Naibu Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete amewasisitiza watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi
kuendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi na ubunifu ili tija ya kazi zao iweze
kuonekana kupitia huduma bora wanazozitoa kwa wananchi.
“Ninatamani kuona utendaji kazi wenu unazingitia misingi ya maadili ya utendaji katika utumishi wa Umma kwani ndiyo msingi wa mageuzi kuelekea maendeleo endelevu vinginevyo watumishi wazembe na wenye mienendo isiyofaa kimaadili mwisho wao umefika.” alisisitiza Mhe. Ridhiwani.
Aidha,
amewakumbusha watumishi hao kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan anasisitiza uadilifu kazini na ametoa haki na stahiki
mbalimbali kwa watumishi, hivyo, Serikali kupitia Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora imekamilisha mapitio, kusanifu na kuanza
kujenga mifumo ya utendaji kazi Serikalini ili dhana ya wajibu pia iweze
kutekelezeka kwa ufanisi.
Pia, Naibu Waziri
huyo amezitaka Mamlaka za Ajira na Nidhamu kuendelea kusimamia haki na stahiki
zote za watumishi na kuachana na kasumba ya utendaji wa mazoea. Pia, amesema
Mamlaka za Ajira na Nidhamu zirejee Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298
ambayo inaonesha kuwa madaraka kuhusu ajira, kuthibitishwa kazini, mafunzo,
kupandishwa cheo, nidhamu hadi hitimisho la kazi kwa mtumishi wa umma
yalishagatuliwa na hivyo kushindwa kutekeleza wajibu huo ni kielelezo cha
kushindwa kutekeleza majukumu waliyopewa.
Katika hatua
nyingine Mhe. Ridhiwani amezitaka Halmashauri nchini kuhakikisha zinaendeleza
miradi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF kwa kuwa ni chaguo na imeridhiwa
na wananchi wenyewe katika maeneo yao. Iwapo Halmashauri na TASAF zitaunganisha
nguvu ni rahisi kuwakomboa wananchi katika umaskini.
“Ninaelekeza
walengwa wote wenye sifa za kunufaika na TASAF wasilipwe fedha nusu
nusu kwa kuwa lengo ni kuwatoa katika wimbi la umaskini” alisema Mhe.
Ridhiwani.
Naye, Mkuu wa
Wilaya ya Manyoni Mhe. Kemilembe Lwotta ameomba pongezi zifike kwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta
watumishi wapya wa kada mbalimbali 228 na wote wameripoti kazini na watumishi
289 walimu na wasio walimu wamepandishwa vyeo na 15 wamebadilishiwa vyeo.
Vilevile,
ameongeza kuwa wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Itigi katika vijiji
vyote 39 wananufaika vyema na uwepo wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF kwa
kiwango kikubwa kwa kuwa kaya masikini zimefikiwa na zinawezeshwa kujikwamua
kiuchumi.
Kwa upande wake
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi Bw. John Mgalula pamoja
na shukurani alizotoa kwa Serikali, ameomba Serikali kuendelea kutoa vibali vya
ajira ili watumishi waongezeke na utoaji huduma kwa umma uimarike.
Mhe. Ridhiwani
amehitimisha ziara yake ya siku moja tarehe 25 Agosti, 2023 katika Halmashauri
ya Wilaya ya Itigi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi na kukagua
utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri hiyo.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi mkoani Singida kwenye kikao kazi ambapo amewataka kufanya kazi kwa weledi na ubunifu katika kuwahudumia wananchi.
Sehemu ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi mkoani Singida wakimsiliza Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati alipofanya ziara mkoani humo kwa lengo la kuwataka Watumishi hao kufanya kazi kwa weledi na ubunifu katika kuwahudumia wananchi.
Mkuu
wa wilaya ya Manyoni Mhe.Kemilembe Lwotta akizungumza na Watumishi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Itigi mkoani Singida kwenye kikao kazi kabla ya
kumkaribisha Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete na Watumishi
hao ambapo amewataka kufanya kazi kwa weledi na ubunifu katika
kuwahudumia wananchi.
Naibu Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani
Kikwete akisalimia na Katibu Tawala wa wilaya
ya Manyoni ,Bw. James Mchembe mara baada ya kuwasili katika Halmashauri
hiyo kwa lengo la kuzungumza na watumishi ambapo amewataka kufanya kazi kwa
weledi na ubunifu katika kuwahudumia wananchi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Itigi,Bw. John Mgalula akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.
Ridhiwani Kikwete kuzungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Itigi mkoani Singida kwenye kikao kazi ambapo amewataka Watumishi kufanya
kazi kwa weledi na ubunifu katika kuwahudumia wananchi.
Naibu Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani
Kikwete akiandika changamoto zinazowakabili Watumishi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi mkoani Singida kwenye kikao kazi
alichokifanya leo mkoani humo ambapo amewataka kufanya kazi kwa weledi na
ubunifu katika kuwahudumia wananchi.
No comments:
Post a Comment