Saturday, June 22, 2024

KATIBU MKUU MKOMI AFURAHISHWA NA TAASISI KUJITOKEZA KWA WINGI KUTOA HUDUMA KWENYE WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

 Na. Veronica Mwafisi- Dodoma  

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi amefurahishwa na Taasisi za Umma kujitokeza kwa wingi kushiriki na kutoa huduma za Kiserikali papo kwa hapo kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma huku akitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kutembelea Maonesho hayo.

Bw. Mkomi ameyasema hayo wakati alipotembelea mabanda na kujionea huduma zikitolewa na Wizara na Taasisi mbalimbali zilizoshiriki kwenye maonesho hayo yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Maonesho hayo yaliyoanza Juni 16 yanatarajiwa kuhitimishwa siku ya kesho Juni 23, ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi.

Maadhimisho na Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kitaifa yameratibiwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambapo Kaulimbiu ya Mwaka huu ni “Kuwezesha kwa Utumishi wa Umma uliojikita kwa Umma wa Afrika ya Karne ya 21 iliyojumuishi na inayostawi; Ni Safari ya Mafunzo na Mabadiliko ya Kiteknolojia”.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akipata maelezo kuhusu kitabu kilichokuwa kinatumika na Serikali ya Kikoloni (Mwingereza) wakati alipotembelea katika banda la Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yanafanyika jijini Dodoma.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Juma Mkomi akifurahia jambo na watumishi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) alipotembelea Viwanja vya Chinangali kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yanafanyika jijini Dodoma.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Juma Mkomi akizungumza na mtumishi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) alipotembelea Viwanja vya Chinangali kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yanafanyika jijini Dodoma.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akizungumza na watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii alipotembelea Viwanja vya Chinangali kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yanafanyika jijini Dodoma.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Juma Mkomi akisisitiza jambo kwa watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma alipotembelea Viwanja vya Chinangali kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yanafanyika jijini Dodoma.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Juma Mkomi (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano, Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bi. Mary Mwakapenda mara baada ya Katibu Mkuu huyo kuwasili katika Viwanja vya Chinangali Park kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea kufanyika Jijini Dodoma.




No comments:

Post a Comment