Friday, June 28, 2024

OFISI YA RAIS, UTUMISHI NA UTAWALA BORA YAWAASA WATUMISHI WA UMMA KUACHA KUCHEZA KAMALI


Na. Lusungu Helela - Dodoma

Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imesema sio maadili kwa Watumishi wa Umma kucheza kamali ikwemo michezo wa kubashiri (betting) kwani inatweza utumishi wao katika jamii.

Kauli hiyo imetolewa leo Ijumaa Juni 28, 2024 katika Ofisi ya Mtumba jijini Dodoma na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Usimamzi wa Maadili, Bw. Ally Ngowo wakati wa utoaji wa Semina ya kuwajengea uwezo Watumishi wa Ofisi hiyo mahali pa kazi

Amesema Mtumishi wa Umma ni kioo katika jamii hivyo kujihusisha kucheza kamali kunapelekea Mtumishi kushindwa kuwahudumia wananchi na wakati mwingine kupata msongo wa mawazo endapo atapoteza fedha kwenye kamari

Katika hatua nyingine, Bw. Ngowo amesema sio maadili kwa Watumishi wa Umma kukopa fedha bila mpangilio.

Amefafanua kuwa baadhi ya watumishi wamekuwa wakikopa pasipokuwa na malengo, hivyo wakijikuta na madeni mengi yasiyokuwa na ulazima, hali inayowafanya kushindwa kufanya kazi zao ipasavyo.

Kwa upande wake Mtaalamu wa Saikolojia, Dkt. Chris Mauki amesema katika maisha ya kila siku mabadiliko hayaepukiki na kama hawatayakubali mabadiliko hayo ni lazima watumishi wapate changamoto ya afya ya akili.

"Miili yetu haijaumbwa kupokea mabadiliko yanayotokea katika maeneo yetu ya kazi na maisha kwa ujumla na hivyo tumejikuta tukipata changamoto ya afya ya akili " amesema Dkt. Chris Mauki

Amesema kiasili binadamu wote ni woga wa mabadiliko na hiyo imepelekea binadamu kupambana na mabadiliko yasitokee hali inayopelekea kujikuta kwenye msongo wa mawazo na muda mwingine kupata matatizo makubwa.

Awali Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, SACP. Ibrahim Mahumi amesema mafunzo hayo yameletwa kwa vile Watumishi wa Ofisi hiyo wana kazi nyingi ambazo zimekuwa zikiwaletea msongo wa Mawazo hivyo mafunzo ni muhimu ili waweze kuwa wastahimilivu.

‘’Hapa kuna msongo wa mawazo sana hivyo mafunzo haya ya afya ya akili ni muhimu ili kuweza kuepukana nayo’’ amesisitiza Kaimu Katibu  Mkuu, SACP. Ibrahim Mahumi

Naye Daktari Bingwa wa Macho, Joshua Yeuze kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa akiwasilisha mada kuhusu Magonjwa Sugu yasiyoambukiza (Sukari na Presha ya Macho) akitoa semina ya magonjwa hayo amewaasa Watumishi wa Umma kujenga utamaduni wa kupima angalau kwa mwaka mara moja ili kujua hali za afya zao

‘’Hakikisheni mnafanya mazoezi mara kwa mara pamoja na kula chakula bora ili kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza’’ amesema Dkt. Yeuze

Katika hatua nyingine Mchunguzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Stephew Agwanda wakati akiwasilisha mada kuhusu Mkakati wa Taifa dhidi ya Rushwa amewaasa Watumishi hao kujiepusha vitendo vya rushwa mahali pa kazi


Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - UTUMISHI, SACP. Ibrahim Mahumi akizungumza na watumishi wa ofisi hiyo (hawapo pichani) wakati akifungua semina ya kuwajengea uwezo watumishi mahali pa kazi iliyofanyika katika ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma.


Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – UTUMISHI, SACP. Ibrahim Mahumi (hayupo pichani) wakati akifungua semina ya kuwajengea uwezo watumishi mahali pa kazi iliyofanyika katika ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma.

Sehemu ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Dkt. Chris Mauki wakati akiwasilisha mada ya Mabadiliko ikiwemo kipengele cha afya ya akili kwenye semina ya kuwajengea uwezo watumishi mahali pa kazi iliyofanyika katika ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma.


Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakimsikiliza Dkt. Joshua Yeuze wakati akiwasilisha mada kuhusu Magonjwa Sugu yasiyoambukiza (Sukari na Presha ya Macho) kwenye semina ya kuwajengea uwezo watumishi mahali pa kazi iliyofanyika katika ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma.


Mtaalam wa Saikolojia, Dkt. Chris Mauki akiwasilisha mada ya mabadiliko kwenye kipengele cha afya ya akili kwenye semina ya kuwajengea uwezo mahali pa kazi watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora iliyofanyika katika ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma.


Daktari Bingwa wa Macho, Joshua Yeuze kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa akiwasilisha mada kuhusu Magonjwa Sugu yasiyoambukiza (Sukari na Presha ya Macho) wakati wa semina ya kuwajengea uwezo mahali pa kazi watumishi wa ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora iliyofanyika katika ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma.


Sehemu ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakimsikiliza Dkt. Joshua Yeuze wakati akiwasilisha mada kuhusu Magonjwa Sugu yasiyoambukiza (Sukari na Presha ya Macho) kwenye semina ya kuwajengea uwezo watumishi mahali pa kazi iliyofanyika katika ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma.


Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Usimamizi wa Maadili, Ofisi ya Rais - UTUMISHI, Bw. Ally Ngowo alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu Maadili katika Utumishi wa Umma wakati wa semina ya kuwajengea uwezo watumishi mahali pa kazi iliyofanyika katika ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma.


Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Usimamizi wa Maadili Ofisi ya Rais - UTUMISHI, Bw. Ally Ngowo akiwasilisha mada kuhusu Maadili katika Utumishi wa Umma wakati wa semina ya kuwajengea uwezo mahali pa kazi watumishi wa ofisi hiyo iliyofanyika Mtumba jijini Dodoma.


Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakimsikiliza Mchunguzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Stephew Agwanda (hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu Mkakati wa Taifa dhidi ya Rushwa wakati wa semina ya kuwajengea uwezo watumishi mahali pa kazi iliyofanyika katika ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma.


Mchunguzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Stephew Agwanda akiwasilisha mada kuhusu Mkakati wa Taifa dhidi ya Rushwa kwenye semina ya kuwajengea uwezo mahali pa kazi watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora iliyofanyika katika ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma.


Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakimsikiliza Mchunguzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Stephew Agwanda (hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu Mkakati wa Taifa dhidi ya Rushwa wakati wa semina ya kuwajengea uwezo watumishi mahali pa kazi iliyofanyika katika ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma.

 



 

No comments:

Post a Comment