Monday, September 30, 2024

KUFUATIA KASI YA UJENZI WA MIRADI YA MAENDELEO NCHINI SERIKALI KUENDELEA KUTOA VIBALI VYA AJIRA ILI KUONDOKANA NA ADHA YA UHABA WA WATUMISHI-Mhe. Simbachawene

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amesema Serikali imeendelea kutoa vibali vya ajira ili kuondokana na adha ya uhaba wa watumishi kufuatia kasi ya ujenzi wa miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali nchini ikiwemo ya afya na elimu.

Mhe. Simbachawene amesema hayo leo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kusikiliza changamoto za wananchi katika Mkoa wa Mara ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.

“Katika sekta ya afya, mchakato wa ajira umefanyika kwenye mikoa yote, waombaji wameomba na katika Mkoa wa Mara kama ilivyo katika mikoa mingine, Katibu Tawala wa Mkoa na wasaidizi wake wamesimamia zoezi hilo na watumishi hao wamepatikana hivyo, wanakuja wa kutosha, Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemaliza kazi yake,” Mhe. Simbachawene ameongeza.

Ameongeza kuwa, katika sekta ya elimu kama ilivyokuwa kwenye afya, mchakato wa ajira utaanza tena ambapo waombaji wataomba tena kupitia kwenye mikoa na huko ndiko watawapangia wenyewe sehemu yenye upungufu na sio tena Ofisi ya Rais-UTUMISHI au Ofisi ya Rais-TAMISEMI kama ilivyokuwa awali.

Mhe. Simbachawene amewasisitiza Viongozi wa mkoa huo kutoa taarifa za upungufu wa watumishi kwa kuwa mahitaji ya watumishi yanapangwa kutokana na maombi ya mkoa husika.

“Katibu Tawala wa Mkoa, kwenye upungufu wa watumishi tusaidiane kupeana taarifa na kwa wale ambao hawatapatikana kupitia mchakato wa ajira mpya katika mkoa wenu, basi tutafanya uhamisho kwasababu kasi ya maendeleo ni kubwa sana hivyo suala la upungufu wa watumishi ni lazima lipewe kipaumbele.

Aidha, Mhe. Simbachawene ametoa wito kwa watumishi wa umma kuhakikisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi unakuwa ndio kipaumbele.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya Musoma mara baada ya kutoka kuweka jiwe la msingi katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya Musoma wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali  ya maendeleo mkoani Mara.


Baadhi ya Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya Musoma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati akizungumza nao mara baada ya kutoka kuweka jiwe la msingi katika Hospitali ya Wilaya ya Musoma wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akifurahia jambo mara baada ya kuzindua Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya Musoma ambayo imewekwa jiwe la msingi na Waziri huyo wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akielekea kukagua majengo ya Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya Musoma wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evance Mtambi wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara. 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisisitiza jambo baada ya kukagua mashine ya x-ray wakati wa ziara yake ya kikazi katika mkoa wa Mara iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.


Mwonekano wa mashine ya x-ray iliyopo katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya Musoma mkoani Mara.

 


Mwonekano wa kitanda cha mgonjwa na mashine za kupima afya zilizopo katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya Musoma mkoani Mara.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisalimiana na Viongozi wa Mkoa wa Mara baada ya kuwasili mkoani humo kwa lengo la kufanya ziara ya kikazi ya kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kuzungumza na wananchi.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akitazama nyaraka za  mwananchi wa Halmashauri ya Wilaya Musoma aliyewasilisha changamoto yake  wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kuzungumza na wananchi.




No comments:

Post a Comment