Na.
Mwandishi wetu-Dodoma
25 Septemba, 2023
Katika michezo hiyo ya kusisimua iliyopangwa kufanyika Mkoani
Iringa, Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora imepeleka wachezaji 46 ambao
watashindana katika michezo ya mpira wa miguu, netiboli, baiskeli, pamoja na
riadha.
Mwaka 2014, Ofisi hiyo ilishiriki katika michezo hiyo na
kufanikiwa kunyakua ubingwa, ambapo tangu mwaka huo haikuweza kushiriki tena
hadi mwaka huu.
Akizungumza wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa kwa ajili ya
kuwaaga wanamichezo hao 46 waliochaguliwa kwa ajili ya kuipeperusha bendera ya
Ofisi hiyo katika michezo ya mwaka huu, Bi. Mavika amewahimiza wawakilishi hao
kuhakikisha wanakwenda kupambana kikamilifu ili kurejesha heshima ya Ofisi hiyo
katika michezo hiyo.
“Kwanza kabisa napenda kuwapongeza kwa kuchaguliwa kuiwakilisha
Ofisi katika michezo ya SHIMIWI ya mwaka huu, kwani Ofisi hii ina watumishi
wengi lakini mmechaguliwa nyinyi, hivyo ni lazima mjue mmepewa heshima kubwa
sana ya kutuwakilisha,” amesema.
Pamoja na kuwataka wakacheze kikamilifu na kurudi na ubingwa, Bi
Mavika amewaasa watumishi hao kuonyesha nidhamu ya hali ya juu, ndani na nje ya
uwanja.
“Lazime mkumbuke mnakwenda kuiwakilisha Ofisi yenye heshima ya
juu sana katika Serikali yetu, hivyo mnapaswa kuwa mfano wa kuigwa na wengine,”
ameongeza.
Hata hivyo, amewatia moyo kwamba uongozi wa Ofisi hiyo utasimama
bega kwa bega na wachezaji hao katika kipindi chote cha mashindano, na kuwataka
wasisite kuwasiliana na uongozi wa Ofisi pale watakapokutana na changamoto
yeyote.
Kwa upande wake, mwakilishi wa timu hiyo, Bw. Charles Shija,
ameishukuru Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa kuwaamini na
kuwapatia huduma nzuri katika kipindi chote cha maandalizi.
“Tunajua Ofisi kwa sasa ina vipaumbele vingi na vya muhimu sana
vya kutekeleza, lakini pamoja na hayo mmeona umuhimu wa kuturuhusu na
kutuwezesha kushiriki katika mashindano ya mwaka huu, tunaahidi hatutawaangusha,”
amesisitiza Bw. Shija.
Aidha, amesema wachezaji wote wana afya nzuri na wamepata muda
mzuri wa kufanya mazoezi chini ya makocha hodari hivyo wana uhakika wa ushindi
na kurudi na ubingwa.
1. Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,UTUMISHI, Bi.
Leila Mavika akizungumza wakati wa hafla
fupi iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwaaga wanamichezo 46 waliochaguliwa kushiriki kwenye Mashindano ya
Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) mwaka huu
yanayofanyika kitaifa mkoani Iringa.
1. Mwakilishi wa timu ya Wanamichezo kutoka Ofisi
ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Charles Shija akizungumza wakati wa hafla
fupi iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwaaga wanamichezo 46 waliochaguliwa kushiriki
kwenye Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali
(SHIMIWI) mwaka huu yanayofanyika kitaifa mkoani Iringa ambapo ametumia fursa
hiyo kuishukuru Menejimenti ya Ofisi ya Rais-UTUMISHI kwa imani kubwa waliyonayo
kwao.
1. Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Utawala kutoka Ofisi
ya Rais-UTUMISHI, Bi. Nyasinde Mukono akizungumza wakati wa hafla fupi
iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwaaga wanamichezo 46 waliochaguliwa kushiriki kwenye Mashindano ya
Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) mwaka huu
yanayofanyika kitaifa mkoani Iringa.
1. Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi.
Leila Mavika akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kuzungumza na
wanamichezo 46 wakati wa hafla fupi
iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwaaga wanamichezo hao waliochaguliwa kushiriki
kwenye Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali
(SHIMIWI) mwaka huu yanayofanyika kitaifa mkoani Iringa.
1. Sehemu ya wanamichezo wakimsikiliza Kaimu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Leila Mavika wakati wa hafla fupi
iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwaaga wanamichezo hao 46 waliochaguliwa kushiriki
kwenye Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali
(SHIMIWI) mwaka huu yanayofanyika kitaifa mkoani Iringa.
1. Sehemu ya wanamichezo wakimsikiliza Kaimu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Leila Mavika wakati wa hafla fupi
iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwaaga wanamichezo hao 46 waliochaguliwa kushiriki
kwenye Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali
(SHIMIWI) mwaka huu yanayofanyika kitaifa mkoani Iringa.
No comments:
Post a Comment