Thursday, June 20, 2024

WADAU WA SERA YA MAFUNZO KATIKA UTUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUTOA MAONI YANAYOENDANA NA KASI YA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA

 Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais -UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi amewataka Wadau wa Sera ya Mafunzo katika Utumishi wa Umma kutoa maoni ya utekelezaji wa Sera hiyo ya Mwaka 2013 yanayoendana na kasi ya mabadiliko ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano yanayotokea Duniani kote katika ufanyaji kazi.

Bw. Daudi ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Juni 20, 2024 wakati akifungua kikao kazi cha siku mbili cha Wadau hao kilichowahusisha Maafisa Tawala na Maafisa Utumishi kutoka kwenye Wizara, Taasisi za Umma na Halmashauri mbalimbali nchini kwa lengo la kupata maoni ya Utekelezaji wa Sera ya Mafunzo  katika Utumishi wa Umma  ya Mwaka 2013.

Amesema maoni watakayoyatoa ni muhimu yakazingatia mabadiliko makubwa yanayotokea duniani ambapo kazi nyingi zinakwenda kufanywa na mashine huku kukiwa na uhitaji mdogo sana wa rasilimaliwatu.

"Hakikisheni maoni mtakayoyatoa yanaakisi mabadiliko makubwa yanayotokea kwenye Teknolojia ya Habari na Mawasiliano hususan matumizi ya akili bandia ambapo huko tuendako kazi nyingi zinaenda kupotea" amesisitiza Mhe. Kaimu Katibu Mkuu Daudi

Amesema Sera ya Mafunzo katika Utumishi ya Umma ya Mwaka 2013 imepitwa na wakati na imeshindwa kujibu changamoto zilizopo kwa sasa katika Utumishi wa Umma kutokana na mabadiliko makubwa ya matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano inayoendelea kubuniwa na kutumiwa katika Utumishi wa Umma.

Kufuatia hatua hiyo, Bw. Daudi amewasisitiza wadau  hao kutoa maoni yatakayojikita  zaidi  katika matumizi ya mifumo ya TEHAMA ili kuhakikisha rasilimaliwatu itakayozalishwa inatoa huduma kwa uwazi na  haraka  kwa wananchi.

Katika hatua nyingine, Bw. Daudi amewataka wadau hao kuhakikisha wanafanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo katika Utumishi wa Umma ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za serikali kwa wakati huku akiwasisitiza kutumia mifumo ya TEHAMA inayotumika kwa sasa katika Utumishi wa Umma.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo na Uendelezaji Sera, Bi. Judith Shoo amemhakikishia Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi kuwa maoni yatakayotolewa yatakuwa na tija na yatadumu kwa muda mrefu kwa maslahi mapana katika Utumishi wa Umma wenye matokeo makubwa kwa taifa.


Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi akizungumza na Wadau ambao ni Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala kutoka kwenye Wizara, Taasisi za Umma na Halmashauri mbalimbali nchini wakati wa kikao kazi cha kupata maoni ya utekelezaji wa Sera ya Mafunzo katika Utumishi wa Umma ya mwaka  2013 kinachofanyika kwa muda wa siku mbili  kuanzia leo  Jijini Dodoma.

Baadhi ya Wadau ambao ni Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala  wa kutoka kwenye Wizara na Halmashauri mbalimbali nchni wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi wakati wa kikao kazi cha kupata maoni ya utekelezaji wa Sera ya Mafunzo katika Utumishi wa Umma 2013 kilichoanza leo jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo na Uendelezaji Sera, Bi. Judith Shoo akizungumza kabla ya kumkaribisha Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw.Xavier Daudi kufungua kikao kazi  cha  Wadau ambao ni Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala  wa kutoka kwenye Wizara, Taasisi  za Umma na Halmashauri mbalimbali nchini ili kupata maoni ya utekelezaji wa Sera ya Mafunzo  katika Utumishi wa Umma ya mwaka  2013 kilichofanyika leo Jijini Dodoma

 

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi  akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua kikao kazi cha Wadau cha kupata maoni ya utekelezaji  wa Sera  ya Mafunzo  katika Utumishi wa Umma  ya Mwaka 2013 kinachofanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia leo jijini Dodoma.

Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo na Uendelezaji Sera, Bi. Judith Shoo mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kufungua kikao cha Wadau ambao ni Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala wa kutoka kwenye Wizara, Taasisi za Umma na Halmashauri mbalimbali nchini cha kupata maoni ya utekelezaji wa Sera ya Mafunzo katika Utumishi wa Umma ya mwaka 2013 kilichofanyika leo jijini Dodoma.

Baadhi ya Wadau ambao ni Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala  wa kutoka kwenye Wizara na Halmashauri mbalimbali nchni wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi wakati wa kikao kazi cha kupata maoni ya utekelezaji wa Sera ya Mafunzo katika Utumishi wa Umma 2013 kilichoanza leo jijini Dodoma.

 




No comments:

Post a Comment