Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene amemtembelea Mama Sitti Mwinyi nyumbani kwake Mikocheni Jijini Dar es Salaam leo Septemba 10, 2024.
“Rais, amenielekeza kuwafikishia
salaam zake na amesema yuko pamoja nanyi na ndio mana amenituma kufika hapa
nyumbani na kuwajulia hali, kusikiliza changamoto zilizopo na kuzitafutia
ufumbuzi” amesema Mhe. Simbachawene.
Mhe. Simbachawene amesema Rais Mhe. Dkt. Samia
anathamini sana mchango wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa waliomtangulia na
ataendelea kusimamia na kutunza familia hizo kwa mujibu wa Katiba na Sheria.
Aidha, Mama Sitti amemshukuru Mhe. Simbachawene kwa
kupata nafasi ya kumtembelea na kumjulia hali na amempongeza Rais Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan kwa kuendelea kuijali familia yake wakati wote bila kuchoka na
amemuombea kwa Mungu aendelee kutumia hekima na busara katika kuiongoza Tanzania.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja
na Mama Sitti Mwinyi wakati alipomtembelea nyumbani kwake Mikocheni Jijini Dar
es Salaam Septemba 10, 2024
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene akifurahia jambo na Mama Sitti
Mwinyi wakati alipomtembelea nyumbani kwake Mikocheni Jijini Dar es Salaam
Septemba 10, 2024
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene akisalimiana na Mama Sitti
Mwinyi wakati alipomtembelea nyumbani kwake Mikocheni Jijini Dar es Salaam
Septemba 10, 2024
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene akifurahia jambo na Mama Sitti
Mwinyi wakati alipomtembelea nyumbani kwake Mikocheni Jijini Dar es Salaam
Septemba 10, 2024
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene wakifuatilia jambo na Mama
Sitti Mwinyi wakati alipomtembelea nyumbani kwake Mikocheni Jijini Dar es
Salaam Septemba 10, 2024
No comments:
Post a Comment