Sunday, September 3, 2023

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YAFANYA ZIARA TGFA

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akizungumza jambo wakati yeye na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria walipofanya ziara kikazi katika Ofisi za Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) zilizopo jijini Dar es Salaam, tarehe 2 Septemba, 2023.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwakaribisha katika Ofisi za Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa ziara yao ya kikazi katika ofisi hizo zilizopo jijini Dar es Salaam, tarehe 2 Septemba, 2023.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakipata maelezo kutoka kwa mmoja wa watendaji wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) kuhusu utekelezaji wa majukumu ya ofisi hiyo wakati ziara ya kikazi ya wajumbe hao katika ofisi hizo jijini Dar es Salaam, tarehe 2 Septemba. 2023.Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na Wajumbe wa kamati hiyo baada ya kuhitimisha ziara ya kikazi kwenye Ofisi za Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) jijini Dar es Salaam, tarehe 2 Septemba, 2023..

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akifurahia majadiliano kutoka kwa Wajumbe wa kamati hiyo wakati wa ziara ya kikazi kwenye Ofisi za Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) jijini Dar es Salaam, tarehe 2 Septemba, 2023.


 

No comments:

Post a Comment