Na. Veronica Mwafisi-Mara
Tarehe 01 Oktoba, 2024
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amesema uhusiano mzuri wa kidiplomasia na kiuchumi alio nao Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na nchi wahisani umechangia kwa kiasi kikubwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.
Mhe. Simbachawene amesema hayo leo
tarehe 1 Oktoba, 2024 wakati wa ziara yake ya kikazi
ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kusikiliza changamoto za
wananchi katika Mkoa wa Mara ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha
Mapinduzi.
Amesema
miradi hii mikubwa inayotekelezwa nchini haitokei kwa bahati mbaya bali ni
jitihada za Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutaka Tanzania iwe na
maendeleo.
“Tunamshukuru
sana Rais, Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uhusiano wake mzuri na nchi
wahisani ambao umewezesha kupata fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya
maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo miundombinu, elimu na afya,” Mhe.
Simbachawene ameongeza.
Mhe.
Simbachawene ametoa wito kwa watumishi wa umma na wananchi kuendelea kumuombea
Rais ili azidi kuwa na afya njema na kuweza kutafuta fedha kwa ajili ya miradi mingi
zaidi ya maendeleo.
Amepongeza
juhudi zinazofanywa na watumishi na wananchi wa Mkoa wa Mara kwa kutekeleza
miradi ya maendeleo kwa ufanisi katika mkoa huo na kuwasisitiza Viongozi wa
Mkoa wa Mara kuwahimiza wananchi wa mkoa huo kufanya kazi za uzalishaji kwa
bidii ili kujiongezea kipato.
“Mkoa
wa Mara mmefanya kazi kubwa sana, tuendelee kutekeleza na kusimamia utekelezaji
wa miradi hii ili kufikia lengo la Serikali ya Awamu ya Sita ya kuwa na
maendeleo katika nchi yetu.” Mhe. Simbachawene amesisitiza.
Amesema
changamoto zilizopo za upungufu wa watumishi na nyinginezo, Serikali
inazitambua na inazifanyia kazi.
Mhe. Simbachawene ameanza ziara hiyo katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma ambapo ameweka jiwe la msingi ujenzi wa hosptitali ya wilaya hiyo na kuzindua vyumba13 vya madarasa, matundu 17 ya vyoo na mabweni matano katika Shule ya Sekondari Songe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akifuatilia taarifa ya Mkoa wa Mara
na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika
mkoa huo wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua,
kuzindua
na kusikiliza changamoto za wananchi katika Mkoa huo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, Bw. Gerald Kusaya (aliyesimama
kulia) akisoma taarifa ya mkoa wa Mara na Utekelezaji wa miradi ya maendeleo wakati
wa ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene iliyolenga
kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisisitiza jambo wakati
akizungumza na Kamati
ya Usalama, Wakuu wa Idara, Wakuu wa Taasisi na Watumishi wa Sekretarieti ya
Mkoa wa Mara wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo.
Kamati
ya Usalama, Wakuu wa Idara, Wakuu wa Taasisi na Watumishi wa Sekretarieti ya
Mkoa wa Mara wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati akizungumza nao mara baada
ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika mkoa huo wakati
wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali
ya maendeleo.
No comments:
Post a Comment