Na. Lusungu Helela- Dodoma
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amezitaka Taasisi za Umma kuweka mipango madhubuti ya kutumia mifumo ya kidijitali ambayo italeta mageuzi ya kiutendaji na kuifanya Tanzania kuendana na mapinduzi ya nne ya viwanda yanayotumia TEHAMA.
Ametoa kauli hiyo leo Jumapili, Juni 23 , 2024 jijni Dodoma katika viwanja vya Chinangali Park wakati akimwakilisha Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma na Uzinduzi wa mifumo ya kidijitali iliyosanifiwa na kujengwa na Ofisi ya Rais-UTUMISHI.
Amezitaka Taasisi hizo kufuatilia na kuhimiza matumizi ya mifumo hiyo kwa Watumishi wanaowaongoza.
Amesema uzinduzi wa mifumo hiyo ya kidijitali ni utelelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi ambapo Serikali itaweza kuwahudumia wananchi kwa uwazi na kwa haraka zaidi.
Ameitaja mifumo iliyozinduliwa kuwa ni HR Assesment, PEPMIS na PIPMIS, e-Watumishi (HCMIS) pamoja na e-Mrejesho.
Amesema mifumo hiyo ikitumika ipasavyo itasaidia kuwabaini Watumishi mahiri na watumishi wazembe pamoja na kuongeza uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika utumishi wa umma.
"Mifumo hii ikitumiwa kama ilivyokusudiwa itasaidia kuwabana Watumishi wazembe na hivyo kuongeza uwazi uwajibikaji na ufanisi katika kuwahudumia wananchi " amesisitiza Mhe.Majaliwa
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amewapongeza vijana wazawa kwa ubunifu wa kusanifu mifumo hiyo huku akiutaja mfumo wa e-Mrejesho uliotambulika kimataifa kutokana na ubora wake.
Akizungumzia Wiki ya Utumishi wa Umma amesema moja ya lengo lake ni kuhimiza uwajibikaji, uwazi, uadilifu pamoja na utoaji huduma bora kwa wananchi
"Hongereni sana Taasisi za Umma kwa utayari wenu wa kutoa huduma kwa wananchi kuanzia Juni 16 hadi leo hii siku ya Kilele" amesisiiza Waziri Mkuu.
Amesema kitendo cha kufanyika kwa maonesho hayo ni dalili tosha kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imejizatiti kutoa huduma bora za papo kwa hapo kwa wananchi pasipo wananchi kulazimika kuzifuata huduma hizo maofisini.
Kwa upade wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ys Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amesema matumizi ya TEHAMA katika Utumishi wa Umma yameondoa usumbufu, rushwa pamoja na kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi.
Amesema mifumo hiyo imesanifiwa na kujengwa na wazawa ukiwemo mfumo wa e-Watumishi (HCMIS) ambao una uwezo wa kuhifadhi taarifa za watumishi wa umma kuanzia siku aliyoajiriwa hadi siku ya kustaafu.
Amesema mfumo wa upimaji wa utendaji kazi kwa watumishi na taasisi PEPMIS na PIPMS umesaidia kuondoa upendeleo na uonevu na unahamasisha utendaji kazi miongoni mwa watumishi.
Naye Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, UTUMISHI, Bw.J uma Mkomi amesema matumizi wa Mifumo ya Utendaji Kazi ikiwemo PEPMIS na PIPMIS imeonekana kuwa ni kikwazo kwa baadhi ya Watumishi kwa sababu Watumishi wengi hawapendi kubanwa
Bw. Mkomi amesema mtumishi yeyote ambaye hatojaza majukumu yake kwenye mfumo huo hatopata ruhusa ya kuhama wala kwenda masomoni pamoja na kutopanda cheo
Katika hatua nyingine Bw. Mkomi amesema Mfumo wa e-mkopo umewarahisishia Watumishi wa Umma kupata mkopo kwa haraka na pia mfumo huo hautoi fursa kwa Watumishi kukopa benki nyingine endapo Mtumishi atakuwa na mkopo katika benki nyingine.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Katiba, Sheria na Utawala Bora, Mhe. Frolent Kyombo ameipongeza Ofisi ya Rais-UTUMISHI kwa usanifu na kujenga mifumo hiyo ya Kidijitali kwani imesaidia kupunguza usumbufu na gharama kwa watumishi wa Umma wa kufuatilia huduma Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu Mifumo ya Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Sera za Tehama na Viwango, Bw. Ibrahim Toure wakati alipotembelea banda la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma na Uzinduzi wa mifumo ya kidijitali iliyofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi mbalimbali wa Serikali pamoja na wananchi walioshiriki kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma na Uzinduzi wa mifumo ya kidijitali yaliyofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.
Sehemu ya watumishi mbalimbali wa Serikali pamoja na wananchi walioshiriki kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma na Uzinduzi wa mifumo ya kidijitali wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa yaliyofanyika kitaifa katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akitoa
neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa kuzungumza na Wananchi na Watumishi
mbalimbali walioshiriki kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma na Uzinduzi wa mifumo ya kidijitali yaliyofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akitoa utambulisho wa Viongozi
waliohudhuria kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma na Uzinduzi wa mifumo ya kidijitali iliyofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akitazama Nyaraka za Kiutumishi wakati alipotembelea banda Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma na Uzinduzi wa mifumo ya kidijitali iliyofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mhifadhi Mkuu wa Malikale Bw. William Mwita wakati alipotembelea banda la Wizara ya Maliasili na Utalii kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma na Uzinduzi wa mifumo ya kidijitali iliyofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akipiga makofi mara baada ya kuzindua
Mifumo ya Utendaji Kazi Serikalini wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma na Uzinduzi wa mifumo ya kidijitali iliyofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma. Wengine ni Viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Watendaji wengine wa Serikali.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akimkabidhi Tuzo ya Usanifu na Ujenzi wa
Mifumo ya Kielektroni katika Utumishi wa Umma Bw. Ibrahim Mrisha wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya
Wiki ya Utumishi wa Umma na Uzinduzi wa
mifumo ya kidijitali iliyofanyika
Kitaifa katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.
Sehemu ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa
Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma na Uzinduzi wa mifumo
ya kidijitali iliyofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa
Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Mussa Magufuli akizungumza jambo na
Wakurugenzi wasaidizi wa Ofisi hiyo wakati
wa Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma na Uzinduzi wa mifumo
ya kidijitali iliyofanyika Kitaifa
katika Viwanja vya Chinangali Jijini
Dodoma. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya
Mikataba ya Utendaji Kazi Serikalini, Bi. Zainabu Kutengeza.
Kwaya ya TAKUKURU
ikitumbuiza wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Wiki
ya Utumishi wa Umma na Uzinduzi wa mifumo ya kidijitali iliyofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment