Na. Veronica Mwafisi-Kwimba
Tarehe 04 Agosti, 2023
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amewataka Makatibu Tawala wa Wilaya kutekeleza majukumu yao kikamilifu ikiwepo kusimamia suala la nidhamu ili kutenda haki na kuondoa changamoto za kiutumishi.
Mhe. Simbachawene amesema
hayo alipokuwa akizungumza na watumishi wa umma wa Wilaya ya Kwimba, Mkoa wa Mwanza
wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji na kutatua kero na
changamoto zinazowakabili watumishi wa umma katika Wilaya hiyo.
“Makatibu Tawala, msidhani
ya kuwa mamlaka ya nidhamu hayapo kwenu, mmechaguliwa kuwa viongozi kwa lengo
la kuondoa changamoto kati ya waajiri na waajiriwa, hivyo mna jukumu kubwa la
kusimamia suala hilo” amesisitiza Mhe. Simbachawene.
Aidha, Mhe. Simbachawene
amesema ni vema viongozi wa Wilaya wakafahamu changamoto mbalimbali za
watumishi na wananchi na kuzishughulikia ili kuondoa tabia ya baadhi ya
watumishi kutaka kuchukua majukumu ambayo hawahusiki nayo.
Akitoa neno la shukrani, Mkuu wa
Wilaya ya Kwimba, Mhe. Ng’wilabuzu Ludigija amemshukuru Waziri Simbachawene kwa
kufanya ziara ya kikazi katika Wilaya yake na kuzungumza na watumishi kwa lengo
la kuhimiza uwajibikaji ambapo ameahidi kwa kushirikiana na watumishi wa wilaya
hiyo watatekeleza maelekezo yote ambayo amewaagiza.
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene yupo katika ziara ya kikazi mkoani Mwanza yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma, kutatua
changamoto zinazowakabili watumishi wa umma pamoja na kukagua utekelezaji
wa Miradi ya TASAF.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
akizungumza na watumishi wa Wilaya ya Kwimba, mkoani Mwanza wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga
kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma.
Sehemu ya watumishi wa Wilaya ya Kwimba, mkoa
wa Mwanza wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya
kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili
watumishi wa Wilaya hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Amos Makalla mara baada ya
kuwasili katika ofisi za Mkuu wa Mkoa huyo wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri
Simbachawene iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto
zinazowakabili watumishi wa umma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
akisalimiana na baadhi
ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, mara baada ya kuwasili katika ofisi
hizo wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua
changamoto zinazowakabili watumishi wa Wilaya hiyo.
Sehemu ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza, wakimsikiliza
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. George Simbachawene (aliyeshika kipaza sauti) alipokuwa akizungumza na
watumishi hao wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na
kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa Wilaya hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Kwimba, mkoani Mwanza, Bi. Hapiness Msanga akiwasilisha taarifa ya
hali ya Watumishi katika Wilaya yake kabla ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
kuzungumza na watumishi wa Wilaya ya Kwimba, mkoani Mwanza wakati wa ziara yake
ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili
watumishi wa umma.
Mtumishi wa Wilaya ya Kwimba, Bi.
Lyidia Bitaliho akiwasilisha hoja kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo mkoani Mwanza iliyolenga kuhimiza uwajibikaji
na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao.
No comments:
Post a Comment