Na. Rainer Budodi-Dodoma
Tarehe 22 Septemba, 2023
Naibu Waziri Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete amewasisitiza watumishi wa umma kushughulikia hoja na malalamiko ya
wananchi kwa wakati ili kuwapunguzia Viongozi wa
Kitaifa adha ya kushughulikia masuala ambayo yangeweza kumalizwa katika vituo
vya kutolea huduma.
“Sote tumeshuhudia namna ambavyo kunakuwa na mabango
yenye malalamiko wakati wa ziara za Viongozi wa Kitaifa. Hii inaashiria kuwa
watendaji wetu katika vituo vya kazi hawatekelezi
majukumu yao ipasavyo na hivyo kusababisha wateja kutafuta suluhisho sehemu nyingine” amesisitiza.
Mhe. Ridhiwani amesema hayo wakati akifunga kikao kazi cha kubadilishana uzoefu kuhusu
masuala ya maadili na utawala bora kilichowashirikisha wadau kutoka Taasisi
Simamizi za Maadili ya Utendaji, Taasisi Simamizi za Maadili ya Kitaaluma na
watumishi kutoka kwenye Wizara mbalimbali na taasisi za kitaaluma katika ukumbi wa PSSSF-Makole
Dodoma.
Aidha, Mhe.Ridhiwani ametoa rai kwa
washiriki hao kufanyia kazi kwa vitendo masuala waliyojifunza katika siku hizo mbili
ili kuendana na maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan ya kuwa na Watumishi wa Umma ambao ni Waadilifu na wenye kuwajibika
kwa hiari.
Ameongeza kuwa wataalamu wa ofisi yake kwa kushirikiana na Taasisi
Simamizi za Maadili katika Utumishi wa Umma wanafanyia kazi hoja na changamoto
mbalimbali kuhusu usimamizi wa maadili, nidhamu na michakato ya ajira ili
kuondoa malalamiko yaliyopo na kuleta ufanisi zaidi.
Naye, Kaimu Katibu Mkuu Bi. Leila
Mavika amesema Ofisi ya Rais UTUMISHI na Utawala Bora itaendelea kushirikiana
na wadau kutoka Taasisi Simamizi za Maadili ya
Utendaji, Taasisi Simamizi za Maadili ya Kitaaluma na watumishi kutoka kwenye
Wizara mbalimbali na taasisi za kitaaluma kutoa
ushauri wa kitaalamu pale itakapohitajika,
kujenga uelewa kuhusu maadili
ya Utumishi wa Umma na
kushirikiana na wadau hao kuleta
mabadiliko ya fikra miongoni mwa watumishi wa umma.
Kwa upande wake Mwakilishi wa
Mamlaka Simamizi za Maadili ya Kitaaluma Bi. Jane Mazigo ameishukuru ofisi ya
Rais UTUMISHI na Utawala Bora kwa kuandaa mafunzo haya muhimu kwa wadau kutoka Taasisi Simamizi za Maadili ya Utendaji, Taasisi
Simamizi za Maadili ya Kitaaluma na watumishi kutoka kwenye Wizara mbalimbali
na taasisi za kitaaluma.
“Mhe. Naibu waziri tumejifunza mambo mengi na tuko tayari kuelimisha kundi kubwa la watumishi wa umma kuzingatia masuala ya nidhamu na Uadilifu kazini. Kundi hili limejifunza masuala muhimu na kwa watu muhimu na sisi hatutokuangusha” alisisitiza.
Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete akifunga kikao kazi cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili
na utawala bora kilichowashirikisha wadau kutoka Taasisi Simamizi za Maadili ya
Utendaji, Taasisi Simamizi za Maadili ya Kitaaluma na watumishi kutoka kwenye
Wizara mbalimbali na taasisi za kitaaluma katika Ukumbi wa PSSSF Jijini Dodoma
tarehe 22 Septemba, 2023.
Sehemu
ya washiriki wa kikao kazi cha kubadilishana
uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora wakimsikiliza Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa
akizungumza wakati wa kufunga kikao kazi hicho katika
Ukumbi wa PSSSF Jijini Dodoma tarehe 22 Septemba, 2023.
Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Ofisi ya Rais- UTUMISHI Bi.
Leila Mavika wakifuatilia kwa makini salamu za shukurani kutoka kwa Mwakilishi
wa Mamlaka Simamizi za Maadili ya Kitaaluma Bi. Jane Mazigo katika Ukumbi wa
PSSSF Jijini Dodoma tarehe 22 Septemba, 2023.
Mwakilishi
wa Mamlaka Simamizi za Maadili ya Kitaaluma Bi. Jane Mazigo akitoa salaamu za
shukurani kwa niaba ya washiriki kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati wa kufunga
kikao kazi cha Taasisi Simamizi za Maadili ya Utendaji, Taasisi Simamizi za
Maadili ya Kitaaluma na watumishi kutoka kwenye Wizara mbalimbali na taasisi za
kitaaluma kilichofanyika Jijini Dodoma tarehe 22 Septemba, 2023.
No comments:
Post a Comment