalendo kwa kuwa taarifa nyingi za Serikali zinapita katika mifumo waliyoijenga
na wanayoisimamia.
Aidha, aliongeza kwa kutoa pongezi kwa watumishi wa eGA kwa kuifanya Serikali
kuwa ya kidijitali na kurahisisha utoaji wa huduma kwa umma, mathalani mifumo
iliyosanifiwa na kujengwa na eGA imeondoa upendeleo katika ajira za Serikali,
wananchi wanaweza kulipia na kupata huduma mbalimbali wakiwa mahali popote na
kwa wakati wowote.
Pia, alisisitiza watumishi wa
Mamlaka hiyo kuendelea kuhimiza taasisi za umma
kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya Serikali Mtandao katika
utekelezaji wa jitihada za Serikali Mtandao kwa lengo la kuimarisha usalama wa
mifumo ya Serikali na ya sekta binafsi iliyounganishwa na Serikali.
Awali, Katibu Mkuu-IKULU Bw. Mululi Majula Mahendeka alisema kuwa
watumishi wa eGA wanatakiwa kufanyakazi kwa weledi na uadilifu ili kuifanya
mifumo ya Serikali kuwa imara na inayoaminika kwa wananchi.
Vilevile, Mkurugenzi Mkuu wa eGA Eng. Benedict Ndomba alisema kuwa pamoja
na mambo mengine mamlaka imeshirikiana na taasisi husika kujenga Mfumo wa
kielektroni wa Usimamizi wa Vyama vya Ushiriki (MUVU) ambao unarahisisha
ukaguzi, usimamizi na uendeshaji wa Vyama vya Ushirika ili kuboresha utendajikazi,
kuchochea mabadiliko ya kiuchumi na kuongeza uwazi na uwajibikaji.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus
Sangu akizungumza
na Watumishi wa Mamlaka
ya Serikali Mtandao (eGA) wakati wa ziara
yake ya kikazi iliyofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya Watumishi wa Mamlaka ya Serikali
Mtandao (eGA) wakimsikiliza
Naibu
Waziri, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi jijini Dodoma.
Katibu Mkuu-IKULU, Bw. Mululi Majula
Mahendeka akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu kuzungumza na Watumishi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyofanyika jijini
Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), Mhandisi Benedict
Ndomba akielezea mafanikio
na utekelezaji wa
majukumu ya ofisi hiyo
kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu (hayupo
pichani) wakati
wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo
iliyofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya Watumishi wa Mamlaka ya Serikali
Mtandao (eGA)
wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Deus Sangu (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi.
Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akisalimiana na baadhi ya Viongozi na Watumishi wa Mamlaka
ya Serikali Mtandao (eGA) wakati alipowasili katika ofisi hiyo kwa ziara ya kikazi jijini
Dodoma.
No comments:
Post a Comment