Saturday, August 5, 2023

WAZIRI SIMBACHAWENE AWASISITIZA WAAJIRI KUINGIZA TAARIFA ZA WATUMISHI KWENYE MFUMO WA HCMIS ILI KUEPUSHA MALALAMIKO YA KIUTUMISHI

 Na. Veronica Mwafisi-Misungwi

Tarehe 05 Agosti, 2023

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amewasisitiza waajiri serikalini kuingiza taarifa za watumishi kwenye Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) ili kuboresha masuala ya kiutumishi na kuepusha malalamiko ya watumishi.

Mhe. Simbachawene amesema hayo alipokuwa akizungumza na watumishi wa umma wa Wilaya ya Misungwi, Mkoa wa Mwanza wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua kero na changamoto zinazowakabili watumishi wa umma katika Wilaya hiyo.

Mhe. Simbachawene amesema, Ofisi ya Rais-UTUMISHI imetengeneza mifumo mingi lakini mfumo mama ni wa HCMIS ambao kupitia huo, Serikali itakuwa na takwimu sahihi za watumishi zitakazosaidia kutatua changamoto mbalimbali za kiutumishi ikiwemo masuala ya malimbikizo ya mishahara na kupanda madaraja.

Ametoa rai kwa Maafisa Utumishi kufuatilia na kuingiza taarifa za watumishi zilizo sahihi tu kwenye mfumo huo wa HCMIS kwani zikiingizwa taarifa ambazo si sahihi zitagoma kuingia.

Akitoa neno la shukrani, Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mhe. Paulo Chacha amemshukuru Waziri Simbachawene kwa kufanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Misungwi na kuzungumza na watumishi kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji ambapo ameahidi watayafanyia kazi maelekezo yote ambayo Waziri Simbachawene amewapatia ili kuzidi kuboresha utumishi wa umma nchini.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amehitimisha ziara yake ya kikazi katika mkoa wa Mwanza iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma, kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma pamoja na kukagua utekelezaji wa Miradi ya TASAF.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na watumishi wa Wilaya ya Misungwi, mkoani Mwanza wakati wa ziara yake ya kikazi   iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma waliopo katika mkoa wa Mwanza.


Sehemu ya watumishi wa Wilaya ya Misungwi, Mkoa wa Mwanza wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa Wilaya hiyo.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mhe. Paulo Chacha mara baada ya kuwasili katika ofisi za Mkuu wa Wilaya huyo wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri Simbachawene iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisalimiana na Viongozi wa wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Misungwi mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, mkoani Mwanza wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, mkoani Mwanza, Bw. Joseph Mafuru akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa halmashauri yake kabla ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuzungumza na watumishi wa Wilaya ya Misungwi, mkoani Mwanza wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma.


Mbunge wa Jimbo la Misungwi, Mhe. Alexander Mnyeti akitoa salamu za wananchi na watumishi wa jimbo lake la Misungwi kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kabla ya Waziri Simbachawene kuzungumza na watumishi wa Wilaya ya Misungwi, mkoani Mwanza wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma.


Mbunge wa Jimbo la Misungwi, Mhe. Alexander Mnyeti akitoa salamu za wananchi na watumishi wa jimbo lake la Misungwi kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kabla ya Waziri Simbachawene kuzungumza na watumishi wa Wilaya ya Misungwi, mkoani Mwanza wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma.



Mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Dkt. Clement Morabu akiwasilisha hoja kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo mkoani Mwanza iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (aliyeshika kipaza sauti) akisikiliza hoja ya Mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi (hayupo pichani) aliyoiwasilisha kwa Waziri huyo wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao.




No comments:

Post a Comment