Saturday, September 16, 2023

MHE. SIMBACHAWENE AWASIHI WANANCHI KUTUNZA MIRADI INAYOTEKELEZWA NA SERIKALI KATIKA MAENEO MBALIMBALI

Na. Rainer Budodi-Geita

Tarehe 16  Septemba, 2023 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amewasihi wananchi kuthamini na kutunza miradi inayotekelezwa na Serikali ikiwemo ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika maeneo yao kwa kuwa ina lengo la kuondoa umaskini katika jamii. 

Mhe. Simbachawene ameyasema hayo alipokuwa akizungumza kwa nyakati tofauti na wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na Wananchi kwa ujumla katika Halmashauri za Wilaya ya Geita, Chato na Bukombe Mkoa wa Geita.

“Nimetembelea na kukagua miradi iliyopangwa, kwa ujumla nimefurahi sana kwa utekelezaji mzuri mathalani shule na vituo vya afya vimejengwa kwa viwango vizuri. Hivyo, nitoe rai kwa halmashauri zote nchini na wananchi kuhakikisha miradi hiyo inatunzwa kwa kuwa ni sehemu ya chaguo na vipaumbele vya wananchi wenyewe katika maeneo yao” amesema Mhe. Simbachawene. 

Aidha, Mhe. Simbachawene ameongeza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa moyo mmoja ametoa fedha nyingi kupitia mpango huo ili ziwafike wanufaika na wananchi kwa jumla kupitia miradi hiyo ambayo ni chachu ya maendeleo. Hivyo, ameomba wananchi kuendelea kumuombea ili aendelee kuwa na moyo wa huruma na unyenyekevu kwa maendeleao ya wananchi wake. 

“Umaskini si kukosa fedha tu, unaweza pia kuwa ni ukosefu wa elimu na afya bora. Kwa kuwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni mtu wa maono amegusa sehemu hizo na kuhakikisha shule nzuri na vituo vya afya kama vilivyojengwa mkoani Geita kupitia Mradi huo vinakamilika haraka na kuanza kutumika” amesema Mhe. Simbachawene. 

Vilevile, Mhe. Simbachawene amewasisitiza Waratibu wa TASAF katika Mkoa wa Geita kuhakikisha shule na vituo vya afya vinavyojengwa kupitia Mradi huo wa TASAF vinawekewa miundombinu ya maji na umeme na kuweka madawati ili madarasa hayo yaanze kutumika. 

Waziri Simbachawene amehitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma mkoani Geita na kusikiliza changamoto zinazowakabili ili kuzitatua na kukagua miradi inayotekelezwa na TASAF katika Halmashauri za Geita, Chato na Bukombe katika Mkoa huo.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akikagua mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya cha Nyabilezi, kilichopo katika Kijiji cha Nyabilezi, Kata ya Bukome, Halmashauri ya Wilaya ya Chato kilichofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) chini ya Mpango wa OPEC awamu ya nne wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Geita.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na watumishi wa Kituo cha Afya cha Nyabilezi na wananchi wa Kijiji cha Nyabilezi Kata ya Bukome, Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Geita.

Sehemu ya watumishi wa Kituo cha Afya cha Nyabilezi na wananchi wa Kijiji cha Nyabilezi, Kata ya Bukome, Halmashauri ya Wilaya ya Chato wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Geita.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisisitiza jambo kwa watumishi wa Kituo cha Afya cha Nyabilezi na wananchi wa Kijiji cha Nyabilezi Kata ya Bukome, Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Geita.


Pichani ni mradi wa ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) la Zahanati ya Ishololo, Kata ya Lyambamgongo, Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita lililofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) chini ya Mpango wa OPEC awamu ya nne.


Pichani ni mradi wa ujenzi wa jengo la darasa la shule ya Msingi Ihulike Kata ya Ushirombo, Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita lililofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) chini ya Mpango wa OPEC awamu ya nne.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akipata maelezo toka kwa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Dkt. Eugene Rutayisire kuhusu Kituo cha Afya cha Nyabilezi, kilichopo katika Kijiji cha Nyabilezi, Kata ya Bukome, Halmashauri ya Wilaya ya Chato kilichofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) chini ya Mpango wa OPEC awamu ya nne wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Geita.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akimsikiliza mlengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Kijiji cha Nyabilezi, Kata ya Bukome, Halmashauri ya Wilaya ya Chato alipokuwa akitoa ushuhuda wa namna alivyonufaika na TASAF wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Geita.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (pichani katikati) akielekea kukagua mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Mkungo, Kata ya Bukome, Halmashauri ya Wilaya ya Chato ulifadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) chini ya Mpango wa OPEC awamu ya nne wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Geita.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akitoa maelekezo kwa Watendaji na Viongozi wa TASAF na wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Mkungo, Kata ya Bukome, Halmashauri ya Wilaya ya Chato ulifadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) chini ya Mpango wa OPEC awamu ya nne wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Geita.

 


 

No comments:

Post a Comment