Na. Lusungu Helela- Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene ametoa rai kwa wananchi
kuwa wafuatilliaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika simu zao za
kiganjani ili kujipatia huduma nyingi za
kijamii zitolewazo na Serikali
Ametoa kauli hiyo leo
Jumatano Julai 19, 2024 wakati akifungua Maadhimisho na Maonesho ya Wiki ya
Utumishi wa Umma yaliyoanza Juni 16 katika Viwanja vya Chinangali jijini
Dodoma.
Mhe.Simbachawene
amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
amekuwa akisisitiza matumizi ya TEHAMA katika kuwawezesha wananchi kupata
huduma zitolewazo na Serikali kwa haraka, uwazi na bila kuwa na urasimu
Kufuatia hatua hiyo
amesisitiza wananchi kutumia simu zao ili kupata huduma hizo badala ya kujikita
kuangalia pekee michezo ya kubashiri na tamthilia kupitia simu zao za kiganjani
Amesema lengo la kuhakikisha
huduma za serikali zinapatikana kupitia simu za kiganjani ni kuona wananchi
wanapata huduma bora zenye gharama nafuu na kwa haraka katika mikoa na wilaya
zote tofauti ilivyokuwa miaka ya nyuma
Wakati huo huo, Mhe.Simbachawene
amewataka Watumishi wa Umma kutumia mifumo ya TEHAMA iliyobuniwa na Serikali ili
kurahisisha utoaji huduma na kuondoa malalamiko kwa wananchi wanaowahudumia
Katika hatua nyingine Mhe. Simbachawene amewataka watumishi ambao hawajajisajili na kujaza mipango kazi katika Mfumo wa Upimaji wa Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma (PEPMIS) wawe wamekamilisha kabla ya wiki ijayo ili kila mmoja awe ameingia kwenye mfumo huo.
“Kabla sijahitimisha hotuba yangu nitoe maelekezo yafuatayo, Watendaji wote wahakikishe watumishi ambao bado hawajajisajili kwenye Mfumo wa Upimaji wa Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma (PEPMIS) wawe wamefanya kazi hii ili mpaka wiki ijayo jambo hili liwe limeshakwisha kabisa na kila mmoja awe ameingia kwenye mfumo.” Amesema Mhe. Simbachawene
Maadhimisho ya Wiki ya
Utumishi wa Umma kitaifa yanaratibiwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora ambapo kwa mwaka huu, Wizara na Taasisi mbalimbali za
serikali zinatoa huduma za papo kwa hapo ikiwemo hati za viwanja, vitambulisho vya uraia na huduma nyinginezo katika Viwanja vya
Chinangali Park.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akizungumza na watumishi
mbalimbali wa Serikali pamoja na wananchi walioshiriki kwenye Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa
yamefanyika katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.
Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, wakimsikiliza Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe.George Simbachawene wakati wa Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa
yamefanyika katika Viwanja vya Chinangali
Jijini Dodoma.
Sehemu ya Wananchi na Watumishi wa Umma, wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene
wakati wa Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa
yamefanyika katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Mhe. Ridhiwani
Kikwete akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene kuzungumza na Wananchi
na Watumishi mbalimbali walioshiriki kwenye Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi akitoa utambulisho wa
Viongozi waliohudhuria kwenye Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.
Sehemu ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene
wakati wa Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa
yamefanyika katika Viwanja vya Chinangali
Jijini Dodoma.
Sehemu ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe.George Simbachawene wakati wa Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa
yamefanyika katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.
Wakuu wa Taasisi,
Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Viongozi wa dini wakimsikiliza Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe.George Simbachawene (hayupo pichani) wakati wa Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma uliofanyika Jijini
Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akipokelewa na Naibu
Waziri wa Ofisi yake, Mhe. Ridhiwani Kikwete mara baada ya kuwasili kwenye Viwanja
vya Chinangali kwenye Ufunguzi wa Maadhimisho ya
Wiki ya Utumishi wa Umma Jijini
Dodoma. Katikati yao ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri. Wa kwanza
kulia ni Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano, Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bi. Mary Mwakapenda akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene pamoja na Viongozi wa ofisi hiyo wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma. Wapili kutoka kulia ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akiwa kwenye picha ya
pamoja na Makatibu Wakuu wa
Wizara mbalimbali mara baada ya Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika
katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Bw. Xavier
Daudi akifurahia jambo na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, ambaye ni Mkuu
wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri. Katikati ni Mkurugenzi wa Kitengo
cha Mawasiliano, Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bi. Mary Mwakapenda.
No comments:
Post a Comment